Mada ingekuwa hainihusu usingeiweka kwenye jukwaa huru, ungejadili nyumbani kwako na shemeji yako, ukiileta jukwaani maana yake public inahusika.
Nia yangu wewe na wenzio mbadili mtazamo na mjifunze kuheshimu watu wengine. Dada wa kazi ni binadamu tu kama wewe, anapaswa kuheshimiwa. Kumjadili madhaifu yake as if hayo madhaifu binadamu wengine hawana ni spesho tu kwa dada wa kazi huo ni ujinga.
Mtu yeyote anayetoka kijijini akifika mjini akakutana na vitu vipya, na mazingira mapya lazima atastruggle. Sasa kumfanya kituko ni dalili ya umaskini wa fikra, yaani unaamini wewe ni superior kwa yeye kuwa inferior. Huo ndio 'uhindi' na ndio mnachojadili hapa mkipongezana to the extent mwenzenu mmoja amethubutu kufikia kusema yeye wa kwake kituko chake ni KUKAA KWENYE MAKOCHI NA KULA PAMOJA DINNING kwa maana hiyo hastahili kula nao na asikae kwenye makochi? Sasa hapa unajiuliza, mnamzungumzia MBWA au binadamu?!
Sisi sisi tunatokwa mishipa ya koo kuwalaani wazungu kwa ukoloni, tunawalaani waarabu wanaowabagua dada zetu na kuwatesa, lakini majumbani mwetu hizi ndio treatment tunazowapa our own kind. Yaani akale jikoni na sio dinning? So low and selfish. Na unayenishangaza zaidi ni wewe mtoto wa kiume, hizi roho za saluni wanaume hatuna, unapata wapi haya dogo? Juzi ulikuwa mtetezi mzuuuri wa singo maza, leo wewe na singo maza mna team up kuongea mambo yasiyo sahihi juu ya watu wengine kwa kuwa tu hawakubahatika kuwa na shemeji kama wako wakaishia hapo kwa dadako kwa status tofauti na yako? Come oooooon boy, Have mercy for your father...he should be proud of you when you display masculine behaviors dear boy, achana na hii kitu.