Changamoto ya umeme nchini ilianza na Awamu ya Tatu, sasa ni mbaya zaidi. Kwanini maji ya Ziwa Victoria yasipelekwe hadi Mtera na JNHPP kupata suluhu?

Changamoto ya umeme nchini ilianza na Awamu ya Tatu, sasa ni mbaya zaidi. Kwanini maji ya Ziwa Victoria yasipelekwe hadi Mtera na JNHPP kupata suluhu?

Wewe ndiye unaonesha hujasoma shule na kama ulisoma basi ulisoma ujinga. Hiyo geographia huijui. Kwa kukuelimisha kidogo ni kuwa kwa kawaida mito yote hupeleka maji aidha kwenye maziwa au baharini. Ziwa Victoria, ambalo ndiyo ziwa la maji baridi kubwa la tatu duniani, hupokea maji yake kutoka mito zaidi ya mia moja ya nchi za Tanzania, Kenya na Uganda. Tanzania ndiyo inayoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mito inayopeleka maji hayo ziwa victoria ikiwemo Mto Mara, Mto Simiyu, Mto Mirongo, Mto Manonga na Mto Kagera - kwa kutaja michache.

Mto Nile ndiyo mto pekee duniani ambao badala ya kupeleka maji ziwani au baharini kama ilivyo mito mingine, mto huu hutoa maji Ziwa Victoria na kuyapeleka kwenye bahari la Mediterranean ukianzia kwenye Mto Kagera na kupitia Uganda, Sudan, Ethiopia na Egypt. Bila kuwepo kwa mto Nile kuyapeleka maji haya ya Ziwa Victoria barahirini, ziwa hili lingalifurika na kuifanya Tanzania yote kuwa bahari. Hii ndiyo design ya Muumba wetu wa dunia na anga. Mto huu pia unajulikana kama the Blue River. Ndiyo mto mrefu kuliko mito mingine yote duniani.

Ethiopia na Egypt wanategemea sana mto huu wa Nile kwa uhai wao kwani nchi hizo ni za ukame throughout. Hawa chanzo kingine cha maji. Wakichimba visima wanapata mafuta badala ya maji. Kwa kutumia mto Nile unaotoka kwetu wanazalisha umeme mwingi ambao wataanza kutuuzia sisi. Pia mafuta yao wanatuuzia kupitia OPEC.

NB: Jaribu basi angalao google: 'The Grand Ethiopean Renaissance Dam'. Utaona ujinga wako uliousoma shuleni uliokurukupa kuuleta hapa.
Unaendelea kuonyesha ujinga wako. Bora ungegoogle kwanza kabla ya Kuja na huo ujinga humu.

Kwa kukusadia tu Google White Nile na blue Nile. Ukijua tofauti rudi uapologize...!!
 
Kuendelezwa kwake maana yake waondoe tope lote kwa kufunga maji yasitiririke kwa muda fulani.

Waweke turbines mpya, generators mpya.
Hiyo ni gharama kuliko kununua generators za gas

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Toa basi takwimu ya generator la gesi la MW 180 na lile la maji la MW 180 bei zake ni kiasi gani? Kifizikia tu generator linalosukumwa na maporomoko ya maji technologically is much simpler and cheaper than ya lile linaloendeshwa kwa nguvu ya combustion ya gesi. Hata running cost and maintenance yake ni much cheaper.
 
Unaendelea kuonyesha ujinga wako. Bora ungegoogle kwanza kabla ya Kuja na huo ujinga humu.

Kwa kukusadia tu Google White Nile na blue Nile. Ukijua tofauti rudi uapologize...!!
Wewe kweli ni Khoisan. Mimi huwa sibishani na watu kama wewe. Mie siyo caliber yako. Kama hutaki nikuelimishe basi kaa kimya. Nimekuambia utembelee the Grand Ethiopian Renaissance Dam, umeshindwa. Bado unaendelea kuwatetea hao waliokutuma wa tanesco plus their allies. Ushindwe na ulegee!
 
