Ndugu wana jukwaa napenda kueleza kwa ufupi sana kusikitishwa kwangu na mfumo mbovu wa secretariat ya ajira yaani Ajira Portal.
Ajira Portal wameweka utaratibu kwamba ili u qualify kuomba kazi ni lazima walau profile yako ya Ajira Portal, wenyewe wanaita dashboard ifikishe walau 70% na ili ufikishe asilimia hizo unatakiwa ujaze maeneo yote muhimu. Mimi ni muhanga wa hiyo changamoto, kwani nimejaza maeneo yote bila kuacha gape lolote lile lakini nimefikisha asilimia 60 tu kwahiyo nanyimwa haki ya kuomba kazi kwa kigezo hicho.
Sielewi ni kwanini wameweka huo utaratibu. Nimejaribu kupiga simu kwenye namba zao za msaada walizoweka kwenye tovuti yao, simu inaita bila kupokelewa. Nimejaribu kutuma email kupitia email ya (support) waliyoweka hii inaenda wiki ya pili sasa haijibiwi na wala changamoto zangu hazitatuliwi.
Lakini kubwa kati ya yote kuna barua ambayo inasambaa kupitia ukuraha wa Facebook wa
TANGANYIKA HURU ambayo inaonekana kwa heading zake kuwa inatoka Ajira Portal ikiwataka watu kuhuisha taarifa zao na kama kuna changamoto wameweka namba za simu za kupiga. Ni kupitia namba hizo nimetapeliwa TSH. 35,000 katika harakati za kutatua changamoto ambayo nimeeleza.
Nimeambatanisha hiyo barua hapa ili nanyi muione.
Hatua nilizochukua;
Kwa takribani wiki ya pili sasa nimewaandikia katika ukurasa wao wa Twitter (X) ORTAMISEMI na UTUMISHI kuelezea hizo changamoto lakini pia kuwaomba ufafanuzi wa barua hii. Lakini pia nimewatag jeshi la Polisi ili wajaribu kufuatilia kujua ukweli wa barua hiyo kupitia intelijensia zao.
Tunawaomba sana Ajira Portal mshughulike na changamoto tunazowaletea iwe kwa simu au email. Tunaomba muangalie upya mifumo yenu, inaonekana ipo domant sana, na kama mnanisoma hapa basi naomba mshughulike na swala langu. Nimejitahidi sana kutumia njia zote stahiki mlizoweka katika mifumo yenu ya kupeleka changamoto bila mafanikio kabla ya kuweka taarifa hii hapa.
Tafadhalini nawaomba sana muuleze umma wa watanzania kuhusu barua hii inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, kama inahusisha utapeli basi mjue ni watanzania wengi masikini wanatapeliwa na hili halikubaliki katika jamii iliyostaarabika.
View attachment 3353561
Ahsanteni.