B M F ICONIC
JF-Expert Member
- Jan 28, 2019
- 824
- 1,631
Kero na malalamiko wanayoyatoa wa Tanzania kuhusu changamoto kwenye Sekta ya Afya moja ya sababu ni Mifumo iliyowekwa huko nyuma kusimamia afya na kum chagua Mtu ambae hana maono / jicho la kutambua kero na Hajasomea Afya kusimamia Sekta ya Afya. Kwani yeye sio Daktari na hajawahi hashinda hospitalini 24hrs kuangalia changamoto zinazowakumba Wagonjwa/wa Tanzania
KWANINI angalau asichaguliwe Daktari mwenye uzoefu na aliekaa hospitalini akaziona na kukumbana na changamoto zilizo kwenye sekta ya afya, kwani ndio field yake na Kila siku anakaa na kushinda huko.Hivyo anazijua kero na wapi atatatua Akiwa waziri. Kuliko yule mtu ambae hashindi hospitali na upokea tu kero kwa wananchi bila kujua undani wa malalamiko hayo .
NB. Unaweza kukaa hospitali na wewe ni daktari lakini ukakosa jicho la kuona hii ni changamoto/ kero kwani wengi ujali zaidi matumbo yao na sio ujenzi wa taifa katika sekta ya Afya
Lengo ni ni kujenga na sio kubomoa, Ili kuhakikisha wa Tanzania wanapata huduma bora za Afya
Twende Direct kwenye Hoja zangu
1 kumekua na changamoto kwa watu waliopata ajali ya vyombo vya moto, uhalifu na kupata jeraha au ubakaji wanapofika hospitali na kuambiwa wale waliowaleta wakafate na kuja na PF3 (police form number 3) ndo huduma nyingine za kiafya zitolewe na hapo unakuta kijografia kituo cha polisi kipo umbali mrefu na hospitali ilipo.
Kwa mtu aliekaa hospitali kama mimi natambua na kuona hii ni kero.
Kwanini serikali kupitia wizara ya Afya isiweke/ kutenga ofisi inayotoa huduma za ki Polisi zinazo husiana na afya kwenye jengo la hospitali na kuajili polisi watakao kua maalum kutoa huduma kama hizo za PF3 hospitalin ili waepushe hio kero ya kufuatilia PF3 umbali mrefu ndo mgonjwa atibiwe
Mfano mtu alietendewa vitendo vya kikatili kama ubakaji inabidi akifika hospitalini humohumo kuna kitengo cha polisi ata fika na kuripoti tukio na kuelekezwa kwa Daktari amfanyie uchunguzi kisha ustawi wa jamii . Ambapo yote haya yakifanyika hospitalini. Kutaondoa usumbufu na kero ya " wewe nenda huku wakujazie fomu kisha rudi huku"
2 kumekua na malalamiko ya watu kutokupewa huduma za kiafya kwa kukosa Fedha au Bima ya afya. .ukiwatoa watoto walio chini ya miaka 5 na wajawazito. Kundi liliobaki hua linapata taabu pale inapotokea ameenda kutibiwa na hana fedha katika hospitali y serikali.. Kwani anaweza kusaidiwa vipimo bure na dawa akajinunulia au matibaba na vipimo bure ila dawa atajinunulia au upasuaji bure au dawa atajinunulia.
Na kweli kama mtu huyo ni kweli hajiwezi kiuchumi basi utakiwa aende ustawi wa jamii kujielezea wamsaidie/ aruhusiwe kutibiwa bure
Kwa mimi ninae kaa muda mwingi hospitali hii kwangu ni kero kwa wa Tanzania.
Kwanini serikali isiweke ofisi za ustawi wa jamii kwenye jengo la hospitali ili watoe huduma zianzo husiana na afya kwa wale walio chini kiuchumi na kuwaruhusu watibiwe kwani wao ndo wana mamlaka hio
Pia serikali inatambua kuna watu walio chini kiuchumi hivyo wakaanzisha TASAF ambayo inawatambua walengwa. Kwanini wakati wa bajeti bungeni wasiwatengeee fedha maalum au mfuko wa Bima maalumu kwa wana TASAF kwa matibabu yao na Afya ili waondoe malalamiko ya "wamekataa kunitibu au wamenipa huduma mbovu kisa sina pesa ya malipo" ma hospitalini..
3. Bima ya afya inakua haijitoshelezi kutoa huduma zote. Kuna dawa zina bei ghali ambazo hazilipiwi kwa bima , pia bima haitoi huduma fulan za upasuaji ambapo inabidi mgonjwa aongezee fedha na bima haitoi huduma ya vifaa tiba kama magongo na miwani.