Duh, sijaelewa
Pole Mbazi, soma taratibu utaelewa tu. Nimependekeza solution ya kudumu ya kumaliza changamoto la upatikanaji wa uhakika wa kudumu na wa bei nafuu wa nishati ya umeme Tanzania. Nimependekeza bomba kuu la maji kutoka Ziwa Victoria ambalo sasa lilishafika mkoa wa Tabora, lipelekwe hadi bwawa la Nyerere na lile la Mtera au Kihansi. Bomba hilo litakuwa akiba kutumika (kufunguliwa) kuyajaza maji pindi mabwawa hayo makubwa kwa uzalishaji wa umeme yanapopata changamoto ya upungufu wa maji hasa kipindi cha kiangazi. Nadhani utakuwa umeelewa sasa.
 
Akili hizi we ukipewa nchi, lazima tuingie kwenye vita na wamisri
Mbona tayari tulishaelewana nao. Tulivutana tulipoanza kuyapeleka maji haya huko Shinyanga na Kahama. Hiyo ilikuwa enzi ya awamu ya tatu ya Mzee Mkapa. Tukaelewana. Lengo ilikuwa kuyapeleka hadi Dodoma. Mzee Lowasa alipendekeza yaende hadi Dar. Awamu ya tano ikayapeleka hadi Tabora. Tunaiomba awamu ya sita iyasogeze hadi kule Mtera na JNHPP. Litakuwa ni jambo la maana sana kuivusha nchi yetu hadi upper middle income country. Hadi sasa wa Misri ni marafiki wetu sana. Na ndiyo maana wanatujengea hilo bwawa la JNHPP na wangalipenda liwe na chanzo cha maji cha uhakika na cha kudumu kama Ziwa Victoria. Hayo maporomoko ya Stiglers gauge ni makubwa kuliko yote yaliyopo barani Afrika. Yanaweza kuzalisha umeme wa zaidi ya MW 10,000. Kwa awamu ya kwanza tutaanza na MW 2,200 kwa kufunga turbines 9. A
 
Wewe kweli ni Khoisan. Mimi huwa sibishani na watu kama wewe. Mie siyo caliber yako. Kama hutaki nikuelimishe basi kaa kimya. Nimekuambia utembelee the Grand Ethiopian Renaissance Dam, umeshindwa. Bado unaendelea kuwatetea hao waliokutuma wa tanesco plus their allies. Ushindwe na ulegee!
Mbuzi wewe. Unasoma magazeti I unakuja humu kujifanya mjuaji. Huko unakokuzungumxia tumefikia. Kwa jinsi ulivyoandika inaonekana kabisa hujawahi kutoka Tanzania..

Kuna white Nile ambayo inaanza lake Victoria na blue Nile ambayo inaanza Ethiopia. Hizo Nile 2 zinakutana Khartoum, Sudan. Nile haitoi Victoria kwenda Ethiopia.

Halafu hiyo suggestion yako ya kutoa maji Victoria kwa mabomba kuyapeleka Mtera na Bwawa la Nyerere ni la kijinga. Linaonyesha ulivyo na upeo mdogo wa kufikiria.
 
Hizi story za bwawa hupotoshwa na wale ambao walikuwa hawataki ni Kama story za gesi pia wale walikua hawataki walipotosha.

Mradi ni 2% tu ya eneo lote. Sasa hao viumbe wanakosaje kutumia hayo maji?
Mimi sizungumzi % ya eneo la bwawa, lakini hayo maji ndiyo muhimu. Unaufahamu ukubwa wa Rufiji basin na catchment yake? Imeanzia kwenye Usangu plains. Hapa sasa hatuzungumzii wanyama tu kwenye mbuga lakini binadamu pia na matumizi mengine kama ya kilimo, viwanda na kadhalika.

Hakuna upotoshaji hapo labda kama umeweka siasa mbele. Bwawa lingejengwa lakini proper studies zingefanyika na mipango ikawekwa vizuri ili ipatikane win-win situation.
 
Kuendelezwa kwake maana yake waondoe tope lote kwa kufunga maji yasitiririke kwa muda fulani.

Waweke turbines mpya, generators mpya.
Hiyo ni gharama kuliko kununua generators za gas

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Unapropose yafungwe (decomissioned)?

