Changamoto za Malezi: Ukigundua umemkosea mtoto wako mdogo huwa unafanya nini? Unamnunulia anachokipenda (chips), unamuomba msamaha au unapotezea tu?

Changamoto za Malezi: Ukigundua umemkosea mtoto wako mdogo huwa unafanya nini? Unamnunulia anachokipenda (chips), unamuomba msamaha au unapotezea tu?

Just imagine umemchapa mtoto kwa kumhisi anang'ata buttons za remote controller ya TV kumbe sio yeye bali ni panya ndio wanaharibu...
Unamwambia ahakikishe anajua ni nani anakula rimoti na aihihfdhi sehemu ambayo panya ahwafikii,ikiwezekana analala nayo kabisa.Hayo ndio malezi.Unampa mtoto principles Justice atajifunza mwenyewe
 
Unamwambia ahakikishe anajua ni nani anakula rimoti na aihihfdhi sehemu ambayo panya ahwafikii,ikiwezekana analala nayo kabisa.Hayo ndio malezi.Unampa mtoto principles Justice atajifunza mwenyewe
Lakini tayari unajua kuwa umemchapa kimakosa?
 
sawa kabisa. Mzazi huwa hakosei. Kitendo cha mtoto kumfanya mzazi amchape kimakosa hilo lenyewe ni kosa kwa mtoto na anastahili nyongeza ya viboko.
Kwanini mzazi hasikosee?

huoni huo ni ukoloni kabisa?

Ndo maana kuna watu waoga sana wa kufanya vitu,kuuliza kwa sababu wanaogopa kumkosea mtu ambaye yupo kama yeye, hata shule hivyohivyo eti mwalimu hakosei.
 
  • Thanks
Reactions: THT
sawa kabisa. Mzazi huwa hakosei. Kitendo cha mtoto kumfanya mzazi amchape kimakosa hilo lenyewe ni kosa kwa mtoto na anastahili nyongeza ya viboko.
Khaaaaaaa nawaonea huruma wanao [emoji23][emoji23][emoji23]
 
  • Thanks
Reactions: THT
Kama mzazi kuna wakati mtoto anakosea namchapa af baadae nagundua kua ningeweza kumuonya kwa mdomo tu, so namkumbatia namwambia pole mwanangu mama hatarudia tena....then namuacha aendelee na michezo yake.Sio kila mara nampa treat kwasabu atazoea kua nikichapwa au nikikosewa natakiwa nipewe kitu. Vizawadi namnunulia tu randomly...
 
Ndio maana unatakiwa kuwa fair. Tafiti na uje na facts kabla ya kumhukumu mtoto kwa mambo ambayo haujaconfirm..... Sio tu mtoto hata mkeo pia usianze kumuwashia moto kwa jambo ambalo hakufanya.

Ukigundua umemkosea mtoto kwa hali na namna unayosema wewe then unatakiwa umwambie kwa upole kuwa ulijua ni yeye ana hatia kumbe si yeye then mwambie mtoto pole kwa kumuumiza hisia halafu mdistract kitu anapenda mfano mnunulie soda au pipi au kitu kitachosindikiza ile pole.

Ila usihangaike na kumwomba msamaha kwa mila zetu za kiafrika mtoto au mdogo haombwi msamaha ili siku nyingine akikosea asije akakubishia maana yeye anajifunza wewe unatekeleza.....
 
Mtoto akikosewa anaombwa msamaha kabisa,yeye ndipo anapojifunza kuwa akikosea naye aombe msamaha.maisha ya famiia ni uwazi na ukweli ndiyo hunogesha mahusiano,hata km ni mtoto wa kindergaten unamwomba tuu.mf ohh mwanangu nilikosea nilipokugombeza kumbe siyo wewe uliyemwaga maziwa,nisamehe mwanangu,then una mb
mzazi hakosei? Kwani kuna mzazi malaika? Hapo tunajifariji kwa ajili ya kuogopa kushuka,shuka ndugu hapo ndipo penye unyenyekevu
HAO WALE WATOTO WENU AKINA JUNIOR. Endelei kuwalea hivo. Mtakuja kutupa majibu.
 
Kwanini mzazi hasikosee?

huoni huo ni ukoloni kabisa?

Ndo maana kuna watu waoga sana wa kufanya vitu,kuuliza kwa sababu wanaogopa kumkosea mtu ambaye yupo kama yeye, hata shule hivyohivyo eti mwalimu hakosei.
Waombeni msamaha, then baada ya miaka michache mje mtupe mrejesho.
 
Mtoto akikosewa anaombwa msamaha kabisa,yeye ndipo anapojifunza kuwa akikosea naye aombe msamaha.maisha ya famiia ni uwazi na ukweli ndiyo hunogesha mahusiano,hata km ni mtoto wa kindergaten unamwomba tuu.mf ohh mwanangu nilikosea nilipokugombeza kumbe siyo wewe uliyemwaga maziwa,nisamehe mwanangu,then una mb
mzazi hakosei? Kwani kuna mzazi malaika? Hapo tunajifariji kwa ajili ya kuogopa kushuka,shuka ndugu hapo ndipo penye unyenyekevu
Naunga mkono wazo lako 100%
Wengi wanabeba tamaduni za wazazi wetu ooh "Mzazi wako ni mungu" uki endelea kuwa hivo hujengi uhusiano mzuri na mtoto, kuwa Transparent sio hypocrite katika malezi, Mtoto ukimkosea mwambie Niwie radhi mwanangu nlighafilika nkakuonea, akikosea ki ukweli muadibishe ki haki, wajua ukikua na kanuni ya "Tenda kwa wengine upendavyo kutendewa " uta ishi kwa amani sana.
 
Back
Top Bottom