Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini?

Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini?

Binadamu tulikuja duniani kwa kazi maalum ambayo imesha isha, haya tunayo endelea nayo, hata alietuleta hayajui na hana habari nayo, kwa hiyo tunaendelea kufuata ecosystem na evolution time time
 
Binadamu wa kawaida kama mimi na wewe tunawezaje kuwa karibu au kuivuta hiyo super natural power ili iwe part and parcel ya maisha yetu ya kila siku ? At least ningekuwa mwalimu wako ningekup 15%/100% Ahsante sana mkuu
Unataka kunambia you don't feel the super natural power? Hata wewe ni part and parcel katika equilibrium iliyopo ulimwenguni, that's why ukijikwaa unaanguka, ukilewa unayumba. Ukitaka kufahamu vitu vingi unatakiwa uwe skeptical hata katika vitu vidogo
 
Nguvu ya asili isiyo na chanzo inayoratibu ulimwengu
Hiyo nguvu iliishi kwenye nini, kama haina chanzo?

Na hiyo nguvu iliuratibu ulimwengu, ikiwa sehemu gani maana si umesema haikuwa na chanzo?

Na ulimwengu ulikuwa bado haujaratibiwa na hiyo nguvu.

Sasa hiyo nguvu ilikuwa wapi, kabla ya kuratibu ulimwengu?
 
Swali: Ukitoa princliple zote za kisayansi unazozijua na usizojijua na Ukitoa imani zote za Dini zote unazozijua na usizozijua Je, Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini ?

NB; Uzi huu utawekwa kwenye record za Dunia kwamba ndio uzi pekee uliotaja chanzo cha Dunia, Uhai na ulimwengu bila kutaja principle zozote za Kisayansi au Imani (Dini)

Nawasilisha.
Uhai, Dunia, na ulimwengu vyote vilianza kutajwa na (Dini na Sayansi).

Brojust Swali lako halijibiki, vinginevyo Kubali kutumia references za waanzilishi wa hayo majina.
Huwezi kusolve swali la Pythagoras theorem bila kufuata maelekezo na hatua zilizoelekezwa na mwanzilishi wa theory.
 
Newton alitumia rejea. Mgoogle mtu anaitwa Galileo Galilei na uhusiano wake na Newton law of motion. Kwa ufupi Newton hakuumba swali, alitengeneza swali akaja na majibu.

tukiachana na Newton tukarudi kwako brojust wa Tanganyika, Wewe hujaumba wala hujatengeneza swali, umeleta swali ambalo lilishaumbwa tayari katika historia na unataka majibu yasiyohusisha historia na huna nyenzo za kuthibitisha majibu ya kufikirika utakayopewa. Hii kwa lugha fupi unataka blah blah.

Hili ufanyalo ndo blah, blah boss.

Hichi unachofanya ni sawa na wale wa Tandale wanaotengeneza helkopta zao kwa tech ya zamani ambayo dunia ilishaiacha miaka 1000 nyuma huku wakisifiwa mbuyu ulianza kama mchicha.

Karne nyingi zimepita na swali limetolewa majibu mengi tayari mpaka kufikia leo hii, ruhusu rejea kisha zikisolewe na kujadiliwa ndo kunaweza kutokea jibu jipya.
Mkuu nadhani hujanielewa na unataka kunivuta kwenye Imani au Sayansi ndio utaridhika, Basi ngoja niachane na chanzo cha Dunia, nikuulize swali dogo tu nione utakavyo jibu Blah Blah.
Swali; Chanzo cha Jua (Sun) ni nini ? Jibu kwa kutumia rejea za imani yoyote au principle ya sayansi unayoijua.
 
Mkuu nadhani hujanielewa na unataka kunivuta kwenye Imani au Sayansi ndio utaridhika, Basi ngoja niachane na chanzo cha Dunia,
Nakuelewa vizuri tu boss. Unataka tutengeneza ndege wenyewe kwa kuanza moja kama vile ndege haijawahi kutengenezwa before na ukihojiwa kwanini tusiichunguze tech ambayo ipo tayari tukaja na kitu kipya unasema ni blah blah.
nikuulize swali dogo tu nione utakavyo jibu Blah Blah.
Swali; Chanzo cha Jua (Sun) ni nini ? Jibu kwa kutumia rejea za imani yoyote au principle ya sayansi unayoijua.
Chanzo cha jua ni muunganiko wa vumbi kubwa jingi lenye gesi ya hydrogen na hellium ambapo muunganiko wake ukatengeneza joto kali sana katikati na baada ya muda mlipuko wa nuclear ambao ndo tunaita mwanga wa Jua.

