Naam timu hizo zingekuwa na mafanikio labda tungewaamini. Kwa maoni yangu kwanza kabisa TFF iwe na sera kwamba timu zote za zinazoshiriki ligi kuu ziwe na timu za watoto na timu ambayo itashindwa kutimiza hili ipewe adhabu kali hata kuzuiliwa kushiriki kwenye ligi.
...kabla ya timu kubwa kuwa na timu za watoto, michezo ya UMISHUMTA, na UMISETA ipewe kipaumbele, kisha chipukizi/wanafunzi wenye vipaji huko 'walelewe kimafunzo zaidi' kwenye timu za daraja la kwanza ama la pili za mikoa yao...
Pili, nadhani kazi iliyofanywa na Maximo inatosha kabisa. Kiwango chake inaelekea kimefikia kikomo hana uwezo wa kuinyanyua juu zaidi Timu yetu zaidi ya hapo alipoifikisha, kwa hiyo inabidi kutafuta kocha mwingine mwenye uwezo zaidi ili ainue zaidi kiwango cha uchezaji cha timu yetu ya Taifa.
...kaka, hili tatizo linaanzia chini zaidi kuliko kiwango cha Maximo, tulikuwa na kina Mwinga Mwanjala, kina Nzael Kyomo, Zakayo Mwarekwa, kina Filbert Bayi, Nyambui na Shahanga huko kwenye Riadha,...hao wote walikuwa wanamichezo walotokea kwenye chimbuko la UMISETA, leo hii hebu taja mwanariadha hata mmoja ambaye hata akija Michael Johnson (400m world record holder) anaweza kutusaidia?
kwenye masumbwi tulikuwa na kina Emmanuel Mlundwa, Benjamin Mwangata, Isangura bros, Makoye na Willy, tulikuwa na kina Nassor Michael, Aloyce Ng'itu, familia ya kina Matumla... wengi wao walitokea Arnatouglo Hall, leo hii hatuna hata bondia mwenye kiwango hata cha kutuletea medali kwenye All african games... wapi michezo ya Majeshi?
Serikali ikitaka, tutaweza pata kina
Edibily Lunyamila na
Dua Saidi wengi tu huko UMISHUMTA na UMISETA... nia tu ikiwepo...
Tatu, migogoro ndani ya vilabu vyetu hasa Simba na Yanga inarudisha sana maendeleo ya soka Tanzania. TFF iweke mikakati ya kupambana na migogoro ndani ya vilabu hasa vilabu hivi viwili vikongwe. Sijui kiifanywe nini ili kuimaliza kabisa migogoro hii. Labda kuwe na adhabu kwamba klabu ambayo inakuwa na migogoro kila kukicha labda ipigwe faini kwa kuwa migogoro hiyo haizoreteshi klabu pekee bali hata soka la Tanzania. Haya ni maoni tu. Hongera timu ya Taifa mmejitahidi kadri ya uwezo wenu.[/B]
...Simba na Yanga ya miaka hii, haina tofauti sana na ile Simba na Yanga miaka ya kina Jabir Shikamkono na kina Ali Kiluvia, yaani kuziba zibia viraka kwa kusajili wachezaji toka mikoani... kina Mavumbi Omar, kina Yussuph Ismail Bana etc... Kama unakumbuka PAMBA enzi zao kina Masatu, Ngassa, Marsha, Fumo Felician, John Makelele wooote hawa walitokea mikoani na vipaji vyao, kama ilivyokuwa kwa vilabu vingine kama TUKUYU Stars, Majimaji Songea, nk...
Ni wakati wa kina Tostao, Adolph Rishard, Peter Tino, Pondamali na wengineo tu ndipo Dar es salaam nao walijitapa 'watoto' wa mjini kuunda timu ya taifa. Kwa mtizamo huo, bado naamini sana mafanikio ya timu ya taifa hayatatokana na Simba na Yanga tu, bali Mikoa yote Tanzania nzima, ndio maana naona umuhimu sana wa TAIFA CUP.
Kumtimua Maximo ni kumuonea tu, serikali kama ilivyo kwa sekta nyingine,
imeshindwa kuweka mikakati ya kuendeleza vipaji kwenye michezo!