Ni kweli mkuu kuna muumba na mm naamini hivoo lakini mada haijataka tujibu kwa dini 🤣🤣 wala sayansi bali tutunie akili zetuu
Unakubali ya kuwa akili ina ukomo ? Ulitakiwa ujue kwanza akili ni nini, ujue ukamilifu wa akili na udhaifu wake.
Ushawahi kujiuliza kwanini Wanafalsafa wa kale walikuja na majibu mengi juu ya swali Moja la chanzo Cha kila kitu ? Wapo walio sema chanzo Cha kila kitu ni Moto, wapo waliosema hewa, wapo waliosema Moshi, wapo walio sema Atomu, bali wapo waliosema namba wakaenda mbali wakasema ukamlifu unawakilishwa na namba kumi. Lakini wapo jaribu kuukaribia ukweli lakini wakakosea katika katika kuelezea mfano ni Aristotle aliyekuja na nadharia ya Prime Mover na zile ten Categories zake. Sasa Hawa walitumia akili na wakakosea sababu akili ina ukomo wake.
Sasa ufunuo Toka kwa yule aliye umba ukaja kutoa majibu ambayo akili imekomea, lakini Kuna ishara za kutumia akili na milango ya fahamu ambazo zipo ukiziangalia hizo unakubali ya kuwa Ulimwengu umeumbwa.