Changamoto kubwa ya Yanga isiyosemwa na wachambuzi

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Bila kupoteza muda yafuatayo ni mapungufu ya club ya Yanga yanayopelekea ipate wakati mgumu uwanjani hasa inapocheza na timu zinazojitambua na zenye kutumia mfumo wa kujilinda.

1. Beki za pembeni zina mapungufu kwenye kushambulia. Mtazame Zimbwe halaafu linganisha na Boka utagundua Zimbwe is far better. Kama timu pinzani inakabia chini na ikiziba vizuri mianya ya kutomruhusu Boka kukimbia basi hapo habari inakuwa imekwisha, Boka anakuwa hana tija uwanjani. Na kwa upande wa kulia toka alivyoumia Kwasi Yao Kibwana na Mwena hawajaweza na hawataweza kufikia level za Kwasi kwenye kushambulia.

2. Viungo wa Yanga Aucho na Mudathiri wana kasi ndogo hali inayosababisha mashambulizi kuchelewa kufika mbele kwa wakati. Its true Aucho ni bora sana kwenye kumiliki na kuachia mpira lakini si mzuri kwenye kukimbia kwa kasi kwenda mbele. Mudathiri licha ya ubora wake kwenye kukaba, ana changamoto ya kuzubaa na kuchelewa kutoa "killer pass" hali inayopelekea kunyang'anywa mpira au kuwapa nafasi mabeki kuziba mianya.

3. Viungo washambuliaji wa Yanga wengi ni "ball dribbler", wanakaa sana mpira mguuni, hali inayowapa nafasi timu pinzani kublock mashambulizi kirahisi na inafanya timu kutabirika kirahisi. Pakome, Aziz Ki, Chama, Max, Mudathiri, Duke Abuya hawa wote wanapenda kukaa na mpira kwa sekunde kadhaa. Ningekuwa kocha wa Yanga ningewakemea viungo kuacha kucheza hii staili ya "anao anao" hasa Pacome. Kinyume na watani wao Simba eneo la katikati lina viungo wenye kasi na ni "gusa achia".

4. Yanga ipunguze wachezaji "ma father" msimu ujao. Ukiwa na ma father wengi kwenye timu, inakuwa hakuna wa kumtuma au kumkemea mwenzake uwanjani. Kila mtu mtemi. Pacome anapoteza mpira kizembe anaangaliwa tu, the likes of Aziz Ki na Max. Ni nadra sana timu kupata mafanikio ikiwa imejaa mastaa.

5. Dube sina haja ya kumzungumzia.

Niishie hapo.
 
Na hii kitu ndo inawasumbua sana Yanga.
 
Hongera sana Mkuu wewe unajua sana Mpira ni watu nadra sana nyie Hapa JF.

Yote uliyoyaandika ni kweli kabisa
Kwa kuongezea kidogo.

6. Sajili zinazofanywa na Engineer hapa karibuni ni unproductive.
Usajili wa Chama, Okra, Mkude, Mwenda Baleke hizi ni sajili za kukurupuka na kisiasa sana.

7. Uongozi kushindwa kuwa na makocha kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa Nabi linawatesa yanga.

8. Kushindwa kupata kiungo wa maana wa Ukabaji Aucho ni mzuri sana akicheza kwenye No 8 ni passer mzuri sana.
Yanga wanahitaji sana kiungo No 6

9. Waache Imani za Kishamba kila wakati Kupita Milango ya Nyuma .


Nikusahihishe kidogo hapo kwa Aucho.
No 6 anatakiwa kucheza Eneo dogo sana hatakiwi kuwa na Mbio wala Kutoka toka kwenye zone yake.
Muangalie kagoma ndio maana anafanya vizuri sana au ilivyikuwa Fabinho livapool.
Aucho ni mzuri akicheza 8 kama pacha yake kwa Bangala.

Thanks
 
Yaani Kagoma umlinganishe na Aucho? Aisee wewe jamaa
 
Yaani Kagoma umlinganishe na Aucho? Aisee wewe jamaa

Wewe sio muelewa so huwezi kuelewa kitu.

-Nimesema Kagoma anacheza Basic Footbal. Anatimiza majukumu yake kwa Asilimia 100
-Hatoki kuwalinda mabeki wake wa kati.
-Yeye ni kukaba kutengeneza nafasi na kuachia mpira kwa haraka.

Nikasema Aucho ni mzuri sana akicheza 8 ni mpigaji pasi mzuri mno.
Sijawafananisha kwa chochote

HUJAELEWA WAPI??????
 
Au kama ukitaka niwalinganishe na kuwatofautisha naweza nikakusaidia Mkuu
 
Timu Inaachawa wengi kuliko wachezaji ?
 
Utaambiwa utopolo ni bia bingwa full bundle.
 
Hakuna kitu Kagoma anaweza lingana na Aucho tuache uongo
 
Uko saw sana,yani sijui nani alishauri lomalisa aachwe, yanga kwa asilimia kubwa inabebwa na mzize kule mbele hakuna anaejituma zaidi yake! Pia idara ya mawasiliano imegeuza timu kuwa kama kijiwe cha taarabu inapoteza focus na concentration ally kamwe alifaa kuwa msemaji manara awe mhamasishaji
 
Hamna la maana blah blah as usual...soka la bongo mihemko zaidi kuliko uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…