Changamoto ya Malezi: Watoto kuharibu vitu

Changamoto ya Malezi: Watoto kuharibu vitu

my son ako na mwaka mmoja....siku nimelala aliiponda ponda samsung[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mama ake yuko bize nje anapika akajua na yy kalala(tulilala wote) akaamka kufanya maasi.....
JamiiForums203134350.jpg

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Yupo shule. Anarudi saa 6. Kwa hiyo bado ana muda mwingi sana wa kuwa nyumbani.

Mdada nishamuelekeza aangalie Tv mtoto wakati hayupo. Asubiri mpaka mama yake mtoto arudi then wataendelea kuangalia.
Kwahiyo unamuacha huyo dada wa kazi aendelee kuangalia na mtoto kwa sababu eti vikapanda vikashuka!

Kama umeweza kununua tv ya 2. Ngapi sijui huko..sidhani kama utashindwa kuweka mfumo wa kamera ndani kupitia simu yako ukawa unamfuatilia dada anafanya nini kwenye tv na baadhi ya maelezo mengine ya mtoto
 
Mnawalea watoto kizungu sana na ndio maana mnalipia kwa uharibiwa mali.

Mtoto anatakiwa kufunzwa kuwa na mipaka na vitu na ndio maana watoto hununuliwa matoi ya kuchezea ili wasishike vitu vya bei.

Kwann usimfunze mtoto kuwa eneo la tv ni off limits kwake?!

Kwann usimfunze kuwa ni marufuku kushika simu ya baba au mama au mtu yoyote, akishika unamkata jicho aina ya "nilikwambia nini ww'' kama utaona analeta upuuzi.

Huo uzungu mnaoleta mnawafunza watoto viburi na kuwa na tabia ya kulazimisha vitu bila mipaka.

Nakumbuka kuna kisa hapa juzi kati cha dereva wa gari ya kiongozi kama sikosei ni waziri, mtoto wake alikuta baba yake anaosha gari. Mtoto akaingia ndani ya gari na alipokuta ufunguo akatekenya likawaka akaweka sijui D kama sio R kisha akakanyagac wese , ngoma V8 ilifyatuka kama mshale ikaenda bamiza sijui wapi mtoto akafa hapo hapo na gari ikawa totalled haifai.

Baba akazimia chali na pressure juu nusu afe kwa mshituko. Waandishi wa habari wanamuhoji anashindwa kuongea huku kapoteza mtoto huku kibarua chake anawazia itakuwaje. Ilionyeshwa sana kwenye mitandao na hata vyombo vya habari hilo tukio.

Kisa kingine ni yule binti kwenye graduation alipochukua ufunguo kwa kaka yake akitaka kuchukua kitu kwenye gari then alipofika akaanza utundu usio na kichwa wala miguu, akawasha gari akatia reverse gear kisha akakanyaga wese hadi mwisho,matokeo yake aliwavaa wenzake kadhaa na kuwajeruhi vibaya na baadhi kuwa sababishia vilema vya maisha , akiwemo binti maarufu "Wakonta mapunda''' ambae hadi leo amepooza kutoka shingoni hadi miguuni.

Haya ni baadhi tu ya matukio ambayo ni matokeo ya ''poor parenting skills' kulea mtoto bila kumdiscipline kuwa na mipaka na utundu wake'.

Sometimes kama mzazi unatakiwa kuwa mbogo kwa mtoto ili ajue kuwa anavuka mipaka. Ninyi wazazi wa siku hizi mna malezi ya kipumbavu sana. Mtoto analeta ujinga mbele yako wewe unakenua meno badala ya kumkemea, ukiulizwa why unalea hivyo utasikia aaah wacha mtoto afurahi akiwa na wazazi afanye atakavyo.

Its okay mtoto kuhave fun but kama mzazi unatakiwa kuwa una calculate associated risks zinazomzunguka mtoto katika michezo yake before hajaleta madhara au hasara ili uweze muwekea mipaka ya michezo yake. Mtoto anarusha rusha vitu sebuleni piga biti la maana aache. Mtoto anaruka ruka kwenye makochi sijui kujibinua sarakasi unamkemea kijeshi. Mtoto analilia simu yako au mkeo/mumeo, piga biti la maana akiiona hiyo simu aione kama bomu aikwepe.

Mtoto anachezea remote za tv na king'amuzi kemea hiyo tabia azishike pale anapobadili channel sio kugeuza remote ni toy.

Mtoto anashika funguo ya gari bila maelekezo yako mzazi mkemee ajue ni mwiko kichezea vitu vya baba bila ruhusa.

Ukicheka na mtoto leo anaporukaruka hapo sebuleni na kuna meza vioo, tv na vitu vingine, kesho hatokusikiliza ukienda nae ugenini na atavunja vitu vya watu vya bei ushindwe lipa.

Wazazi acheni malezi yasiyo na kichwa wala miguu. Mtoto wa miaka 1,2,3,4,5,6, hadi kumi anashikaje simu yako na kuipekua pekua..... Hebu tuwe responsible......
 
Uzi una kila dalili ya madeko kupitiliza. Vijunia grade 1.
 
Mnawalea watoto kizungu sana na ndio maana mnalipia kwa uharibiwa mali.

Mtoto anatakiwa kufunzwa kuwa na mipaka na vitu na ndio maana watoto hununuliwa matoi ya kuchezea ili wasishike vitu vya bei.

Kwann usimfunze mtoto kuwa eneo la tv ni off limits kwake?!
Huu ni ushauri bora zaid kuliko shauri zote hapa....
Mwamba nimekuaminia
 
Mnawalea watoto kizungu sana na ndio maana mnalipia kwa uharibiwa mali.

