Changamoto za Wivu na Chuki: Mwaliko wa Kujenga Jamii Inayothamini Mafanikio

Changamoto za Wivu na Chuki: Mwaliko wa Kujenga Jamii Inayothamini Mafanikio

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Katika pitapita zangu za hapa na pale nimekuja kugundua kwamba...baadhi ya wananchi wenzangu wa kitanzania wanapendelea kuona wenzao wakishindwa katika maisha, badala ya kufurahia au kuwahamasisha kufanikiwa zaidi (samahani chuki hii mimi naiita "wana roho ya kichawi")...

Wengi huombea wenzao kupata anguko, ndiyo furaha yao...

Mara nyingi, mtu akizidiwa kwa uwezo kazini, biasharani, au katika masuala ya kiroho, au kijamii, hukabiliwa na chuki na wivu usiomithirika!!!...Mifano michache ni kama ifuatavyo:-

  • Matajiri/wenye kipato bora; hushutumiwa kuwa na utajiri/kipato haramu, kama vile wizi au kukwepa kodi.
  • Watu wachapakazi na wabunifu; mara nyingi husemwa kuwa wanajipendekeza kwa mabosi/wanajifanya wajuaji; hufikiwa hatua ya kutengenezewa fitina kazini, hadi kuzuiwa kupata nafasi za uongozi kwa sababu wengine hawataki kuongozwa na mtu mwenye uwezo mkubwa (Hili alishawahi kuligusia Mchengerwa...kwamba mabosi baadhi hawapendi watu "smart" wanataka akina bora liende)
  • Wanaozingatia kufanya Ibada; wale wanaojitolea sana katika ibada husemwa kuwa wanajifanya watakatifu kupita kiasi...hufikia hatua baadhi ya hawa "wachawi" kuwaita majina yasiyopaswa kwamba "eti wanajifanya wao ni mitume"
  • Wakulima hodari na wabunifu; hukejeliwa na kupuuzwa.
  • Watu wanaozingatia maadili ya jamii; hawa huonekana wamepitwa na wakati, washamba na wasiojitambua
  • Watu wasiopenda elimu; hawa huonekana kwamba ndiyo watu timamu, ila anaependa elimu au kusomesha jamii yake huonekana hamnazo utasikia "kusoma bongo?" au "john kisomo" nk...wakati kule Kenya majirani wanachangia ada mtoto akasomeshwe nje ya nchi kupitia wakfu wa 'harambee' hapa kwetu elimu kwa baadhi/wengi ni ushamba na haitakiwi...
Kinyume chake, watu wanaoonekana kuendekeza ujingaujinga au wanaoendeleza tabia zisizo na maana kama vile uzinzi,ulevi,ubadhirifu,wizi,matusi,uchawa nk, hawa hupendwa na kuungwa mkono pakubwa na jamii yetu hasa jamii ya vijana (mostly Generation Y (Millennials) na Generation Z (Zoomers).

Tukubaliane na ukweli kwamba tuna tatizo kubwa hasa kwa vijana wengi katika zama hizi, viongozi wa vijana wengi hawachukui mambo kwa uzito na badala yake hujihusisha na vitendo visivyo na tija na kuwahamasisha vijana kwenye hivyo...

Jamii yetu ina changamoto ya kuthamini maendeleo kwa sababu wale wenye ushawishi mkubwa mara nyingi ni wale wanaokumbatia mambo yasiyo na tija kwa jamii (uchawa).

WITO WANGU:

Lea watoto wako kuepuka kuwa sehemu ya jamii inayoona ujinga kama mtindo unaofaa wa maisha. Watoto wafundishwe kufurahia mafanikio ya wengine kwani ndiko kufanikiwa kwa jamii yote. Si sawa Mtanzania kuchukia mafanikio ya Mtanzania mwenzake. Chuki huwa haifichiki...tuna tatizo kubwa la kuchukiana hasa kwa kigezo cha tofauti ya mafanikio. Tubadilike.
 
Back
Top Bottom