#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

Jamani wilaya niliopo sijashudia kisa chochote cha Covid 19, sio wimbi la kwanza, lapili wala hili la tatu, kwahiyo huwa na jiuliza hiyo Corona inatuogopa watu wa maeneo haya niliyopo?
Ni wapi huko?
 
Kaa karantini wewe na familia yako. Kwani lazima uchangamane na wasiochanjwa.? Kama ni mwajiriwa chukua likizo ama uache kazi (kama ulivoshauri wasiochanjwa waache kazi) ili ujilinde dhidi yao
 
Chukulia assumption watu wote duniani ama Tanzania kwa mfano mdogo wangekubali kuchanja unajua serikali haina uwezo wa kuwafikia wote ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, sasa ungeweza tumia utaratibu gani kuwabagua watu hawa kiajira walio tayari kuchanja ila uwezo mdogo wa serikali kuwafikia umesababisha wao kutochanjwa? Ungewalipa mishahara ya bure ili wakae nyumbani hadi watakapopata chanjo? Ungewapelekea mahitaji yao ya kutosha milangoni mwao kwa sababu hutaki wachangamane sehemu za public wasije kusambaza virus?
 
Kaa karantini wewe na familia yako. Kwani lazima uchangamane na wasiochanjwa.? Kama ni mwajiriwa chukua likizo ama uache kazi (kama ulivoshauri wasiochanjwa waache kazi) ili ujilinde dhidi yao
Yaani niache kazi kwa ubishi wa kujinga kama wako wa kukataa chanjo? Hamna kitu kama hicho kutokea. Tutakupata tu na kukuchanja, la sivyo jifungie chumbani na mkeo tusikuone hadharani.
 
Wewe ni nani kuwapangia Moderators cha kuedit katika heading?

Wewe ni nani kuwataka watu wachanjwe?

Wewe ni nani kuwataja baadhi ya watanzania waache kufanya kazi zao kiss hawajachanjwa?
 
Kwani ukichanjwa halafu ukapata maambukizi unakuwa hauambukizi wengine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…