Mfano; amekuja bodaboda kapata ajali na kuvunjika mguu. Hali yake kiuchumi ndo hio anategemea bodaboda. Inatokea amefanyiwa upasuaji kwa msaada na hospitali ili kuunganisha mifupa ila kwa sababu ya kiuchumi anakosa fedha y kuji hudumia ili anunue dawa au magongo hivyo kupelekea mguu wake kuoza au kupata mal formation ( mifupa kujiunga kwakujipinda) na hapo kakaa hospitalin kalibia miezi 2. Au mtu kavunjika/kuteguka/ Dislocation ila fedha za kulipia upasuaji ili waunganishe mifupa amekosa na kuamua kurudi nyumbani na kutumia tiba asili.
Mimi hii changamoto nimeishudia mahospitalini na naona ni kero katika huduma za afya katika nchii hii
Kwanini serikali isiunde Bima maalum kwa hili kundi la waendesha vyombo vya moto (bodaboda, maroli ,gari madereva) ili iwe maalum kwa kuwatibu endapp wakipata ajali na huduma watakazo zipata kipondi hicho.
Pia wahakikishe BIMA angalau ina toa huma zote za kiafya kwa watu wote kwani mpka leo ni changamoto
4. Kuna ile mgonjwa kalazwa na ana hali ya chini kiuchumi na hana ndugu ata wakumletea chakula au mgonjwa anatakikana kula vyakula fulan ili kuongeza madini mwilini ila anashindwa pa kuvipata au wagonjwa wa utapiamulo kulosa lishe bora
Ni iweke hivi; Nchi nyingine Africa mfano kenya kwenye hospitali na vituo vya kutolea Afya kuna kitengo kinacho husika na kutoa huduma za chakula mahospitalini (SIO CANTTEEN) Ila ni sera ya nchi kuto kukubali/kuruhusu vyakula vinavyopikwa nyumbani kuletewa wagonjwa. Kazi ya kitengo hicho ni spesho kwa kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa waliolazwa kila siku kuhakikisha wanapata balanced diet na chakula kinachokidhi matakwa ya kiafya kwa mgonjwa kwa wakati huo
Mfano mama mjamzito katokea nyumbani kuja hospitalini saa 4 usiku ili ajifungue au mgonjwa katoka kwenye oparesheni iliofanyika usiku chakula kinachoendan na hali yake ya kiafya atakipata wapi kwa muda huo. Kwani muda wa kuletewa wagonjwa chakula unajulikana
Ndo maana nchi nyingine pamoja na wazungu huwezi kukuta watu wamerundikana getini eti wanapelekea wagonjwa chakula. Huko kwao ni kwenda kusalimia na kumjulia hali tu.
Serikali ikijipanga katika hili na kuhakikisha Bill haiwi ya juu na iwe affordable au bure kwa wasiojiweza maana kuna scenario ndugu na jamaa wanatelekeza wagonjwa hospitali na kukosa pakula
Tanzania inatoa huduma bora ya afya na kuwalipa madaktari kwa wakati ndo maana husikii migomo ila nchi nyingini haya mambo madogomadog sijui ya bima, PF3,chakula... yamefanyiwa kazi ishu ipo kwenye kulipa mishahara.
Ila sisi tumekomaa na mamitambo makubwa ya afya na huduma za madaktari bingwa wakati huduma za kawaida na mifumo ya afya iiliopo nchini ina changamoto lukuki.
5 serikali iongeze elimu kuhusu Afya ya Akili na huduma zake katika vituo vya Afya na kuhakikisha wananchi wanapata na kujua cha kufanya wanapokumbwa na hali hiyo
Vitendo vya watu kujinyonga, kunywa sumu, kupata Stress/ sonona vipo kwenye jamii na wa TZ hawana uelewa wa kutosha juu ya Afya ya akili lwani nao ni ugonjwa kama ilivyo malaria
Huenda wewe ukawa Mjini ila kuna wenzako wa Tanzania wako mikoani ndanindani wanapitia Changamoto hizi kwenye Huduma za Afya.
#naendeleo hayana chama ni mtu kuweka maslahi na ujenzi wa nchi mbele, wengi wenye mamlaka wanawaza matumbo yao na sio maisha ya wa Tz na ujenzi wa Taifa
Mwenye kutoa maoni, ushauri, na kuongezea aongezee......