Changamoto katika mfumo wa PEPMIS

Changamoto katika mfumo wa PEPMIS

digodigo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
311
Reaction score
254
Huu mfumo bado haujakaa sawa kwani kuna mambo kadhaa yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi.

Kwanza katika siku zilizopendekezwa au mara nyingi ukifungua mtandao huu speed au kasi ya ufungukaji ni ndogo hadi inakatisha tamaa sijui ni kasi ya inteneti iliyopo haikidhi mahitaji ya taasisi zinazojaza au mfumo tulionao wa 4G umeelemewa kiasi kwamba taasisi zote za serikali zinapojaza basi kasi inakuwa ndogo.
kuna haja wahusika wakalitazama hili.

Pili kuna kuwa na mkanganyiko wa muingiliano wa taasisi yaani unaweza fungua na kukuta majina ya watu usiowafahamu na details zao na wakati mwingine hata kazi zako usizione hii pia ni changamoto.

Nafikiri kuna haja zaidi ya kulitazama hili.
 
Tumeamua kuingia kwa kasi sana. Ilitakiwa kwanza taasisi chache zianze kwa ajili ya majaribio kisha nyingine zifuate baadae. Hii kila taasisi na halmashauri kuutumia huu mfumo na miundombinu ya kimtandao haijakaa sawa bado. Ila mdogomdogo tutafika.....
 
Ni kweli kabisa,, portal Yao Ina shida,, japo sisi watumishi wa Huku vijijini tunaendelea kupambana maana wanasema kama mtumishi hutafikisha 60% basi huwezi kupanda Daraja mwaka huu
 
Aliyebuni hili limfumo alaaniwe yeye na kizazi chake,ameleta mambo ya kijinga afu ya uwongo!mi nmejiwekea sub task zangu 10,leo wameleta majina eti inatakiwa nijaze task 32,sasa sijui zimetoka wapi😲😲🙄
 
Back
Top Bottom