Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini?

Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini?

Umesema tutoe majibu bila rejea ya popote si dini wala sayansi. Kwa ufupi umesema jibu liumbwe na akili na si kutengenezwa kutoka majibu ambayo tayari yapo katika historia.

Nikuulize, unaweza kusema wewe ni nani bila rejea yoyote? Embu tuambie, wewe ni nani? Jibu bila kuwahusisha wazazi wako wala binadamu wengine waliosema wewe ni binadamu. Tuambie wewe ni nani?

Kama una jibu basi hata swali ulilouliza lina jibu, kama huna basi hakuna jibu bila kuchimba rejea.
Sahihi kabisaa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nashukuru nimesoma maoni yote!
Kama umepata like yangu, basj maoni yako ni ya thamani sana
 
Swali: Ukitoa principles zote za kisayansi unazozijua na usizojijua na Ukitoa imani zote za Dini zote unazozijua na usizozijua Je, Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini ?

NB; Uzi huu utawekwa kwenye record za Dunia kwamba ndio uzi pekee uliotaja chanzo cha Dunia, Uhai na ulimwengu bila kutaja principle zozote za Kisayansi au Imani (Dini)

Nawasilisha.

Ulitakiwa kwanza utuambie unawezaje kuelezea hilo jambo nje ya vitu hivyo viwili ? Hasa dini., ondoa utoto na nadharia za Kisayansi ambazo haziwezi Wala hazitokuja kuweza kuelezea chanzo Cha ulimwengu na ikawa sahihi.
 
Haya huyo mtamkaji yeye alitoka wapi na nini kilitumika kumuumba?

Nakuuliza swali rahisi sana, nipe sababu tatu ya kwamba aliyefanya ulimwengu ukawepo lazima awe ameumbwa ?

Unakubali Kuna infinity series ? Kwamba ina exist ?
 
Aahahahaha wewe una maoni gani kuhusu jambo hilo ili tupate pakuanzia kwanza

Mimi maoni yangu ni kuwa Dunia na vyote vilivyomo yupo aliye fanya vikawepo, na huyo aliyefanya vikawepo ana sifa hizi :

1. Mjuzi
2. Ana nguvu
3. Ana hekima
4. Hana chanzo
5. Mkamilifu
6. Ana huruma
7. Ana upendo
8. Muafilofu
9. Mwenye kubaki

Na sifa nyingine nzuri ambazo sijazitaja.
 
At least umeanza kuniaelewa nataka nini ? Mtu anatakiwa kujibu on his/her own free mind, ndio tutapata chanzo

Akili iliyo salama inakubali ya kuwa hii Dunia ina chanzo. Ukiona akili yako inapinga hilo ujue unafikiria kitoto au ni mgonjwa w akili au umeathiriwa na Wafalsafa.
 
Mimi maoni yangu ni kuwa Dunia na vyote vilivyomo yupo aliye fanya vikawepo, na huyo aliyefanya vikawepo ana sifa hizi :

1. Mjuzi
2. Ana nguvu
3. Ana hekima
4. Hana chanzo
5. Mkamilifu
6. Ana huruma
7. Ana upendo
8. Muafilofu
9. Mwenye kubaki

Na sifa nyingine nzuri ambazo sijazitaja.
Kwahiyo kwa kifupi unaamini katika uumbaji
 
Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na chanzo, Hata chanzo cha kila kitu lazima kiwe na chanzo chake kingine.

Hiki ulichokiandika inaonekana hujakifikiria vizuri.

Nakuuliza swali, je infinity ina exist ? Katika uhalisia ? Ulisema ina exist nitakuomba ushahidi na utupe marejeo na kama hai exist, basi unashida katika ufikiriaji yaani unafikiria kitoto.
Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo chanzo, Maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo pasipo chanzo
Uko sahihi kabisa.
Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina chanzo, Hata Ulimwengu na Viumbe vyote havina na havihitaji kuwa na chanzo.

Hili linapingana na akili. Kauli yako hii inajumuishwa na kauli yako ya kwanza na inakuwa hivi, kila kitu kina chanzo isipokuwa MOLA muumba.
 
Nakuuliza swali rahisi sana, nipe sababu tatu ya kwamba aliyefanya ulimwengu ukawepo lazima awe ameumbwa ?

Unakubali Kuna infinity series ? Kwamba ina exist ?
Define existence.

Does it exist from no where? What is infinity? Is it the source of all things?
 
Define existence.

Does it exist from no where? What is infinity? Is it the source of all things?

Ulitakiwa kwanza ujibu swali langu kisha uulize nikujibu. Swali langu naliacha kiporo, uje kulijibu.

Ngoja nijibu maswali yako.

Uwepo ni hali ya kitu kudirikiwa katika hakika yake.

Haiwezekani kuwepo kitu from no where.

Infinity ni kisicho mpaka au mwisho. Hapana sio chanzo Cha kila kitu sababu hiyo ni hali, hali ambayo haimiliki, yaani haidhuru Wala kuathiri.

Usisahau kujibu swali nililo kuuliza.
 
Chanzo cha mawe ni nini? Na mwisho wake ni nini?

Chanzo cha Ardhi ni nini? Na mwisho wake ni nini?

Katika vitu vyenye mwanzo ni mawe na ardhi.

Mawe au jiwe ni katika vilivyo umbwa na Mola. Mwisho wa mawe ni siku ya Kiyama, na mwisho wa ardhi kadhalika
 
Bila shaka kabisa, na anaye umba ni mmoja tu pekee.
Ni kweli mkuu kuna muumba na mm naamini hivoo lakini mada haijataka tujibu kwa dini 🤣🤣 wala sayansi bali tutunie akili zetuu
 
Ulitakiwa kwanza ujibu swali langu kisha uulize nikujibu. Swali langu naliacha kiporo, uje kulijibu.

Ngoja nijibu maswali yako.

Uwepo ni hali ya kitu kudirikiwa katika hakika yake.

Haiwezekani kuwepo kitu from no where.

Infinity ni kisicho mpaka au mwisho. Hapana sio chanzo Cha kila kitu sababu hiyo ni hali, hali ambayo haimiliki, yaani haidhuru Wala kuathiri.

Usisahau kujibu swali nililo kuuliza.
1. Si lazim awe ameumbwa.
Umesema vitu haviji from no where.

So kama ni hivyo chanzo cha uwepo wa tuvionavyo na tusivyo viona ni nini? Material yaliyotumika yalitoka wapi?

Jiwe unaloliona mahala popote liwe dogo au kubwa.. Hakuna binadamu ambaye lisogelea kwa umri. Hewa unayo vuta binadamu kaikuta. Unalijua hilo?
 
Back
Top Bottom