#COVID19 Chanjo milioni moja hazijaisha tu?

#COVID19 Chanjo milioni moja hazijaisha tu?

Kituko ni waliokua wanapayuka leteni chanjo ni hiari sisi tutachanja HAWAJACHANJA..
Takwimu za walioxhanja zinatia aibu...mpaka serikali ni kama imekata tamaa..
 
Acha unafiki wewe msukule wa Gwajima,watu tumechanjwa na Wala hakuna madhala yoyote, zaidi utendaji kazi wa baadhi ya mambo umeongezeka mara elfu mwilini
Hahaa kumbe nguvu za kiume kwa familia yako tabu unaamua kuzisaka kwenye chanjo ya korona, ngoja tukusaidie kazi, maana utachoma had chanjo ziishe na nguvu hakuna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaani kwetu,kuna wazee wengi sana tena wengine wana magonjwa nyemerezi ya kisukari,presha, lakini toka wimbi la kwanza mpaka sasahivi wote wanadunda,wewe kamwamashishe Baba yako na ukoo wenu wote, wengine tumekataa kufanyiwa majalibio.Nasikia Zanzibar inabidi warudie chanjo ya mwanzo haifahi 😀😄😃😃
Kama usemavyo kwamba mtaani kwenu wapo wazee wengi tena wana matatizo ya afya washauri waende wakachanjwe, vinginevyo muda ni mwalimu mzuri, Corona haina utani na wazee wenye matatizo ya kiafya, USIWAPUMBAZE
 
Kuna kitu hakiko sawa kwenye chanjo za J&J in term of efficacy kulinganisha na chanjo nyingine za Uviko 19, ila nilisikia bakabaka na askari wengine walichanjwa kwa nguvu, nje ya hapo unatengwa.

Bora tungeendelea kuyaishi maneno ya Hayati Tanzania ingeendelea kuwa salama.
Kama ulimuangali mkuu wa majeshi na hata Sirro siku ile wakichanjwa unaona kabisa walikubali tu hivyo hivyo.
 
Hii chanjo imetuumbua, Dunia imeshatujua kuwa Watanzania bado tupo nyuma sana kielimu, ni watu wa kusikiliza sana maneno ya vijiweni na ni wepesi sana wa kukaririshwa uongo, Hivi haya mataifa yote yaliyoendelea duniani yanawachanja RAIA wao yana nia mbaya na RAIA wao ? Hii haihitaji elimu ya chuo kikuu kugundua bado tuko nyuma sana kielimu
Sijajua kwanini unasema hivyo wakati hata huko kwa wenzetu kuna hadi manesi wamefukuzwa kazi kwa kugoma kuchanjwa yani kwa kifupi hata huko watu wanaogoma wapo.
 
Kituko ni waliokua wanapayuka leteni chanjo ni hiari sisi tutachanja HAWAJACHANJA..
Takwimu za walioxhanja zinatia aibu...mpaka serikali ni kama imekata tamaa..
Ilikuwa inaonekana kwamba kikwazo ni Magufuli tu ndio anakwamisha watanzania kukosa kuchanjwa ila chanjo zimekuja wakuchanjwa wanatafutwa.
 
Kama usemavyo kwamba mtaani kwenu wapo wazee wengi tena wana matatizo ya afya washauri waende wakachanjwe, vinginevyo muda ni mwalimu mzuri, Corona haina utani na wazee wenye matatizo ya kiafya, USIWAPUMBAZE
Mkuu unaongea kana kwamba corona imeingia juzi tu Tanzania kumbe toka mwaka jana ipo halafu sasa ndio et unaona hao wazee watakufa wasipochanjwa, kitu kinachonishangaza ni kwamba watu mshasahau kuhusu kujikinga na corona ili kuzuia maambukizi kitu ambacho unatakiwa kufanya hata baada ya kuchanjwa naona mmekazana kuambiana kuchanja tu.
 
Siku moja nilimsikia mheshimiwa sana waziri wangu wa Afya akisema watu wanajitokeza kwa wingi kudungwa kuliko walivyo tarajia, siku nyingine nikamsikia mheshimiwa sana Rais Samia Suluhu akisema kuwa kinacho muumiza kichwa kwasasa ni wapi watapata chanjo zaidi, maana kwa jinsi hizi za awali zilivyo changamkiwa ni wazi kuwa hazitoshi.

Swali langu ni jepesi tu, endapo watu wanajitokeza kwa kasi hiii, mbona haziishi? Yaani pamoja na kuziandalia siku maalumu pale uwanja wa taifa, pamoja na timu zetu kuhamasisha mashabiki wake, pamoja na vyombo vya habari kuzipa promo, pamoja na viongozi wa Bunge kuhamasisha, pamoja na wasanii kuzitungia nyimbo lakini hazijaisha mpaka leo.

Nini tatizo? Waziri wa Afya na naibu wako mnakwama wapi?
Kwani hao wasanii na ndugu zao jumla yao ni ngapi!! Wameshaishiwa nguvu, sasa hivi wanapambana na Gwajima wanajua yeye ndo chanzo!! Wameliwa na hadi mwaka huu unaisha hizo milioni moja haziishi...
 
