Ilikuwa ni siku ya krismasi, Baba anamleta mwanamke nyumbani na kumtambulisha kwa lazima na madaha kwetu. Akimwambia mama "Huyo ndio mke mwenzako muheshimu".
Kabla ya hapo huyu mwanamke alikuwa mchepuko wa mzee, akazaa nae, na baadae akawa akawa ni mchepuko wa mzee, nahisi mzee alinogewa na shepu la yule mama, angali hata alikuwa ana mtoto (aliezaa na mwanaume mwingine) ila mdingi alimfanya official.
Mzee wangu alimnyanyasa sana mama yangu hata mbele yetu. Kusahau juhudi ya mama ndio ilikuwa sababu ya mzee kufika alipo (na hata pesa ya kuwa na jeuri ya kuoa mke mwingine). Alijitamba sana kuwa huyo mwanamke ndio aina ya mwanamke aliekuwa ana hitaji na kwa mama yangu alikosea step. Huyu mwanamke (mke wa pili) ili alinde nafasi yake alijitahidi zaidi katika ushirikina na vioja vingi vya kumharibia mama yangu.
Ilifika wakati mama aliondoka nyumbani. Maisha ya kuona mama ananyanyasika na baade ile hali ya kumkosa mama ilituathiri sana watoto kisaikolijia hadi katika elimu. Hatimaye biashara za mzee zilianza kufeli na mambo yake yakaanza kwenda vibaya, na ilionekana wazi kuwa baraka za huyu mzee ni kutokana na uwepo wa mama.
Wadogo zangu walikuwa wadogo sana, na malezi ya huyu mama hayakuwa original kwa wadogo zangu. So mama aliamua kusacrifice furaha yake na kuja kurudi ili akae atuleee ili hali alijua bado atakutana na kero.
Lakini yule mwanamke hakuwa kama vile mzee alivyotegemea, kama ni tabia mbaya aliionesha hata mara tano zaidi ya mama yangu. DAYS ARE NUMBERED! Yani huyu mwanamke ambae alikuwa anaonekana kama sweetheart wa mzee, Mzee alimfumania meseji za mapenzi kutoka kwa mmoja wa wateja wake na inasemakana kipindi huyu mzee alipokuwa hayupo huyu mwanamke alikuwa anaenda kujivinjali usiku na awala yake. hahah ...Mdingi alipiga akataka kuua na ilimuuma sio kawaida hadi akaita ndugu zake.
■WANAWAKE
JIULIZE, KWANINI MWANAMKE AKUBALI KUOLEWA KAMA MKE WA PILI KAMA SIO AMEKOSA UTU AU KUTAKA MTELEMKO WA MAISHA KWA KUWA WANAUME WALIOKWISHA KUOA UNAKUTA WAMESHATOKA KIMAISHA. MARA NYINGI MNAKUJA KUHARIBU MAISHA YA FAMILIA YA MKE YULE NA WENGI WENU MNAHAKIKISHA NAFASI MAALUM MNAISHIKA NYIE, SO MNAHANGAIKA KWA WAGANGA.
■MWANAUME
HAKUNA SABABU YOTOTE YA KUWA MKE ZAIDI YA MMOJA, HAWA WANAWAKE NI WALE WALE NA HATA HUYO WA PILI ATAKUWA NA MAPUNGUFU PIA. NA KWA SISI WAKRISTO TUNAAMINI KUWA MUNGU ANAFANYA AGANO NA NDOA YA MKE WA KWANZA NA UZAO WA KWANZA.
Sent using
Jamii Forums mobile app