KERO Changamoto za mfumo wa Ajira Portal zinachochea Matapeli kuigeuza fursa!

KERO Changamoto za mfumo wa Ajira Portal zinachochea Matapeli kuigeuza fursa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

the ultimatum

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2012
Posts
420
Reaction score
143
Ndugu wana jukwaa napenda kueleza kwa ufupi sana kusikitishwa kwangu na mfumo mbovu wa secretariat ya ajira yaani Ajira Portal.

Ajira Portal wameweka utaratibu kwamba ili u qualify kuomba kazi ni lazima walau profile yako ya Ajira Portal, wenyewe wanaita dashboard ifikishe walau 70% na ili ufikishe asilimia hizo unatakiwa ujaze maeneo yote muhimu. Mimi ni muhanga wa hiyo changamoto, kwani nimejaza maeneo yote bila kuacha gape lolote lile lakini nimefikisha asilimia 60 tu kwahiyo nanyimwa haki ya kuomba kazi kwa kigezo hicho.

Sielewi ni kwanini wameweka huo utaratibu. Nimejaribu kupiga simu kwenye namba zao za msaada walizoweka kwenye tovuti yao, simu inaita bila kupokelewa. Nimejaribu kutuma email kupitia email ya (support) waliyoweka hii inaenda wiki ya pili sasa haijibiwi na wala changamoto zangu hazitatuliwi.

Lakini kubwa kati ya yote kuna barua ambayo inasambaa kupitia ukuraha wa Facebook wa TANGANYIKA HURU ambayo inaonekana kwa heading zake kuwa inatoka Ajira Portal ikiwataka watu kuhuisha taarifa zao na kama kuna changamoto wameweka namba za simu za kupiga. Ni kupitia namba hizo nimetapeliwa TSH. 35,000 katika harakati za kutatua changamoto ambayo nimeeleza.

Nimeambatanisha hiyo barua hapa ili nanyi muione.

Hatua nilizochukua;

Kwa takribani wiki ya pili sasa nimewaandikia katika ukurasa wao wa Twitter (X) ORTAMISEMI na UTUMISHI kuelezea hizo changamoto lakini pia kuwaomba ufafanuzi wa barua hii. Lakini pia nimewatag jeshi la Polisi ili wajaribu kufuatilia kujua ukweli wa barua hiyo kupitia intelijensia zao.

Tunawaomba sana Ajira Portal mshughulike na changamoto tunazowaletea iwe kwa simu au email. Tunaomba muangalie upya mifumo yenu, inaonekana ipo domant sana, na kama mnanisoma hapa basi naomba mshughulike na swala langu. Nimejitahidi sana kutumia njia zote stahiki mlizoweka katika mifumo yenu ya kupeleka changamoto bila mafanikio kabla ya kuweka taarifa hii hapa.

Tafadhalini nawaomba sana muuleze umma wa watanzania kuhusu barua hii inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kama inahusisha utapeli basi mjue ni watanzania wengi masikini wanatapeliwa na hili halikubaliki katika jamii iliyostaarabika.

FB_IMG_1748861906932.jpg

Ahsanteni.
 
Nichek inbox saivii nikusaidie tatizo lako sitokuomba hata mia maake naona umeteseka Sana kwa tatizo dogo sana
 
Umeapload vyeti vyote vinavyohitajika na una uhakika vipo na unaweza kuvidownload tena
 
WEWE HUONI HIYO UNAYOSEMA BARUA INA MAPUNGUFU...imekaa kitapeli...

Eti mwishoni signature.

Katibu mtendaji
Ajira portal makao makuu dodoma.

Alafu siku nyingine acha ujinga...hawatozi hela...alafu simu za serikali ukiacha tanesco tu...zimekaaga ushahidi tu pale..hazina kazi yoyote pale...hazipokelewagi...

Cha msingi pambana na wajuzi wakusaidie physically lazima kuna kitu hakipo sawa...
 
Hapo kwenye kutapeliwa ni ujinga wako mwenyewe, wajanja wamekupata ukapatikana.

Anyway, angalia kwa makini ulipojaza, ni lazima kuna mahali hujapajaza.
 
Interview dogo anafanya tarehe 08. 06.2025 Mpaka sasa hawajaweka kituo Cha kufanyia kwenye account yake na anafanya online imekaaje mbona hawaweki vituo mapema watu wakajipanga kuna wengine inabidi wasafiri.
 
Wataweka tu, cha msingi ajiandae saivi hicho ndo cha muhimu
 
Ndugu yangu pole sana kwa kutapeliwa, inawezekana ulipanic ndio maana ukashindwa kuona kuwa barua hiyo ina mapungufu mengi na sio ya Utumishi. kikubwa jitahidi sana kuwa makini na vitu kama hivi, mara nyingi tunaambiwa kuwa hakuna utaratibu wa kutoa hela ili usaidiwe changamoto zako.

Kwanza, HAKUNA Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma bali ni KATIBU.
Pili, Taarifa zao huwa zinatolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini.
Tatu, hakuna kitu kinaitwa AJIRA PORTAL MAKAO MAKUU DODOMA
Mwisho japo si kwa umuhimu ni hiyo signature 😀😀, eti myson.

Kiufupi hiyo barua haiko sawa mwanzo mwisho. Pole na naamini changamoto zako zitatatuliwa.
 
Mkuu umeweka namba yako ya NIDA vizuri?
NA ukajibu Yale maswali wanayo kuuliza kuhusiana na taarifa zako za NIDA?
Sehemu ya NIDA inachukua % kubwa Sana
Aisee mimi pale sehemu ya nida number inanikatalia inasema my nida number has already been used sijui nifanyeje
 
Aisee mimi pale sehemu ya nida number inanikatalia inasema my nida number has already been used sijui nifanyeje
ulishawahi kuwa na akaunti zaidi ya moja mkuu ndio maana unambiwa hivyo nida hutumika mala moja tu watafute utumishi wakusaidie kuifuta akaunti moja ambayo huitumii sasa hivi mkuu
 
Kama umetapeliwa kizembe hivyo ni lazima mfumo ukusumbue kwa sababu inaonesha una uwezo mdogo sana
 
WEWE HUONI HIYO UNAYOSEMA BARUA INA MAPUNGUFU...imekaa kitapeli...

Eti mwishoni signature.

Katibu mtendaji
Ajira portal makao makuu dodoma.

Alafu siku nyingine acha ujinga...hawatozi hela...alafu simu za serikali ukiacha tanesco tu...zimekaaga ushahidi tu pale..hazina kazi yoyote pale...hazipokelewagi...

Cha msingi pambana na wajuzi wakusaidie physically lazima kuna kitu hakipo sawa...
Pharmacy council wanapokea. Don't fool majority for your Own experience.
 
ulishawahi kuwa na akaunti zaidi ya moja mkuu ndio maana unambiwa hivyo nida hutumika mala moja tu watafute utumishi wakusaidie kuifuta akaunti moja ambayo huitumii sasa hivi mkuu
Simu hawapokei wala kujibu email,nafanyeje mkuu
 
Back
Top Bottom