Changamoto katika ujenzi: Mafundi uchwara wanavyoharibu kazi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kama hujaanza ujenzi hasa wa nyumba yako ya kwanza ya kuishi jitahidi sana upate elimu ya kutosha kwenye
Ununuzi wa ardhi/kiwanja
Mafundi wa kila idara
Makisio ya vifaa, ufundi
Muda sahihi wa kuanza ujenzi
Nini cha kuanza kufanya nknk
Fanya utafiti wa kutosha.. Pata makisio ya ujenzi kwa kila hatua kwa mafundi tofauti
Ukiachana na changamoto za kuongezewa gharama kwenye vifaa na gharama za ufundi ama kuibiwa kwa vifaa vilivyokwisha nunuliwa kuna hili la kuharibiwa kazi
Na kazi iliyoharibiwa ina changamoto kubwa zaidi za kurekebisha kuliko kazi mpya
Kuna mengi sana ya kuambiana hapa lakini machache makubwa ni haya
1. Usifanye malipo ya ardhi/kiwanja bila kujihakikishia umiliki wake, migogoro, mipaka nk
2. Usifanye malipo bila kujihakikishia serikalini ramani ya mipango miji
3. Usianze ujenzi bila kufanya ibada ya kutakasa ardhi.. Ukishindwa hapo basi ibada ya kuitakasa nyumba
4. Usianze ujenzi bila kujihakikishia sehemu salama ya kuweka vifaa vyote vitakavyohusika kwenye ujenzi
5. Usianze ujenzi kwa kufanya mkupuo wa manunuzi.. Anza na vitakavyohitajika kwa wakati huo tu.. Na kama kina baadhi utavipata mapema kwa bei nzuri kaa navyo mwenyewe
6. Piga kenchi ukiwa umejihakikishia uwepo wa mabati
7. Usifanye wiring kama hakuna mtu anayekaa hapo.. Utajuta
8. Usiiache nyumba tupu/peke yake unapoelekea kumaliza ujenzi wa awali
9. Kumbuka gharama za finishing ndio kaburi la pesa😂 hivyo jiandae
10. Jihadhari na majirani...😀🤔🙇🏿‍♂.... Wakati wa ujenzi na utakapohamia.. Kuna jirani anaweza kuwa rafiki wakati wa ujenzi lakini akaja kuwa adui mkubwa utakapohamia
 
Hiyo ni kweli kwenye ujenzi mafundi uchwara wanahalibu sana. Yahitaji umakini sana. Kuna nyumba nyingne ukiitizama vizuri jinsi ilivyo pauliwa paa limelalia upande kabisa. Na kama unavojua gharama ya nyumba ipo kweny kupaua na finishing
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…