KERO Changamoto za Mfumo wa Ajira Portal kwa Vijana Wanaotafuta Ajira

KERO Changamoto za Mfumo wa Ajira Portal kwa Vijana Wanaotafuta Ajira

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaiomba mamlaka husika kuboresha mfumo wa Ajira Portal. Vijana wengi tunapata changamoto kubwa kupata usaidizi kuhusu mfumo huo kwani namba za mawasiliano hazifanyi kazi na email hazijibiwi.

Hali hii inatulazimu kutumia fedha nyingi kwenda Dodoma kwa ajili ya kupata msaada wa huduma ambazo zingeweza kutolewa karibu nasi.

Tunaomba kuwepo kwa ofisi za Ajira Portal angalau kwa kila kanda ili kupunguza usumbufu na gharama kwa vijana wanaotafuta ajira.
 
waombaji wengi tunapitia changamoto kubwa ya kushindwa kuwasilisha maombi yetu kupitia mfumo wa Ajira Portal kwa sababu mfumo unakataa kusasisha taarifa zetu binafsi,(personal details)na tunapojaribu tunapata ujumbe kuwa namba zetu za NIDA zimeshasajiliwa kwenye akaunti nyingine ambazo hatuzitambui, huku Kitengo cha Huduma kwa Wateja pia hakipokei simu zetu licha ya kuwa na changamoto nyingi zinazotuhitaji msaada wa haraka.Tunaomba mamlaka husika itutatilie hili
 
Changamoto nyingi ni solvable (zinatatulika) ndugu.
Mifano Mimi nimetatua changamoto za watu kama vile:
1.Kusahau email
2.Kusahau password
3.Kushindwa kuapply
4.changamoto ya nida kwenye mfumo nk

Izo ni pamoja na ushauri
Kama Bado una changamoto au kuna mtu ana changamoto kama izo tuwasiliane kwa
0623446608
Au

0792715343
 
Back
Top Bottom