Frumence M Kyauke
JF-Expert Member
- Aug 30, 2021
- 630
- 1,262
Kituo cha mabasi cha Magufuli Mbezi kimekuwa na idadi kubwa ya watu wenye nia mbaya na abiria ikiwemo wezi na matapeli wanaosababisha usumbufu mkubwa sana kwa abiria wanatumia kituo hiki.
Kituo hiki kinaweza kuwa genge la wezi na matapeli wanaoleta usumbufu mkubwa kwa abiria kwa kuwaibia mali zao ikiwemo simu na mali zenye thamani.
Sisi wananchi tukiwa kama wahanga wakubwa tunaomba Serikali, na wasimamizi wa kituo hiki kufanya uchunguzi wa kina wa kubaini wezi hao wanaotumia kituo hiki kama sehemu ya kufanya uhalifu.