Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,107
- 9,272
Nu wajibu watu wazima na wazazi usikubali kituoni kuoanda gari bila wanafunzi kupanda.Kuna changamoto jana nilikutana nayo wakuu ya wanafunzi wasichana kama watano walinifata kituoni kuomba simu kuwapigia wazazi wao wawatumie nauli hata elfu mbili watoe wapande bajaji waende nyumbani ilikuwa mida ya saa mbili kasoro hivi maeneo ya relini na walikuwa wanaelekea Gongo la Mboto.
Na mara nyingi makonda wa daladala za G/Mboto kupitia hii njia ya Buza huwa wanakataa sanaa wanafunzi watoto wanakaa kituoni mpaka na watu wakubwa wengine gari zinakuja wala hawa wasemei au kuwapazia sauti hawa wanafunzi.
Na hizi mvua wanakaa vituoni mpaka saa tatu nimeona wanafunzi vituoni na magari yakija wanafungia milango kabisaa hata kituo cha kwa Azizi Ally wanafunzi wanaelekea Buza wanajaa pale kituo cha mafuta cha Oil com ambako gari husimama mpaka saa tatu na ugomvi makondakta wanafunga kabisaa milango wakiona wanataka kupanda