Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Bila kupoteza muda yafuatayo ni mapungufu ya club ya Yanga yanayopelekea ipate wakati mgumu uwanjani hasa inapocheza na timu zinazojitambua na zenye kutumia mfumo wa kujilinda.
1. Beki za pembeni zina mapungufu kwenye kushambulia. Mtazame Zimbwe halaafu linganisha na Boka utagundua Zimbwe is far better. Kama timu pinzani inakabia chini na ikiziba vizuri mianya ya kutomruhusu Boka kukimbia basi hapo habari inakuwa imekwisha, Boka anakuwa hana tija uwanjani. Na kwa upande wa kulia toka alivyoumia Kwasi Yao Kibwana na Mwena hawajaweza na hawataweza kufikia level za Kwasi kwenye kushambulia.
2. Viungo wa Yanga Aucho na Mudathiri wana kasi ndogo hali inayosababisha mashambulizi kuchelewa kufika mbele kwa wakati. Its true Aucho ni bora sana kwenye kumiliki na kuachia mpira lakini si mzuri kwenye kukimbia kwa kasi kwenda mbele. Mudathiri licha ya ubora wake kwenye kukaba, ana changamoto ya kuzubaa na kuchelewa kutoa "killer pass" hali inayopelekea kunyang'anywa mpira au kuwapa nafasi mabeki kuziba mianya.
3. Viungo washambuliaji wa Yanga wengi ni "ball dribbler", wanakaa sana mpira mguuni, hali inayowapa nafasi timu pinzani kublock mashambulizi kirahisi na inafanya timu kutabirika kirahisi. Pakome, Aziz Ki, Chama, Max, Mudathiri, Duke Abuya hawa wote wanapenda kukaa na mpira kwa sekunde kadhaa. Ningekuwa kocha wa Yanga ningewakemea viungo kuacha kucheza hii staili ya "anao anao" hasa Pacome. Kinyume na watani wao Simba eneo la katikati lina viungo wenye kasi na ni "gusa achia".
4. Yanga ipunguze wachezaji "ma father" msimu ujao. Ukiwa na ma father wengi kwenye timu, inakuwa hakuna wa kumtuma au kumkemea mwenzake uwanjani. Kila mtu mtemi. Pacome anapoteza mpira kizembe anaangaliwa tu, the likes of Aziz Ki na Max. Ni nadra sana timu kupata mafanikio ikiwa imejaa mastaa.
5. Dube sina haja ya kumzungumzia.
Niishie hapo.