DOKEZO Changamoto ya wizi Hospitali ya Rufaa Simiyu (Simiyu RRH) ipo muda mrefu, ishughulikiwe vizuri

DOKEZO Changamoto ya wizi Hospitali ya Rufaa Simiyu (Simiyu RRH) ipo muda mrefu, ishughulikiwe vizuri

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mfanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu (Simiyu RRH), niliajiriwa miaka kadhaa iliyopita. Kwa muda ambao nimefanya kazi katika hospitali hii, nimekuwa nikishuhudia changamoto nyingi, ikiwemo tuhuma za wizi na upotevu wa mali na fedha za hospitali.

Pia soma ~ RC Mtanda awapa saa 24 polisi kuwakamata walioiba betri 40 za MRI na X Ray

Nilipoajiriwa kwa mara ya kwanza, nilikuta suala la wizi wa hadubini za maabara. Baada ya muda, kukaibuka suala la upotevu wa fedha za ujenzi wa majengo ya hospitali.

Pia, kulikuwa na tuhuma za baadhi ya watu kuiba vifaa vya ujenzi na kuvihamishia kwenye maeneo yao binafsi ya ujenzi. Wafanyakazi walifikia hatua ya kuandika barua kulalamikia hali hiyo, lakini hakuna mabadiliko ya kuridhisha yaliyoonekana.

Kinachoniumiza zaidi ni kwamba hii ni hospitali ya rufaa ya mkoa, lakini wafanyakazi tunakabiliwa na changamoto ya kutolipwa stahiki zetu, ikiwemo fedha za kazi za ziada (extra duty) na malipo ya bima.

Kwa upande wangu, tangu nilipoajiriwa mwaka 2022, nimekuwa nikipokea fedha za bima kwa viwango vinavyotofautiana, wakati mwingine Sh 400 na wakati mwingine Sh 700, huku nikishuhudia viongozi wa juu wakilipana fedha nyingi zaidi.

Suala la malipo ya kazi za ziada nalo ni changamoto kubwa. Ukithubutu hata kuandika au kuhoji kuhusu malipo hayo, unaonekana kama mpinzani wa uongozi. Hali hii inakatisha tamaa sana, hasa kwa wafanyakazi ambao tunajitahidi kutekeleza majukumu yetu.

Kwa kweli, hali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu inasikitisha sana. Ndiyo maana baadhi ya wafanyakazi wanapoajiriwa hapa hawakai kwa muda mrefu. Kila siku uongozi unabadilishwa, lakini changamoto zinaendelea kuwa zilezile bila kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Binafsi nimefikia hatua ya kuiita hospitali hii 'TAMISEMI iliyochangamka' kutokana na mambo yanayoendelea hapa. Inasikitisha sana kuona hospitali ya rufaa ya mkoa ikiendelea kukabiliwa na changamoto hizi kwa muda mrefu bila ufumbuzi wa kuridhisha.
 
kama wameshindwa kuiendesha hiyo hospital ifungwe,majengo yatumike na gereza la maswina
 
Poleni kwa kutolipwa extra duty inaumiza kama mpangiwe zamu za kawaida mkitoka mkafanye kazi zenu zingine zitakazowaingizia kipato
 
Hizo changamoto za hapo spitali ya Simiyu ni za kweli kabisa.

Mimi ni shuhuda ila baadhi ya wahusika wa wizi sitowataja hapa.
 
Back
Top Bottom