Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Wasalaam Wakuu!.
Watoto ni baraka kubwa sana na kila mzazi angelipenda kuwa na watoto ili kujenga familia yenye furaha na amani. Watoto ni faraja kubwa sana kwa wazazi lakini muda mwingine ni changamoto sana.
Je, umewahi kukutana na changamoto ya watoto kuharibu mali na vitu vya thamani katika kipindi cha ukuaji wao? Tena kwa sababu ya utoto wake, huna cha kufanya. Unabaki kugugumia tu kwa maumivu.
Mimi ilinitokea hivi,
Smart Tv yangu ya LG, nimenunua zangu kwa Benson Electronics (Arusha), Tsh 2,700,000. Nikatumia kwa miezi miwili tu 😭😭😭.
Nipo sebuleni naagalia TV, mwanangu wa miaka minne aliwekewa Movie ya Jet Lee (sina hakika). Sasa kashazoea kuangalia mara nyingi sana. Movie ile ilikuwa ni ya kutumia majambia.
Mimi nipo zangu busy kumuangalia anavyocheza na mwiko mkononi, 'baba anafanya hivi'.
Najisemea moyoni, nimepata kidume. Atakuja kuwatandika watu mpaka washangae. Pasipo ya kujua nahatarisha amani ya moyo wangu kwa dakika chache zijazo.
Dogo anacheza mbele yangu, ili nimuone vizuri. Wala hata sikumuambia aje mbele, basi tu baada ya kuona nafurahia akaamua kuja mbele kunifurahisha zaidi.
Karusha rusha mwiko, Paaph Kwenye TV. Aliipiga kwa nguvu na tv kuweka crack na kuvujia wino. Haikuonyesha tena.
Ile hasira niliyokuwa nayo, acha kabisa. Dogo kanichomea 2.7m yangu wakati hata sijaenjoy bado? Hasira zilinitanda sana. Nikabaki naduwaa tu.
Pasipo kujua akaniletea remote, 'babaa imezima, niwashie'. Nikatamani nimuwashe yeye kibao cha nguvu, ila mkono unashindwa kunyanyuka kumfikia.
Kwa ile hasira, akatokea mama yake. Nikamuwakia yeye kuwa kamfundisha mwanae upuuzi kaja kuvunja TV bure. Hahahaha!.
Anamuambia mama yake, mbona haioneshi? In fact, sauti bado ilikuwa inasikika kutoka kwenye Theater.
Basi bhana, nikapotezea. Sasa ningelifanyaje? Ndiyo ile, umia utakavyotaka. Huna cha kunifanya 😂😂😂.
Ni bora watoto wafanye uharibifu ukiwa mbali. Vinginevyo unaweza kufanya jambo ambalo hukulitegemea. Hasira zitakuongoza kufanya jambo ambalo utalijutia baadae.
Je, ni changamoto gani iliyowahi kukukumba wewe kama mzazi?