Halafu mbona hao wajamaa wakisema mitambo ni mibovu watu wanapiga kelele?
 
Unajua kwamba kuna blue nile na white nile na vyanzo vyao ni tafauti?
Najua sana bintimkongwe. White nile aka mto tana ni moja ya tributaries za mto nile kama ulivyo mto kagera. Mto tana ukitokea ziwa tana nchini Ethiopia wakati mto kagera ukitokea nchini Tanzania. Isitoshe mito yote inayoingia ziwa victoria kama niliyoitaja hapo awali maji yake hupumulia mto nile unayoliunganisha ziwa lote la victoria na mabahari yote ya dunia kupitia Mediterranean sea. Sasa hizo mantiki za kubatilisha hoja yangu kwa sababu tu huo mto tana haupitii ziwa victoria, siioni kama ina mashiko yo yote. If any ni kwamba sisi Tanzania tumebarikiwa sana na Mwenyezi Mungu kwa utajiri wa maji baridi kuliko hao wa Ethiopia. Cha kushangazq Ethiopia inautumia utajiri wao mdogo wa white nile kuzalisha umeme mwingi hadi kuu export kwetu. Hawaogopi kelele za wana Misiri. Sisi kutengeneza bomba (artifial nile river aka suluhu nile river) kupeleka maji haya maeneo mbali mbali ya nchi yetu yenye uhitaji tunaogopa nini? Maji yetu haya yangaliweza kutuzalishia umeme mwingi kuliko ule unaozalishwa Ethiopia au Misiri. Yangaliweza kutuzalishia mpunga, ngano na mahindi zaidi ya yanayozalishwa huko Ukraine ambayo ulaya yote ndiyo wanayoyategemea. Sisi sijui tukoje. Inauma sana hasa pale nchi inakuwa gizani kama vile kuna vita. Inauma sana pale nchi inakuwa na mgawo wa maji na uhaba mkubwa wa chakula. Inauma sana pale nchi inakuwa na uhaba mkubwa wa chakula Bashe anaendelea ku export millions of tons ya chakula kwenda Kenya na Somalia. Au ni kwa sababu ana asili ya Somalia? Inauma sana pale nchi inakuwa na uhaba mkubwa wa nishati, Januari anjenga bomba la kupeleka nishati yetu ya gesi Mombasa wakati haijafika hata Mwanza. Au naye ana asili ya Mombasa. Samahani kwa kuropoka haya, ni kwa sababu ya uchungu wa kukosa umeme, chakula na maji.
 
Tanzania na African zina shida sana kuanzia Wananchi mpaka wanao pewa dhamana,Duniani kote hamna nishati rahisi kupatikana kama Umeme. Tuna kila chanzo cha umeme,tatizo ni kuwa hamna Rais mwenye uchungu na Nchi they all after money and prestige kuanzia kwa Mwinyi,Mkapa,Kikwete na Samia.

At least magufuli licha ya kuwa na approach mbovu katika ku-solve mambo but alikuwa na nia ya kutoka moyoni ya kutaka kufanya kitu kwa ajili ya Nchi.

Yani inaboa kwa kweli Leo kusipokiwa na umeme kesho maji hamna-halafu sababu ya kutopatikana umeme na maji ni zilezile toka tumepata Uhuru hadi Leo zaidi ya miaka 60.Afu at the same time unategemea uchumi wako ukue ajira ziwepo-ni upumbavu mtupu

Hii Nchi naona inahitaji Rais dikiteka zaidi ya Magufuli,maana hata historian inaonesha Marais madikiteta ndio sana uchungu na Nchi na huwa wanabadilisha mambo.

..tatizo letu ni kumtegemea Raisi kuwa na majibu ya kila changamoto ya nchi hii.

..yaani mtu akiwa Raisi wa Tz mara moja anageuka bingwa wa siasa, uchumi, sheria, ujenzi, nishati, elimu, etc etc.

..ukifuatilia historia yetu utaona Maraisi wetu wote walijifanya wajuaji ktk jambo fulani na matokeo yake vizazi na vizazi vya nchi hii vimeathirika.

..Kwa mfano, Nyerere alijifanya bingwa wa uchumi akataifisha mashamba na viwanda vya katani matokeo yake zao hilo likaanguka na halijatengemaa mpaka leo.