Mtoto anatakiwa kufunzwa kuwa na mipaka na vitu na ndio maana watoto hununuliwa matoi ya kuchezea ili wasishike vitu vya bei.
Kabisa mkuu
 
Watoto wa siku hizi hawafunzwi value ya vitu. Hawajui thamani ya chochote. Enzi zetu mtoto ana miaka mitatu ameshajua kitu flani cha mama na kitu flani cha baba sio cha kushikashika, au kitu flani ni cha thamani kubwa kwa wazazi. Kuna jirani hapa ,eti mtoto alikasirika akatupia kikombe kwenye Tv. Wazazi wengi wanafeli.
 
Mkuu Samcezar umemaliza kila kitu, mtoto lazima afunzwe kujua mipaka yake toka akiwa mdogo sana, nina wa kwangu wa miaka 3 sasa, kitu pekee ambacho nakumbuka amewahi kuvunja ni kikombe cha udongo.

Nilijitahidi kumfunza toka akiwa anatambaa kutogusa au kusogelea vitu fulani(mfano maeneo karibu na TV na vyote vinavyohusiana nyaya, deki n.k na anaheshimu hadi kesho, tena sasa anajifunza kwa utaratibu maalumu kama kuwasha, kupunguza sauti, kubadilisha channel na inalipa kwa kweli maana hata vitu ambavyo ni delicate ukimwambia achukue,atakibeba kwa uangalifu sana....

Wazazi tusizidishe urafiki wa kwa watoto,tukumbuke pia wao ni wanafunzi wetu.Vile tunavyotaka wawe wakiwa wakubwa,inatupasa tuanze kuvifundisha sasa.Tukumbuke mazoea hujenga tabia,na tabia ni ngumu kuiacha.
 
Kan
Wasalaam Wakuu!.

Watoto ni baraka kubwa sana na kila mzazi angelipenda kuwa na watoto ili kujenga familia yenye furaha na amani. Watoto ni faraja kubwa sana kwa wazazi lakini muda mwingine ni changamoto sana.

Je, umewahi kukutana na changamoto ya watoto kuharibu mali na vitu vya thamani katika kipindi cha ukuaji wao? Tena kwa sababu ya utoto wake, huna cha kufanya. Unabaki kugugumia tu kwa maumivu.

Mimi ilinitokea hivi,
Smart Tv yangu ya LG, nimenunua zangu kwa Benson Electronics (Arusha), Tsh 2,700,000. Nikatumia kwa miezi miwili tu 😭😭😭.

Nipo sebuleni naagalia TV, mwanangu wa miaka minne aliwekewa Movie ya Jet Lee (sina hakika). Sasa kashazoea kuangalia mara nyingi sana. Movie ile ilikuwa ni ya kutumia majambia.

Mimi nipo zangu busy kumuangalia anavyocheza na mwiko mkononi, 'baba anafanya hivi'.

Najisemea moyoni, nimepata kidume. Atakuja kuwatandika watu mpaka washangae. Pasipo ya kujua nahatarisha amani ya moyo wangu kwa dakika chache zijazo.

Dogo anacheza mbele yangu, ili nimuone vizuri. Wala hata sikumuambia aje mbele, basi tu baada ya kuona nafurahia akaamua kuja mbele kunifurahisha zaidi.

Karusha rusha mwiko, Paaph Kwenye TV. Aliipiga kwa nguvu na tv kuweka crack na kuvujia wino. Haikuonyesha tena.

Ile hasira niliyokuwa nayo, acha kabisa. Dogo kanichomea 2.7m yangu wakati hata sijaenjoy bado? Hasira zilinitanda sana. Nikabaki naduwaa tu.

Pasipo kujua akaniletea remote, 'babaa imezima, niwashie'. Nikatamani nimuwashe yeye kibao cha nguvu, ila mkono unashindwa kunyanyuka kumfikia.

Kwa ile hasira, akatokea mama yake. Nikamuwakia yeye kuwa kamfundisha mwanae upuuzi kaja kuvunja TV bure. Hahahaha!.

Anamuambia mama yake, mbona haioneshi? In fact, sauti bado ilikuwa inasikika kutoka kwenye Theater.

Basi bhana, nikapotezea. Sasa ningelifanyaje? Ndiyo ile, umia utakavyotaka. Huna cha kunifanya 😂😂😂.

Ni bora watoto wafanye uharibifu ukiwa mbali. Vinginevyo unaweza kufanya jambo ambalo hukulitegemea. Hasira zitakuongoza kufanya jambo ambalo utalijutia baadae.

Je, ni changamoto gani iliyowahi kukukumba wewe kama mzazi?
Ndio maana hata TV ya 90elfu sina, yaani pesa yakumiliki heka kumi huko chaugingi inakaa sebuleni 😡?
 
Kwenye hiyo changamoto uliyoitaja kuhusu mtoto, nimejaribu kufikiria tu kama ingetokea kinyume chake na ikaleta madhara kwa mtoto iwe ulemavu au kumpoteza kabisa halafu hicho kifaa au kitu cha thamani kilichokupa hasira kikabakia kizima, ungejisikiaje? Nafikiri wazazi na walezi tunatakiwa kujifunza ku-control hasira na kutovipa thamani kubwa na umuhimu vitu ambavyo vikiharibika tunaweza kuvi-replace kuliko watoto wetu.

Tujiepushe ku-attach thamani ya vitu kwa watoto wetu.
 
Back
Top Bottom