First Year nilipanga na mwamba mmoja (binamu yangu) yeye alikua second year, aisee alinyoosha siwezi sahau. [emoji23]
Kwanza, alikua anapenda juice za matunda. Kila siku alikua ananunua lita mbili za juice ya matunda, halafu alikua hamalizi yote, lazima abakize kwenye chupa.
Halafu hayo mabaki ya juice alikua anayatunza ndani ya nyumba hata kwa mwezi mzima mpaka yanavunda bila kuyatupa dampo. Alikua anapenda kufunga madirisha, hiyo harufu ya uvundo ndani ya ghetto aiseee ukikaa dakika moja tu lazima ukimbizwe ICU kwa matatizo ya upumuaji [emoji23].
Pili, alikua hajui kupika wala kuosha vyombo ila nikipika alikua wa kwanza kuja kula. Sema fresh tu nilivunga sababu alikua mwenyeji wangu wa jiji wakati huo.
Tatu, Alikua anafua nguo mara moja kwa semester, mara zote ilikua kipindi anachotaka kurudi nyumbani baada ya kumaliza UE. Nguo chafu alikua anatunza uvunguni mwa kitanda halafu anachagua zile zilizochafuka kidogo anarudia kuzivaa tena ( kitaalamu inaitwa system update). Harufu ya uvundo wa nguo ilifanya kusiwe na tofauti kati ya gari la taka na ghetto.
Nne, Alikua anapenda kuangalia movies mpaka sasa 8 usiku huku sauti ikiwa juu sana na wakati mwingine alikua akikesha na movies mpaka asubuhi. Hivyo alinipa wakati mgumu sana wakati wa kulala sababu ya makelele.
Tano, Alikua anapenda kushinda ndani hata wakati wa mchana akicheki movies hivyo alininyima chance ya kuleta totoz ghetto. Hivyo sikuweza kumpiga exile hata mara moja, inauma sana [emoji23]
Sita, alikua hapendi wageni waje ghetto sababu ya uchafu wa ghetto. Hivyo hata rafiki zangu sikuwahi kuwakaribisha nyumbani licha ya wao kutaka kunitembelea mara kwa mara. Alikua mchafu asiependa kudhalilika.
Sema mwamba alikua anapenda sana kusikiliza mahubiri ya Mwl.Mwakasege na kusoma Biblia hivyo alikua ananifundisha mambo mengi ya Kikristo.
Kingine hakua na mkono wa birika.
Nilikaa na mwamba semester moja tulivyorudi chuo kutoka likizo nikapanga ghetto langu nikapumua, nikaanza kula utawala na mimi.