Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Nataka kubadilisha attachment ya cheti Cha kuzaliwa kwenye taarifa binafsi, nafanyaje wakuu au ndo imekula kwangu mana nimekosea
Kwenye attachment ya cheti Cha kuzaliwa nimeweka cheti kingine
Kuna option ya kufuta/toa
 
Sasa ndugu zangu walimu na manesi hapa kosa la mtu wa IT ni lipi jamani?

Mbona mnapenda kutoa lawama sana.Haya unataka mtu wa IT afanye nini cha ziada hapa?

Nakupa elimu ya bure ili siku nyingine kabla ya kuponda IT wa bongo ujue nini kiko nyuma ya pazia.

Ni kwamba unapoingia kwenye browser yako na kutype address yako kwa ajili ya page hiyo ya maombi.Browser yako ndio inakuwa mteja na mhudumu wake ni hizo servers ambazo zina hiyo page.Ombi lako linapochelewa kushughulikiwa ni kwamba unakuwa umewekwa foleni kwa sababu server inakuwa imepokea maombi mengi na kila ombi linalotumwa linakuwa na mda wake wa kusubiri kabla ya kujibiwa.Mda wa kusubiri unaokuwa umepewa ukiisha bila kuhudiwa wewe unakuwa umetolewa kwenye foleni.

Sasa kama kwa kifupi sana jambo liko hivi kosa la IT wa bongo ni lipi sasa hapa?
Mkuu upo serious au una nijibu kwa majibu ya utani.

Kwamba wanashindwa kuboresha mfumo, mfumo unakuwa na changamoto amabazo ni aibu tu kuzielezea.
Mfano. Unaattach docoment zen mwisho wa siku unaambiwa huku attach.

Kiufupi: bado tupo nyuma ya teknolojia.
Mifumo ya serikali huwa ni shida tu ukienda TRA , nako shida.

Tukubaliane kuwa serikali haipo serious wapo wapo tu.
 
Habari zenu?Binafsi sijakamilisha Bado kwa sababu ya ile sehemu ya kuambatanisha nyaraka za chuo!Nauliza tu endapo pdf zangu hazijafika 2MB inaweza ikaniletea shida ya kukosa sifa ya kuchaguliwa?(Kwa kuwa mafaili yote niliyotuma mpaka Sasa Ni chini ya 2 MB)!Ni hayo tu wadau
Mwaka huu hawajaandika limit ya MB, but mwaka juzi walisema isizidi 2MB
So inatakiwa iwe FILE CAPACITY≤2MB
 
Jamani mie najaza details za NIDA mda wote inasema umekosea. Nifanyeje
 
Chagua Dar. Wengi wanaikwepa wakijua hawawezi kuchaguliwa kwahiyo utajikuta upo pekee ako
Hahahaha Dar hapana aisee, lkn kama mikoa uliyochagua ikishindikana c unaweza kupangiwa mikoa mingine huko huko na Tamisemi au.?
 
Back
Top Bottom