Chanjo zimewadodea, sasahivi Watanzania sio mapompoma tena,hao mawaziri wawadunge watoto wao,huku kwetu mtaani corona tunaisikia redioni na kwenye matangazo ya tv,sasa nidungwe sumu za nini, wakati corona tangu imeingia sijawai kutana na mgonjwa wa corona,hata mtaani kwangu sijawai kusikia kifo cha mgonjwa wa corona.R.i.p Magufuri kwa kutuambia ukweli,hata ifike wimbi la kumi atuogopi
Kummammaee zao!!
 
Hata mimi kwa kweli niwe mkweli sijawahi kusikia mtu ninayefahamiana nae kabisa amefariki kwa Covid. Ninasikiaga tu kwa watu wakisema. Na hao wanaosema wanasikiaga pia[emoji23][emoji23][emoji23]

Na hata kama wanakufa, takwimu zinaonesha wanaokufa haizidi hata 2% ya wote wanaougua. Yaani 98% wanougua wanapona, achilia mbali ambao hawajaumwa[emoji3][emoji3][emoji3]

Na hao 2% (ya wanaougua tu, sio ya watu wote) wanaokufa, katika hiyo 2% humo ndani yao kuna wazee, wenye magonjwa mengine sugu, n.k.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Kwa maana hiyo wanaokufa wakiwa wazima kabisa bila kuwa na matatizo mengine unaweza kukuta hawafiki hata 1%[emoji23][emoji23][emoji23]

Alafu bado wanakulazimisha chanjo. Matangazo yote yanatutia hofu,viongozi wote wanatutia hofu. Hakuna anayetueleza upande mwingine wa kutochanjwa na kutokufa. Lengo lao ni tudungwe tu. Inaonekana kuna biashara kubwa ya watu, na woga wa kupoteza madaraka kwa wenye nyadhifa kiasi kwamba wanaona namna ya kubaki salama ni kuhakikisha watu wao wanadungwa tu.

Mi nitakuwa wa mwisho kuchanjwa.
Yaani ukifatilia kiundani kwa akili yako bila kuvurugwa na uvumi wowote, utacheka sana kuhusu huu uhuni nanutapeli.

Safi mkuu
 
Ilikuwa inaonekana kwamba kikwazo ni Magufuli tu ndio anakwamisha watanzania kukosa kuchanjwa ila chanjo zimekuja wakuchanjwa wanatafutwa.
Ndo wajue kuwa wameeua Mtanzania halisi Magufuli, hao wengine ni wa kwào..watanzania halisi tunajijua
 
Je Chanjo zinaexpire lini?
Una maana Serikali inaweza kuwachanja Watu chanjo iliyokwisha muda wake ? Au kuwapa dawa yeyote iliyo- expire ? Kweli unaaminishwa inaweza ikafanya unyama kama huo ? HAIWEZEKANI KABISA KABISA, NENDENI MKACHANJWE JAMENI !!
 
Hii chanjo imetuumbua, Dunia imeshatujua kuwa Watanzania bado tupo nyuma sana kielimu, ni watu wa kusikiliza sana maneno ya vijiweni na ni wepesi sana wa kukaririshwa uongo, Hivi haya mataifa yote yaliyoendelea duniani yanawachanja RAIA wao yana nia mbaya na RAIA wao ? Hii haihitaji elimu ya chuo kikuu kugundua bado tuko nyuma sana kielimu
Mbaya zaidi watumishi wa afya ndiyo hawataki hata kuisikia hii chanjo
 
Hii chanjo imetuumbua, Dunia imeshatujua kuwa Watanzania bado tupo nyuma sana kielimu, ni watu wa kusikiliza sana maneno ya vijiweni na ni wepesi sana wa kukaririshwa uongo, Hivi haya mataifa yote yaliyoendelea duniani yanawachanja RAIA wao yana nia mbaya na RAIA wao ? Hii haihitaji elimu ya chuo kikuu kugundua bado tuko nyuma sana kielimu
Ndugu uko dunia hii hii au? Kwamba wewe nchini kanada ni asilimia 30 tu wamepata chanjo asilimia 70 wawajapata fuatilia ijekua Kua bongo.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Ndo wajue kuwa wameeua Mtanzania halisi Magufuli, hao wengine ni wa kwào..watanzania halisi tunajijua
Tulikuwa tunauliza hapa hao watanzania wanaotaka chanjo wako wapi? wakawa wanasema wako wengi wanaotaka chanjo,haya wameletewa hizo chanjo matokeo yake wanasema watu wanapotosha wakati wenyewe walizitaka toka kipindi cha Magufuli sasa leo Magufuli hayapo hao waliyotaka chanjo wanapotoshwa vp tena? si ajabu hata hawa waliyokuwa wanalilia chanjo humu wengi hawajachanja.
 
Hawana mchezo ndiyo maana kwao corona siyo issue tena
Ingekuwa kwao corona sio issue tena basi wasingekuwa wanatumia nguvu tena kiasi hicho mambo hayo tunatakiwa tufanye sisi huku.
 
Back
Top Bottom