..Sitawajadili Mwinyi, Mkapa, na Kikwete, ili kuokoa muda. Twende kwa Magufuli.

..Tatizo la Magufuli kuhusu changamoto ya umeme ni kuwekeza ktk mradi mmoja tu mkubwa wa Stieglers gorge.

..Mradi mkubwa kama ule unachukua muda mrefu sana kakamilika. Pia unatumia fedha nyingi ktk ujenzi. Tulitakiwa tuwe na mradi wa ukubwa wa kati ambao ungekamilika ndani ya muda mfupi.

..Tatizo lingine la Magufuli ni kutumia fedha ktk miradi isiyo na tija kwa nchi. Kwa mfano, ujenzi wa mji mkuu Dodoma.

..Kupanga ni kuchagua. Tuliamua kujenga ikulu, maofisa, na majumba ya vigogo wa serikali Dodoma, badala ya kuelekeza fedha hizo kukarabati miundombinu ya kusambaza umeme, na maji.

..Wakati Magufuli akilazimisha maamuzi yake kulikuwepo na mawazo mbadala toka kwa wabunge ambayo kama yangesikilizwa tusingekuwa ktk mkwamo tulionao sasa hivi.

..Badala ya kuombea tupate Raisi Dikteta zaidi ya Magufuli tungeomba tupate Bunge imara linalotoa changamoto kwa serikali.
 
tupate Bunge imara linalotoa changamoto kwa serikali.
Unamaanisha bunge la kuipa changamoto serikali ama bunge la kuondoa changamoto za wananchi? Kwani huoni wabunge kama akina Mpina na Bashiru wanavyoipa changamoto serikali? Lakini mwisho wao si unajulikana?
 
Unamaanisha bunge la kuipa changamoto serikali ama bunge la kuondoa changamoto za wananchi? Kwani huoni wabunge kama akina Mpina na Bashiru wanavyoipa changamoto serikali? Lakini mwisho wao si unajulikana?

..vyovyote utakavyoitafsiri lakini tunahitaji BUNGE linalotekeleza wajibu wake sawasawa.
 
Tutashikana uchawi bure,,endeleni kukata miti ovyo. akili ikikaa sawa ndipo tutajielewa kuwa miti ni muhimu.Tatizo la vyanzo vya maji ndio chanzo cha kukosa umeme.umeme tusubiri mvua mbona tatizo halitaisha hilo.zaman haya mambo hayakuwepo wazee wetu walitunza misitu.walijua faida ya misitu ya asili.Siku hizi katakata ovyo misitu.kisha tutegemee Umeme usio katika haiwezekani..Tubadilike watanzania.Kauli mbiu kwa sasa iwe panda mti itutunze
 
Tutashikana uchawi bure,,endeleni kukata miti ovyo. akili ikikaa sawa ndipo tutajielewa kuwa miti ni muhimu.Tatizo la vyanzo vya maji ndio chanzo cha kukosa umeme.umeme tusubiri mvua mbona tatizo halitaisha hilo.zaman haya mambo hayakuwepo wazee wetu walitunza misitu.walijua faida ya misitu ya asili.Siku hizi katakata ovyo misitu.kisha tutegemee Umeme usio katika haiwezekani..Tubadilike watanzania.Kauli mbiu kwa sasa iwe panda mti itutunze
Waswahili wanasema it is a vicious cycle. Uwezekano wa kuingia kwenye hiyo cycle ni kuanza na kupunguza bei ya unit moja ya umeme kuwa shilingi zisizozidi 50 per unit. Wananchi wengi watapikia umeme badala ya kuni au mkaa. Wataacha kukata miti labda iwe ķwa ajili ya mbao za kujengea ambazo ni rahisi kuzithibiti. Miti itaongezeka hasa ile ya asili. Hivyo mvua zitaongezeka na maji yatajaa zaidi kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme. Umeme utazalishwa kwa wingi zaidi na bei yake itapungua zaidi na wananchi wengi zaidi watatumia umeme na kucha kukata miti ............ the cycle will go on and on.
 
Back
Top Bottom