NB:
BINGBANG ILIKUJA KWA SWALI KAMA HILI LAKO, YALIPITA MAJIBU MEEEENGI MPAKA KUIFIKIA BINGBANG.
HAKUNA JIBU LA CHANZO CHA ULIMWENGU UTAKALOPEWA NA YEYOTE HUMU AMBALO HALIJAWAHI KUJADILIWA NA WALIOPITA.

KWA KUPUUZA REJEA ZA WALIPOISHIA WENZAKO, UTAPATA REJEA ZA BLAH BLAH AMBAZO ZILISHAJADILIWA SANA TU NA BINADAMU NA KUPUUZWA KWA SABABU HAZINA MASHIKO.
 
Swali: Ukitoa principles zote za kisayansi unazozijua na usizojijua na Ukitoa imani zote za Dini zote unazozijua na usizozijua Je, Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini ?

NB; Uzi huu utawekwa kwenye record za Dunia kwamba ndio uzi pekee uliotaja chanzo cha Dunia, Uhai na ulimwengu bila kutaja principle zozote za Kisayansi au Imani (Dini)

Nawasilisha.
Chanzo cha akili ninini
 
Habari wakuu

Kwanza kabisa niombe shukrani kwa kunipa nafasi ya kujibu swali hili kama ifuatavyo;
1;dunia
Hakuna kitu kinaitwa dunia bali dunia ni ni human mind perception moja kwa moja hakuna chanzo cha dunia wakamua kuita dunia

2;kuhusu uhai niseme kwamba ,hakuna kitu kinaitwa uhai na hakuna uhai bali uhai neno ambalo limeundwa na mwanadamu kutokana na human mind perception yaan mind concious ya mwanadamu ambayo inaamini kuna kitu kinaitwa uhai na kiumbe kisicho hai, wakati kiuhalisia hakuna kiumbe kisicho hai bali concious mind ya mwanadamu imeishia hapo nakuamini kua kuna viumbe hai na visivyo hai kitu ambacho si sahihi

3;ulimwengu kwa kimombo ni universe ni miongoni wa maneno ambayo yaliundwa kutokana na ufahamu wa mwanadamu kuhusu mazingira yanayomzunguka

JIBU.
hakuna kitu kinautwa uhai,dunia na ulimwengu in real world bali ni ni perception of human mind yaani concious mind

💥hakuna dunia ,hakuna uhai,hakuna ulimwengu bali hivyo vyote ni illision tu na propaganda za wanadamu

👉No sources for nothing
Wewe unajibu kama umeulizwa : kwa nn lugha ni sauti za nasibu? Uko nje kabisa ya mada .
 
Swali: Ukitoa principles zote za kisayansi unazozijua na usizojijua na Ukitoa imani zote za Dini zote unazozijua na usizozijua Je, Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini ?

NB; Uzi huu utawekwa kwenye record za Dunia kwamba ndio uzi pekee uliotaja chanzo cha Dunia, Uhai na ulimwengu bila kutaja principle zozote za Kisayansi au Imani (Dini)

Nawasilisha.
Wahi Mirembe
 
Chanzo cha jua ni muunganiko wa vumbi kubwa jingi lenye gesi ya hydrogen na hellium ambapo muunganiko wake ukatengeneza joto kali sana katikati na baada ya muda mlipuko wa nuclear ambao ndo tunaita mwanga wa Jua.
Jibu zuri sana, kwahyo lile vumbi lilitokana na nini ? na Je, Kati ya hizo theories za Bing bang kwa upande wa sayansi na zile za imani, mzani wako wewe unaangukia wapi ? Assume una alama 100% je, Kuhusu chanzo cha dunia, uhai na ulikwengu utazigawaje kwa akili yako binafsi kwamba at least upande huu una ukweli ili tuanze kulijibu swali letu kwa ufasaha.
 
Jibu zuri sana, kwahyo lile vumbi lilitokana na nini ?
Inasemekana kwenye space kuna eneo lina hayo mavumbi yanajulikana kama GMC ambao ni mchanganyiko wa hydrogen na Helium, Ni kama tu kule kijijini kwenu kulivyo na tope au vumbi. Unajua chanzo cha vumbi pale kijijini?
na Je, Kati ya hizo theories za Bing bang kwa upande wa sayansi na zile za imani, mzani wako wewe unaangukia wapi ?
Kwa upande wangu, Mwanzo wa imani ni mwisho wa Sayansi. Naikubali Sayansi ila pale inapokosa majibu sina ninachopoteza ninapogeukia imani, ila za kuambiwa huwa nachanganya na zangu.
Assume una alama 100% je, Kuhusu chanzo cha dunia, uhai na ulikwengu utazigawaje kwa akili yako binafsi kwamba at least upande huu una ukweli ili tuanze kulijibu swali letu kwa ufasaha.
Angalau hapa sasa umeruhusu rejea za sayansi na dini.

