Hata mimi kwa kweli niwe mkweli sijawahi kusikia mtu ninayefahamiana nae kabisa amefariki kwa Covid. Ninasikiaga tu kwa watu wakisema. Na hao wanaosema wanasikiaga pia[emoji23][emoji23][emoji23]
Na hata kama wanakufa, takwimu zinaonesha wanaokufa haizidi hata 2% ya wote wanaougua. Yaani 98% wanougua wanapona, achilia mbali ambao hawajaumwa[emoji3][emoji3][emoji3]
Na hao 2% (ya wanaougua tu, sio ya watu wote) wanaokufa, katika hiyo 2% humo ndani yao kuna wazee, wenye magonjwa mengine sugu, n.k.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa maana hiyo wanaokufa wakiwa wazima kabisa bila kuwa na matatizo mengine unaweza kukuta hawafiki hata 1%[emoji23][emoji23][emoji23]
Alafu bado wanakulazimisha chanjo. Matangazo yote yanatutia hofu,viongozi wote wanatutia hofu. Hakuna anayetueleza upande mwingine wa kutochanjwa na kutokufa. Lengo lao ni tudungwe tu. Inaonekana kuna biashara kubwa ya watu, na woga wa kupoteza madaraka kwa wenye nyadhifa kiasi kwamba wanaona namna ya kubaki salama ni kuhakikisha watu wao wanadungwa tu.
Mi nitakuwa wa mwisho kuchanjwa.