Changamoto wanazopitia wasaidizi wa kazi majumbani

Ni vyema sana ndugu ata Mungu ata kubariki sana
 
kweli kabisa ndugu wengine hutaka sifa tu kwa watu na kutesa vijana wa watu
 
kweli ndugu wanaweza kukumizia ata familia yako nakutokomea kusikojulikanana uko !
Inasikitisha sana ,kati ya watu ambao unatakiwa uishi nao vizuri ni hao wafanyakazi wa ndani ,ukiwa treat vibaya wanaweza wakafanya tukio la hatari ,ndio maana mimi huwa si entertain Hg.
 
Inaelekea we hujawahi kaa na hawa watu ila unafanya hadithi na porojo tu kwa sababu tu una bando.

Wapo maboss wabaya na wa hovyo. Pia wapo mabinti wabaya na wahovyo sana.

Nilitamani nizae watoto angalau 5 ila changamoto za watoto wa kazi ilininidi niishie 3 tu.

Ni mabinti 3 tu kati ya 12 nilio wahi kukaa nao ndio nilimudu kukaa nao zaidi ya 5yrs na kuondoka kwa heshima wawili wakiolewa kutokea kwangu na mmoja nilimtafutia kazi supermarket kwa rafiki yangu ambapo alikuwa anapata mshahara mara 6 zaidi ya kile nilichokuwa namlipa mimi na alihama kwangu baada ya kuwa amejijengea uwezo wa kulipia chumba na tuilimnunulia mahitaji mengine yamsingi ili kuanzia maisha.

Hao wote 3 mpaka leo wana familia zao na ni familia rafiki na yakwangu tukisaidiana kwa kila panapowezekana.

Hao 8 waliobaki ilikuwa ni changamoto sana kwani wapo waliokuwa wachawi, wazinzi ukiondoka anashinda kwa midume ama kuroroka usiku mkilala, wapo waliokuwa wezi, wapo waliokuwa kazi yao kulala tu na usomwambie kitu atashinda kavimba siku nzima, wapo waliokuwa wachavu na vikojozi na wadokozi wakati huohuo.

Mungu ni mwema sana ila wanagu wamepitia mapito ya kutisha na kuogofya ya mabinti wa kazi mpaka hapa walipofikia.

 
Porojo gani bibie? Nimeishi sana na mabinti tangu nikiwa mdogo kwetu na mpaka nimekua nimeishia nao kwangu na bado naishi nao, hapo point ni kwamba ukiishi na binti wa kazi ishi nae vzuri kama yeye hafai usiishi nae fukuza tafta mwingine mwenye unafuu, alichozungumza mtoa mada ni untanyasaji kwa mabinti, kuliko kumtukana binti, kumnyima mshahara, kumpiga na manyanyaso mengi bora uachane nae aende kwao, mm nimeongelea binti niliye nae kwa miaka hii, she is good lazima niishi nae vzuri sana sijawah kumnyanyasa binti na haitokuja kutokea nkigundua tu ana mambo mengi ya kunikera had kupelekea nimchukie siendelei kuishi nae
 
Uko vizuri sana ndugu na ubarikiwe sana sana !
 
Ila sasa usiombe HG akampenda baba mwenye nyumba,wanahisi Kali sana aisee
Kwasababu hayo mambo yapo sana ikitokea ntajua cha kufanya sababu unakuta kuna familia haiwezikaa bila HG, kuna familia hata kama hakuna HG maisha yanasonga, wengine lazima pawepo na HG kwakweli!! ukitoka kwenye mihangaiko saa tatu usiku hautaweza fanya chochote labda kama unarudhia kulala saa saba kila siku.
 
Tatizo baadhi ya waAfrika kwa waAfrika hawahurumiani,hawapendani!!
Haswa Akiwa ana hali na sauti ya juu!!!
Muogopeni Mwenyezzi MUNGU !!
 
Maelezo yako yana msingi sana .Ma housemaids hawana chombo cha kuwatetea zipo kesi ambazo unakuta anapata manyanyaso lakini hana pa kusemea,wengi wao hunyanyaswa katika nyanja zifuatazo:-
(1) Kusakamwa na familia nzima
-Watoto wanawadharau wazi wazi bosi (mwenye nyumba upo hukemei
-Mama anawaunga mkono watoto kwa kila wanachomsingizia housemaid
(2)kutowalipa kwa visingizio eti bosi anawawekea fedha zao na mwisho kuwarusha .
(3) Kwa baadhi kuwapa kazi za kuwadhalilisha mfano eti house girl anapewa nguo za ndani (Si ufue mwenyewe?).....nyumba nyingine INA watoto wakubwa hawajifunzi kazi za mikono akitoka shuleni,kwenye Mpira,matembezini anamrushia house girl minguo yake michafu (O.k analipwa ndio! kwa nini mtoto usisaidiane naye ili ujifunze kazi za mikono) Matokeo yake tunazalisha mabonge nyanya!
Jamani wanaitwa wasaidizi wa kazi za ndani haina maana kuwaachia kazi zote.
 
Mi wangu ananisaidia mno yani abarikiwe mno huyu binti, mwaka wa tano sasa nipo nae kanikuta nna mtoto mmoja sahivi watatu na wote amewalea yeye....yani hamna hata cha kumlipa huyu binti.
Jipe cheo.Malipo bora kabisaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…