Hiyo njia
Ukiendesha gari muda mrefu ukaona macho yanataka kufunga lazimisha next ten km. Kisha uniambie utakuwa umeona vibwengo vingapi.
Unapochoka ubongo unatabia ya kutaka kushutdown (ni Kama radiator umepata Moto Sana gari huzima). Katika process hiyo macho hushurutishwa kufunga na hapa ndipo utaanza kuona vitu vya ajabu ajabu kwa sababu ushirikiano n aubongo umekuwa ndogo hivyo tafsiri za ilichokiona inaweza isitafsiriwe sawia, hivyo Calvert utaona Kama ni mbwa etc tukilazimisha kidogo ajali tunaanza kusema Kuna mtu alikatiza
Nocturnal wengi wanajua ukiendesha every 2.5 - 3hrs simama stretch kidogovuta sigara, kojoa hutakaa uone hivyo vibwengo Ila tutakutana na vitu vya kweli.
Mfano: maeneo ya hedaru mpaka Mwanga kukutana na punda ni jambo la kawaida sio miujiza ni wanyama kweli.
Njia ya mkuranga Lindi Kuna wabeba mkaa na magogo wa hatari jiandae, Morogoro kongwa jiandae na matrekta vicheche na waswaga Ngombe usiku Dodoma babati Arusha Ngombe, wanyama pori. Tabora Urambo Kaliua Uvinza mifugo na vinyama vya porini. Kila njia inachangamoto zake za kweli sio vibwengo.
Ingawa sipangani na ukweli kwamba hao washirikina hawapo la hasha Ila tahadhari ni muhimu Sana uweze kutofautisha story za vijiweni na reality