Kama hujui mpangiliaji na yeye kapangiliwa au la, Sasa ulijuaje yupo?
Au unafosi tu kwamba kuna mpangiliaji, ilhali hata hujui huyo mpangiliaji mwenyewe katoka wapi?🤷
Kwani lazima mpangilio uliopo uwe umepangiliwa?
Kwa nini unadhani mpangilio uliopo, lazima uwe umepangiliwa?
Kwa nini hudhani kwamba, mpangilio uliopo umejipangilia wenyewe tu?
Kama mpangilio huu uliopo lazima uwe umepangiliwa, Hata huyo mpangiliaji mwenyewe lazima awe amepangiliwa.
Mpangiliaji huyo hawezi kuwepo tu from no where.
Na kama si lazima kwamba mpangilio uliopo umepangiliwa, Basi pia hakuna haja ya kuwepo mpangiliaji wa mpangilio huu uliopo.
Kwani lazima viumbe hai wote viwe na mwanzo?
Kama ulazima huo upo, Hata huo mwanzo wa viumbe hai wote, Lazima uwe na mwanzo wake mwingine. Hivyo hivyo to infinity
Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo mwanzo maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo tu chenyewe, pasipo mwanzo.
Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mwanzo, Hata viumbe hai wote hatuna na hatuhitaji tuwe na mwanzo.
Je huyo mtengenezaji wa mikate, yeye alitengenezwa na nani?
Na huyo aliye mtengeza, alitengenezwa na nani?
Unapoweka ulazima wa kwamba lazima awepo mtengenezaji, Je huoni kwamba hapa kutakuwa na watengenezaji endless, wasio na mwisho?