Habari wakuu,
Hapa nakusudia mwanamke mwenye mtoto ambaye si wako, Mtoto ambaye kwa kiasi kikubwa bado anahitaji ukaribu na mama yake.
Nimeshuhudia ndoa ya Jirani yangu ikiyumba baada ya mtoto wa miaka takribani miwili na nusu au mitatu Kuletwa nyumbani na mkewe kwani wamekaa wastani wa miezi 3 bila ya mtoto huyo kuwepo.
Tatizo ninaloliona ni utundu wa huyo mtoto ambao wakati mwingine unasababishwa na kudekezwa na mama yake.
Mfano siku moja aliiburuza chini Iphone ya baba yake mlezi, akafokewa na baba huyo, Jambo hilo lilisababisha mama akasirike kwa madai kuwa baba hampendi mtoto.
Je changamoto gani nyingine za kuoa mwanamke mwenye mtoto mdogo?