KERO Changamoto kubwa kwa Wanafunzi wa Masters IAA: Matokeo, Appeals na Dissertation

KERO Changamoto kubwa kwa Wanafunzi wa Masters IAA: Matokeo, Appeals na Dissertation

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kutumia jukwaa hili kueleza changamoto kubwa zinazowakumba wanafunzi wa ngazi ya Masters katika Chuo cha IAA. Kwa masikitiko makubwa, namna wanafunzi wa Masters wanavyotendewa haiakisi hadhi ya elimu ya juu, wala misingi ya haki na taaluma.

1. Matokeo (SAP, SUPP na Appeals)
Kumekuwa na tatizo kubwa kwenye utoaji wa matokeo. Wanafunzi wanapewa SAP ambazo hazina maelezo ya wazi wala mantiki ya kitaaluma. Baadhi ya wanafunzi wanakuwa na SAP nyingi bila kufahamu kosa halisi walilofanya.

Katika hatua ya appeal, mwanafunzi analazimika kulipa TZS 50,000 kwa kila somo, lakini kinachorudishwa mara nyingi ni majibu ya jumla ya “SUPP” bila mabadiliko wala ufafanuzi wa kitaaluma. Hali hii inajenga hisia kuwa mchakato wa appeal haulengi kusahihisha makosa, bali ni chanzo cha mapato.

2. Mfumo wa Matokeo na Uadilifu
Mfumo wa matokeo unaonekana kuwa na mapungufu makubwa ya kiutendaji na uadilifu:

- Kuna wanafunzi ambao hawajawahi ku-submit dissertation, lakini wanawekewa F kwenye mfumo; jambo linaloibua swali, mtu anafeli nini kama hakuwasilisha kazi?

- Wapo wanafunzi wenye SUPP mbili tu, lakini status inawekwa DISCO, na wanapofuatilia wanaambiwa “mfumo umemisbehave”. Cha kushangaza, mfumo huo huo haujawahi “kumisbehave” kwa wanaopata A zote.

- Kuna wanafunzi ambao hawajawahi kufanya defence au wamefanya re-defence, lakini majibu hayajatolewa kwa muda mrefu bila sababu za msingi, huku idara husika zikirusha lawama kati yao.

3. Rushwa Kwenye Dissertation
Kilio kikubwa zaidi ni tuhuma nzito za rushwa katika mchakato wa dissertation. Kuna malalamiko kuwa mwanafunzi analazimika kutoa fedha kwa baadhi ya wahusika au panel ili apite. Wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha huzungushwa, hufeli au huendelea ku-re-defend bila maelezo ya kitaaluma yanayoeleweka. Hili linadidimiza thamani ya shahada ya Masters na kuharibu sifa ya chuo.

Hitimisho
Kwa ujumla, hali hii inawadhalilisha wanafunzi wa Masters, inadidimiza ubora wa elimu, na kuharibu taswira ya Chuo cha IAA. Tunaiomba menejimenti ya chuo na mamlaka husika (kama TCU na Wizara ya Elimu) kuchukua hatua za haraka kuchunguza na kurekebisha mifumo hii kwa haki, uwazi na uwajibikaji.

Nawasilisha kwa masikitiko makubwa, nikitumaini sauti za wanafunzi zitasikilizwa.

Na kingine mtu anakuwa amefanya test eti inapotea anakosa course work anaambiwa arudie tena mtihani , graduetion ilikuw iwe dec mwaka jana wakasema wameghairisha hadi mwezi wa pili ili changamoto zote zifanyiwe kazi ila hadi sasa ni kimya hakuna tamko.

Pia soma:

~ Uongozi wa IAA, tafadhali chukueni kwa uzito suala la weledi, maadili ya ufundishaji na usimamizi wa mitihani
~ Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) boresheni huduma zenu za online, zinatukwaza Wanafunzi
~ Serikali ya wanafunzi chuo Cha uhasibu Arusha (IAA) main campus - Arusha umefanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi
~
Chuo cha uhasibu Arusha kinawalazimisha waombaji wajiunge chuoni hapo,hakuna option ya kuahirisha maombi,na wanachagua kozi ambazo hawajaomba
 
Mtu umedisco halafu unaleta uongo huku, we ulidhani elimu ya Master ni lele mama. Husomi unataka alama za mezani kwa nn usi disco. Mm mwenyew ni mwanafunzi wa master hapo IAA, watu zaidi ya 50 wamedisco kwa sababu ya mtu kuwa na supp zaidi ya nusu ya masomo. Nahisi na wew mleta mada upo kwenye kundi hilo kwa hyo ni wivu tu unakuponza ,kwan nani alikutama usisome. Tembelea chuo uone watu wanaofanya supp walivyo wengi, chuo cha IAA kinahitaji usome na sio lelemama.
 
Uzi umepuuzwa yaani tuliocomment ni wawili tu na ni muda mrefu tokea januari,duuh!
 
Back
Top Bottom