Changamoto ya mtoto kulia sana usiku

ndugu nimehangaika sehemu tofauti tofauti bila mafanikio natamani sana haya mazonge yaishe usiku usiwe kama adhabu kwetu
Mkuu hizi ni changamoto za kawaida sana kwetu sisi wazazi.
Na usijaribu kuingia kwenye imani hizo za ajabu, kwani amini hapo ndipo anguko lako litakapo tokea
 
mkuu mtoto anazidi kudhoofika bila sababu za msingi inauma mkuu
Kama wewe ni mtumishi nina uhakima haujapata mtu sahihi wa kukulelea mtoto wakati unapo kua kazini ndio maana anadumaa na anakua nyuma kukua ukilinganisha na umri wake sababu ya kukosa lishe.
Mkuu....
Kuna mwaka tuliwahi kukubaliana mimi na mke wangu nikaamua kuacha kazi ili nibaki nyumbani nilee mtoto.
 
Minaona mkuu, utakua unashida kwenye mtu anae mlea mwanao wakati wewe umeenda kazi.
Huyo mtoto nikama amedumaa na afya yake imedhoofika kutikana na lishe tu.
Ebu fanyia kazi hili maana unaweza ukawazunguka wataalamu wa watoto kwanza wakakusikiliza kisha wakaona kabisa tatizo lilipo ila wewe hautaki kuliona ukiamini hilo sio tatizo.
 
Pole sanavkwa changamoto unazopitia.
Hayo maswali yanaweza kuksaidia kutafta chanzo kiutalamu
1 .KWanza mtoto wa mwaka 1 anatakiwa awe na kilo angalau 10 na kuendelea.wako ana ngp?
2 . Mwaka 1 na miezi. 4 na hajaanza kutambaa hapo tunasema kachelewa kwenye stage ya ukuuaji tena sana(delayed millestone). Sahvi anawez kufany nn upand wa ukuuaji? Ashawahi kuugua utapiamulo?

(Kama bado ypo legelege kwenye mikono au miguu au upande mmja wa mwili ni dhaifu ndo hio ishu ya utindio wa ubongo/celebral palsy inaibuka)

3 . Hio kukohoa na kutapika. Nawez kusem inawezekan kua n hali ya utumbo haujakaa sawa kumeng'enya chakula vzri ila kuna watoto uzaliw na changamoto z utumbo kujikunja. Choo anapata? Ulimnyonyesha miez 6 ya mwanzo bila kumpa chochte?

4 . Kwako mama, Kipindi cha ujauzito wake uliwahi kuugua? Ulimzaa ana kilo ngapi? Ulijifungulia hospitali au nyumbani? Chanjo amepata ipasavyo?
5 . Ulijifungua kwa njia y kawaida au operation? Mtoto alichelea kulia baada y kutoka tumboni? Kwenye kitovu hajawahi shida kam kupata usaha. Ashawahi kua na manjano?
ILA kama hayo yote yapo vzri mtaalamu ausike ktafta chanzo maana sio kawaida.
 
ana kilo 8
kila anapo taka kutamabaa anaumwa sana hali inayo mfanya kurudi nyuma
kipindi cha mimba hakuwai kuugua
na alijifungua kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…