Katika 100. Imani siipi chochote sababu imani ni mambo ya kufikirika na mambo ya kufikirika hayana mipaka ya %, katika ulimwengu wa fikra lolote linawezekana hakuna mipaka inayosababisha kushindikana kwa jambo. Mfano, katika ulimwengu wa fikra unaweza kupaa ila ukirudi katika ulimwengu halisi kuna mipaka ya wewe kuruka. Biblia inasema YESU alitembea juu ya maji na watu wanaingia katika fikra na kuamini ila wakirudi katika uhalisia hakuna aliyejaribu kutembea juu ya maji akatembea. Inamaana katika imani YESU ametembea juu ya maji ila katika Sayansi hilo jambo lina mipaka na haliwezekani.

Nikiamini chanzo cha ulimwengu ni MUNGU hakuna mpaka katika hiyo imani mpaka pale sayansi itakapokuja ikasema chanzo cha dunia ni nini na kwa sababu sayansi huja na majibu yenye mipaka tayari itakuondoa kwenye imani.

MKUU, uwepo wa imani unatokana na udhaifu wa sayansi. Binadamu hata yule mjinga kabisa anataka majibu, usipompa atatengeneza ya kwake na ndipo imani inapozaliwa.

Imani/kufikirika na Sayansi/uhalisia havikai chungu kimoja ila sayansi inapofeli ndipo imani huzaliwa.
 
Swali: Ukitoa principles zote za kisayansi unazozijua na usizojijua na Ukitoa imani zote za Dini zote unazozijua na usizozijua Je, Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini ?

NB; Uzi huu utawekwa kwenye record za Dunia kwamba ndio uzi pekee uliotaja chanzo cha Dunia, Uhai na ulimwengu bila kutaja principle zozote za Kisayansi au Imani (Dini)

Nawasilisha.
Hakuna dunia
 
Ni vigezo vipi vitakavyotumika kuhitimisha kuwa majibu yatakayotolewa ni sahihi au la?.
 
Chanzo cha universe ni ajali.
Comet ( Comet, yaani,kama Haley's Comet)inapogongana na Black Hole,a new universe is formed.
Kwa hiyo kama unaiona Comet inakwenda inaelekea ku collide with a Black Hole,basi we will soon have a new universe.
Kuhusu sayari zinavyotengenezwa, a star will spit out fire,the fire cools down, solidifies,and that is your new planet .
Kuhusu watu wanatoka wapi,well,
Civilizations nyingine ni very advanced.
Wanafanya exploration here and there.
Wakiona a sun somewhere, spitting out fire, creating planets wanasema,"Hey, what have we got here? Planets being formed?"
Basi,wanasubirisubiri planet ipoe.
Planet inapoa,halafu you have a planet,winds are raging,volcanoes, earthquakes,and what have you.
Wanangoja ipoe zaidi.
Halafu ikishapoa kiasi cha kutosha they go there and land.
Wanachukua soil samples,water samples,Hawa wametua,wenzao wako juu katika mothership.
Wanachukua samples,wanarudi nazo kwenye mothership,wanazichunguza zile samples,halafu craft nyingine zinatumwa kwenye hiyo sayari kuangusha packages here and there kuharakisha normalization of the planet.
Wanarudi kwao,wanasubiri.
Halafu planet inakuwa ready for for habitation.
Planet ya namna hii iliyotokana na nova, lazima iwekwe dinassaur type animals na special trees.
Hawa wanyama ndio wanaitayarisha planet for human habitation.
Mizoga yao na excreta yao ndicho tunachoita "ardhi".
Watu wanaletwa.
Wanatoka wapi hao watu?
Ile ni advanced civilization tumesema. Hawa watu wanatengenezwa katika maabara zao.
Wanaletwa katika planet,and they are always savages.
A new civilization begins.
The average length of a civilization is 12,,000 years,Toka pale wanapokuwa savages mpaka pale wanapoanza kutishia kuilipua sayari with nuclear weapons.
Unfortunately,it is not always threats,mara nyingi wanailipua Dunia,na Civilization inaanza upya.
 
Back
Top Bottom