#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Acheni ukuda wenu.
Mimi nikifa wewe unaumia nini? Lazima lazima ndio sitakufa au?

Acheni mambo ya ajabu bana. Hata wakisema leo lazima, sichanji ni bora waniue kuliko kuchanja.

Et unachanja kisa li ugonjwa la kutunga. Ujinga bana. Nikichanja then what? Sitaumwa? Sitakufa? I fear nothing to die when right time comes..
Tena weye unatakiwa utandikwe na viboko vya shingoni hadi upate chanjo.😝😝😝😝😝
 
To be honest siko tayari kuchanjwa.......

Mkuu huo ni uchaguzi wako. Mapema kwa mwuungwana kama wewe niliandika hii:

IMG_20210719_184727_684.jpg

Kwamba sana sana Mbowe hakuwa na haja ya kuingia huku kisiasa, lakini si morally au kiuhalisia.

Kwamba hata aliingia huku inaonesha ni kiwango kipi huyu bwana ni a real selfless individual.
 
Acheni ukuda wenu.
Mimi nikifa wewe unaumia nini? Lazima lazima ndio sitakufa au?

Acheni mambo ya ajabu bana. Hata wakisema leo lazima, sichanji ni bora waniue kuliko kuchanja.

Et unachanja kisa li ugonjwa la kutunga. Ujinga bana. Nikichanja then what? Sitaumwa? Sitakufa? I fear nothing to die when right time comes..

Uganda na Rwanda hapana kuendekeza ujinga. Huko wala si ukuda bali utachezea kichapo!

Kumbuka ujinga si tusi. Ni suala la kutokuelewa tu. Ujinga dawa yake ni elimu dunia tu mkuu.

Huku kwetu tutabembelezana kwanza, ila baadaye kutakuwa na vikwazo hapa na pale. Mdogo mdogo tutafika tu.

Hiyo ndiyo sayansi ya chanjo.
 
Uganda na Rwanda hapana kuendekeza ujinga.

Kumbuka ujinga si tusi. Ni suala la kutokuelewa tu.

Ujinga dawa yake ni elimu dunia tu mkuu.

Huku kwetu tutabembelezana baadaye kutakuwa na vikwazo hapa na pale. Mdogo mdogo tutafika tu.

Hiyo ndiyo sayansi ya chanjo.
Muulize ni nini kinachomfanya aikatae chanjo?
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!

Cc: BAK Erythrocyte technically Salary Slip Jumbe Brown Mshana Jr
Umetoa mfano wa Uganda na Rwanda, ebu tuambie mpaka sasa ni asilimia ngapi huko Uganda na Rwanda wamepata hizo chanjo? halafu ndio nitaendelea na swali la ziada
 
Umetoa mfano wa Uganda na Rwanda, ebu tuambie mpaka sasa ni asilimia ngapi huko Uganda na Rwanda wamepata hizo chanjo? halafu ndio nitaendelea na swali la ziada
Kwa hiyo ukipewa asilimia ndiyo zitakuponya na maradhi?Pokea chanjo acha maroroso.😝😝😝😝
 
Ndio shida ya misukule unaulizwa Data unaleta porojo , Uganda na Rwanda asilimia ngapi wamepata chanjo?
Data haitokusaidia weye!Utakaa unasoma data za wenzio huku unapangusa makamasi ya korona?Kuwa mwerevu.Pata chanjo.Mambo ya Uganda na Rwanda watahesabiana huko.
 
Watanzania, kwanini mnaogopa chanjo? Mbona ni kitu cha kawaida tu!

Alafu hapo kwenye "lazima" watu wanadhani utafuatwa nyumbani na maaskari na nesi akuchome kwa nguvu. Ulazima wa chanjo ni masuala ya sera na mipango tu!
 
Data haitokusaidia weye!Utakaa unasoma data za wenzio huku unapangusa makamasi ya korona?Kuwa mwerevu.Pata chanjo.Mambo ya Uganda na Rwanda watahesabiana huko.
Kusaidia au kutokusaidia hiyo sio kazi yako, lete hapa Data acha mboyoyo watu kiasi gani Rwanda na Uganda wamepata chanjo?
 
Watanzania, kwanini mnaogopa chanjo? Mbona ni kitu cha kawaida tu!

Alafu hapo kwenye "lazima" watu wanadhani utafuatwa nyumbani na maaskari na nesi akuchome kwa nguvu. Ulazima wa chanjo ni masuala ya sera na mipango tu!
Jamaa waoga wa kudungwa sindano.Wanaweza hata kuhama nchi.😂😂😂
 
Back
Top Bottom