geraldincredible
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 2,035
- 7,223
Kwahiyo unamuacha huyo dada wa kazi aendelee kuangalia na mtoto kwa sababu eti vikapanda vikashuka!Yupo shule. Anarudi saa 6. Kwa hiyo bado ana muda mwingi sana wa kuwa nyumbani.
Mdada nishamuelekeza aangalie Tv mtoto wakati hayupo. Asubiri mpaka mama yake mtoto arudi then wataendelea kuangalia.
Huu ni ushauri bora zaid kuliko shauri zote hapa....Mnawalea watoto kizungu sana na ndio maana mnalipia kwa uharibiwa mali.
Mtoto anatakiwa kufunzwa kuwa na mipaka na vitu na ndio maana watoto hununuliwa matoi ya kuchezea ili wasishike vitu vya bei.
Kwann usimfunze mtoto kuwa eneo la tv ni off limits kwake?!
Kabisa mkuuMnawalea watoto kizungu sana na ndio maana mnalipia kwa uharibiwa mali.
Mtoto anatakiwa kufunzwa kuwa na mipaka na vitu na ndio maana watoto hununuliwa matoi ya kuchezea ili wasishike vitu vya bei.
Ndio maana hata TV ya 90elfu sina, yaani pesa yakumiliki heka kumi huko chaugingi inakaa sebuleni π‘?Wasalaam Wakuu!.
Watoto ni baraka kubwa sana na kila mzazi angelipenda kuwa na watoto ili kujenga familia yenye furaha na amani. Watoto ni faraja kubwa sana kwa wazazi lakini muda mwingine ni changamoto sana.
Je, umewahi kukutana na changamoto ya watoto kuharibu mali na vitu vya thamani katika kipindi cha ukuaji wao? Tena kwa sababu ya utoto wake, huna cha kufanya. Unabaki kugugumia tu kwa maumivu.
Mimi ilinitokea hivi,
Smart Tv yangu ya LG, nimenunua zangu kwa Benson Electronics (Arusha), Tsh 2,700,000. Nikatumia kwa miezi miwili tu πππ.
Nipo sebuleni naagalia TV, mwanangu wa miaka minne aliwekewa Movie ya Jet Lee (sina hakika). Sasa kashazoea kuangalia mara nyingi sana. Movie ile ilikuwa ni ya kutumia majambia.
Mimi nipo zangu busy kumuangalia anavyocheza na mwiko mkononi, 'baba anafanya hivi'.
Najisemea moyoni, nimepata kidume. Atakuja kuwatandika watu mpaka washangae. Pasipo ya kujua nahatarisha amani ya moyo wangu kwa dakika chache zijazo.
Dogo anacheza mbele yangu, ili nimuone vizuri. Wala hata sikumuambia aje mbele, basi tu baada ya kuona nafurahia akaamua kuja mbele kunifurahisha zaidi.
Karusha rusha mwiko, Paaph Kwenye TV. Aliipiga kwa nguvu na tv kuweka crack na kuvujia wino. Haikuonyesha tena.
Ile hasira niliyokuwa nayo, acha kabisa. Dogo kanichomea 2.7m yangu wakati hata sijaenjoy bado? Hasira zilinitanda sana. Nikabaki naduwaa tu.
Pasipo kujua akaniletea remote, 'babaa imezima, niwashie'. Nikatamani nimuwashe yeye kibao cha nguvu, ila mkono unashindwa kunyanyuka kumfikia.
Kwa ile hasira, akatokea mama yake. Nikamuwakia yeye kuwa kamfundisha mwanae upuuzi kaja kuvunja TV bure. Hahahaha!.
Anamuambia mama yake, mbona haioneshi? In fact, sauti bado ilikuwa inasikika kutoka kwenye Theater.
Basi bhana, nikapotezea. Sasa ningelifanyaje? Ndiyo ile, umia utakavyotaka. Huna cha kunifanya πππ.
Ni bora watoto wafanye uharibifu ukiwa mbali. Vinginevyo unaweza kufanya jambo ambalo hukulitegemea. Hasira zitakuongoza kufanya jambo ambalo utalijutia baadae.
Je, ni changamoto gani iliyowahi kukukumba wewe kama mzazi?
Kwenye hiyo changamoto uliyoitaja kuhusu mtoto, nimejaribu kufikiria tu kama ingetokea kinyume chake na ikaleta madhara kwa mtoto iwe ulemavu au kumpoteza kabisa halafu hicho kifaa au kitu cha thamani kilichokupa hasira kikabakia kizima, ungejisikiaje? Nafikiri wazazi na walezi tunatakiwa kujifunza ku-control hasira na kutovipa thamani kubwa na umuhimu vitu ambavyo vikiharibika tunaweza kuvi-replace kuliko watoto wetu.Wasalaam Wakuu!.