Changamoto za Malezi ya Watoto kipindi wakiwa kwenye Balehe

Changamoto za Malezi ya Watoto kipindi wakiwa kwenye Balehe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Huu ni wakati ambao mabadiliko mengi katika mwenendo wa maisha ya mtoto hujitokeza ambayo hutokana na homoni ambazo husababisha mabadiliko ya kimwili, kiakili, kihisia, na mahusiano yake kijamii pia.

Katika umri huu, watoto hufanya uamuzi wenyewe kuhusu marafiki, michezo wanayoipenda. hisia za kujiamini na kujitegemea huongezeka maradufu, ingawa uangalizi wa wazazi ni muhimu. Miongoni mwa changamoto wanazopitia Watoto katika kipindi cha balehe ni kama zifuatazo.

Muonekano Huu ni wakati ambao watoto wanajali muonekano wao wa nje. Hii ni fursa kwako mzazi kumpa majibu ya kweli kuhusu maadili, haiba, mtazamo halisi wa jamii juu ya muonekano wake, mahusiano, ngono na matumizi ya madawa ya kulevya.

Usununu uisokuwa na sababu Mwanao ghalfa tu anakuwa mkali au mkimya na ‘mkorofi’ asiyetaka ‘kukusikiliza’. Humjui tena! Usikate tamaa onyesha kujali kwa dhati mambo yanayohusu maisha yake.

Anaegemea zaidi ushawishi wa makundi-rika. Humuoni mpaka unapokutana naye huwa na ‘wenzake’ katika ‘mambo yao.’ Panga kuwafahamu rafiki zake. Wataalamu wa malezi wanashauri uweke bidii katika kuwafahamu marafiki zake kwani ‘mustakabali’ wake uko juu ya maamuzi yao.

Mtoto kukata tamaa na kukosa ari ya kusoma. Msongo wa mawazo unaotokana na kutojua majibu ya maswali mengi aliyonayo mtoto hupelekea kupoteza mwelekeo na hata kukata tamaa.

Zungumza naye huku ukijiepusha na makaripio. Namna hii atapata faraja na kuelewa kuwa yuko katika umri wa mpito na kuwa sasa utu uzima unaingia na majukumu yanazidi kuwa mengi.


Sema Tanzania
 
Back
Top Bottom