Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

This is the reason behind kupandisha bandiko hili, limefuatiwa na makala ya kina kwenye Nipashe la Leo, na kipindi cha TV cha uelimishaji umma kuhusu secure investment kwa wastaafu watarajiwa kitafuata na naamini kitasaidia wengi.

P

Mkuu sijui umelifikiriaje, ila kuwa kwenye nchi isiyo na social security pamoja na Pension ya kueleweka hasa kwa watu waliofanya kazi kwenye private sector huoni kama kuzaa ni changamoto?
 
Mkuu sijui umelifikiriaje, ila kuwa kwenye nchi isiyo na social security pamoja na Pension ya kueleweka hasa kwa watu waliofanya kazi kwenye private sector huoni kama kuzaa ni changamoto?
Mkuu Rebeca 83, you are absolutely right, na mimi ni mfano hai, nimefanya public sector, for just 12 years, na sasa niko private sector for 20 years now. Ukisoma tuu heading ya bandiko hili, "

Changamoto za Kupata Mtoto Mchanga, Ukiwa Umri wa Kustaafu!. Unakuwa ni Baba Babu!. Dawa ni Kujipanga Kabla, Vinginevyo ni Kubebesha Watu Mizigo Yako!",​


The heading says it all, hivyo japo lengo na target ya bandiko hili ni wazee vijana, wanaolea mwana mjukuu, lakini hoja zake zitawasaidia wengine wengi, ambao bado wako kazini, kuanza kujipanga mapema kustaafu, ili hata wakistaafu wafanye secure investments na fedha za mafao Yao.

Kwenye kipindi cha TV kuhusu mada hii, pia nitakuwa na program II itakayo wahusu watu wa informal sector ambao hawana pensheni yoyote, hawana savings zozote, they live hand to mouth.
P
 
Makala kwa kiingereza , tunaiitaje ?
Niliomba safu The Daily News, The Guardian na The Citizen, niliahidiwa kupatiwa nafasi, ila bado sijapewa, labda niwakumbushie tena, ila pia kuandika makala lugha isiyokuwa lugha yako ya asili, ni changamoto, ingawa mimi ni a university graduate,na A-level nimefanya HGL, na nimeishi ughaibuni nazungumza fluent, ila kiukweli kuandika bado ni changamoto.
P
 
Kwenda kliniki mnapishana na wanao na wakwe zako umewaaibisha sana wanao ujui tu tena umesoma. Ungekuwa huna elimu sijui ungefanya utaira gani.
 
Ila kwa ujumla kuwa na vitoto uzeeeni ni dalili ya umasikini, yani unaacha kuwaza maisha yako ya uzeeni yanakuwa vipi unaanza kuhangaika na pampasi na wipes, kaka sema ilikua bahati mbaya tu nyie wazee wa lake zone usitake kuhalalisha, ndiomaana katika maisha kuna umri wa kuzaa, kulea na hata umri wa kupumzika. Usidanganye watu kwa andiko lako kwingine watu wangeuchuna wala isingekua public kaka Paskali.
 
Leo Ijumaa ya Tarehe 8 April, ni siku yangu ya kuzaliwa, nikiwa nimeipiga mingi nikikaribia 60! ambao ndio umri rasmi wa kustaafu, nikiwa tayari ni father of 8 +1= 9, Grand Pa of 6, and about to retire!.

Sababu ya makala hii ya leo sio kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, bali kutoa mbinu za changamoto za ulezi katika umri mkubwa kwa huku unajiandaa kustaafu, huku vichanga vinaendelea kuzaliwa!.

Naomba kutoa taarifa ya ujio wa mgeni mwingine kwenye familia yangu, ujio wa mgeni huyu, ume concide na tarehe yangu ya kuzaliwa, mgeni huyu mpya, amebisha hodi Duniani Leo, 8 April, 2022 majira ya saa 4:00 asubuhi, katika hospital ya Aga Khan, na kwa vile mgeni mwenyewe ni kidume, hivyo nimetoa jina langu la Pascal, hivyo ataitwa Pascal Mayalla, Jnr na kuanzia leo mimi nimebadili jina na kuwa Pascal Mayalla Snr baada ya ujio wa Pascal Mayalla Jnr.

Happy Born Day Pascal Mayalla Jnr
Happy Birthday Pascal Mayalla Snr
Paskali
Mimi Niko 50+ nilikuwa naogopa bure tuu, angalia mwenzagu huyu
1650554265357.png

 
Happy birthday Legendary.....

Ludi matizi hakikisha unakula vyakula vya asili,Miaka 60 kidini ndio miaka ya kuishi baada ya hapo ni zawadi tuu...
Mimi kwangu Aluta Kontinua na nikigonga 60 natafuta mwana mwali nimalizie nae dunia😁😁😁 Bina Shadeeya uwongo uwongo!
 
Happy birthday Legendary.....

Ludi matizi hakikisha unakula vyakula vya asili,Miaka 60 kidini ndio miaka ya kuishi baada ya hapo ni zawadi tuu...
Mimi kwangu Aluta Kontinua na nikigonga 60 natafuta mwana mwali nimalizie nae dunia😁😁😁 Bina Shadeeya uwongo uwongo!
Wacha weee!! 😀

Kweeli Binamu japo kwa mbaali si ajabu ukazisogeza siku zako za kuaga dunia karibu hasa pale ambapo utafanya uchaguzi usiyo sahihi.
 
Kumuona sura au akili huyo mtoto wa Pascal Mayala? Sura aweza kuwa vizuri shughuli kwenye akili .Toto la baba mzee na Mama mzee changamoto hata akizaliwa mzima iko kwenye akili mbele utaliona performance shule kuwa kuna walakini hata ulipeleke shule nzuri
Acha fikra potofu. Mama yangu alinizaa akiwa 45 na baba akiwa 6o, likini nikazaliwa mtoto bright hadi nikachaguliwa shule vipaji maalum. Na sasa hivi niko njema huko kazini.
 
Pascal Mayalla wewe ni humble sana ata kwenye kujibu maswali japo wengine kejeli nyingi kama vile wamekamilika, pia kikubwa umetoa elimu nzuri kwa wastaafu, ila kwa hizo Government bonds kwa 25 years( mfano wako ) na suala currency kutopeza value inakuwaje hapo?
 
Hongera sana naona we ni umri wa baba yangu kabisa,, nikupongeze na Wala usijutie kupata huyo mtoto, waafrika wengi tumekuwa wazungu eti na sisi hatutaki watoto, hasa wanawake ndo kabisaa tunaogopa hatari,, kanifurahisha sana CONTROLA
 
Back
Top Bottom