Sishangai wewe kutokusoma na kuelewa.
Maana wengi wenu humu mna uwezo hafifu wa kuchanganua mambo katika muktadha wake.
Na cha ajabu kuna wengine wanajiita majasusi humu. (sijui hata waliutoa wapi huo ujasusi?).
Tanzania inajulikana msimamo wake tangu kipindi cha Rais Magufuli kwamba imekataa kufuata masharti yaliyowekwa kupambana na huo ugonjwa wa kizungu unaoitwa corona.
Kisha mama samia akaunda kamati ili kupima kama huo msimamo wa Rais Magufuli uko sawasawa!
Kamati ikatoa majibu kwamba, msimamo uliowekwa na Rais Magufuli haukuwa sawasawa (as expected).
Unatarajia samia aende tofauti na hilo?
Kama angekuwa anatambua kwa dhati kwamba msimamo wa Rais Magufuli uko sawasawa, unadhani angeunda kamati?