KERO Changamoto ya mfumo wa ESS kwa watumishi wa Umma, nani awajibishwe?

KERO Changamoto ya mfumo wa ESS kwa watumishi wa Umma, nani awajibishwe?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mfumo wa ESS kwa watumishi wa Umma umekua na changamoto za mara kwa mara ..mara nyingi unakua down,je wanao simamia au walioleta huu mfumo hawakujua unyeti wa hili wanalo anzisha ?

Hawakujua kuwa mfumo unapaswa kuwa bora sana kuliko ulivyo sasa ..

Kumbuka huu mfumo ndio unaonesha uwajibikaji wa watumishi wa Umma [Performance 】 lakini huu unasumbua mara nyingi sana ,hata maelezo wanayotoa utumishi muda mw8ngine unaona kabisa sio ya msingi ,

Kushuka mara kwa mara kwa mfumo kunasababisha watumishi wa Umma kushindwa kupandisha kazi kwa wakati lakini mfumo au wanaosimamia mfumo unataka watumishi wafikie vigezo vilivyowekwa wakati mfumo wenyewe unachangamoto..

Nina mashaka na wasiwasi kuhusu manunuzi ya huu mfumo je ulikuja kwa vigezo vya kuondoa changamoto kwa watumishi wa umma au kuongeza changamoto..

Mfumo unapima kwa njia mbili mwaka wa fedha na kalenda ya mwaka January to Disemba ..lakini kuna malalamiko kwa wanaotumia kalenda kuanzia January mpaka Leo kwenye menu ya utendaji bado mfumo hajaruhusu kuweka mipango ya mwaka husika .

Tuombe TAKUKURU INUSE na kuchunguza unanunuzi wa mfumo huu ,je mfumo una vigezo vya kweli au fedha zetu za Umma hazina huruma kwa walipa Kodi.

Binafsi nikiona watumishi wanavyopata tabu mfumo kuwa down mara kwa mara ,najiuliza kwanini Utumishi wasiwajibike kwenye hili hatuwezi kuwa na mfumo kila wiki unapotea au unashindwa kufanya kazi unaanza kuwa unavizia upo au haupo ..

JF tusaidieni kupaza sauti ili kukuza uwajibikaji..
 
Back
Top Bottom