Chanzo cha Dunia, Uhai na Ulimwengu ni nini?

Boss, hilo swali lina umri mkubwa sana kukushinda. Limekuwepo karne na karne. Hapa unachofanya ni kupokea majibu yaleyale yaliyokwishatolewa na waliozaliwa na kuishi miaka mingi nyuma kabla wewe hujazaliwa.
Je, unakubali hakuna jibu ? na kwa vizazi vyote vilivyopita na vijavyo hakutatokea jibu ? Nini majibu yako sasa ?
 
Unathibitishaje kwamba dunia na maisha yalisukwa kwa mipangilio?

Je dunia na maisha haviwezi kujipangilia vyenyewe tu?

Kwa nini unadhani dunia na maisha vilipangiliwa?

Kwa nini Hudhani dunia na maisha havija pangiliwa?

Kama dunia na maisha lazima viwe vimepangiliwa, Je huyo mpangiliaji wa dunia na maisha, Yeye alipangiliwa na nani?
Kwanza mikate🍞haina uwezo wa kutambua kitu.

Mikate si kiumbe hai chenye fikra na ufahamu.

Kufananisha mkate 🍞 usio na ufahamu wowote ule na binadamu mwenye ufahamu ni kufanya, Logical non sequitur.

Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule, kuunda hitimisho potofu.

Ulijuaje dunia ina mwanzo na unathibitishaje kwamba dunia na binadamu tuna mwanzo?
 
Je atakayesahihisha ile jibu na kupata mshindi, atatumia reference ipi?
 
Unathibitishaje kwamba dunia na maisha yalisukwa kwa mipangilio?
Angalia maisha ya binadamu na viumbe wengine, angalia kila hatua,,,, alafu kwa kutumia akili yako Fikia hitimisho, kwamba yalitokea kwa bahati mbaya au yamepangiliwa, sababu Mtoa Mada amekataza tusitumie principles, sayansi au Dini,,, kinachobaki ni reasoning ,,, ambayo ni self reasoning( akili).
 
Je, unakubali hakuna jibu ? na kwa vizazi vyote vilivyopita na vijavyo hakutatokea jibu ? Nini majibu yako sasa ?

Umesema tutoe majibu bila rejea ya popote si dini wala sayansi. Kwa ufupi umesema jibu liumbwe na akili na si kutengenezwa kutoka majibu ambayo tayari yapo katika historia.

Nikuulize, unaweza kusema wewe ni nani bila rejea yoyote? Embu tuambie, wewe ni nani? Jibu bila kuwahusisha wazazi wako wala binadamu wengine waliosema wewe ni binadamu. Tuambie wewe ni nani?

Kama una jibu basi hata swali ulilouliza lina jibu, kama huna basi hakuna jibu bila kuchimba rejea.
 
Swali : Nini chanzo cha binadamu , yeye anakuambia ''hamna chanzo''. Huoni kama ni akili mbaya.
Kwani jibu lazima litoe chanzo cha binadamu?

Je kama chanzo hakipo?

Si unasema hakipo.

Kwani lazima chanzo kiwepo?

Kama kipo ndio unajibu kipo, kama hakipo unajibu hakipo.

Ili anayesema kipo, Athibitishe uwepo wa hicho chanzo kilichopo.

Sasa wewe unataka niseme chanzo kipo wakati hakipo, Na wewe mwenyewe umeshindwa kujibu na kuthibitisha hicho chanzo unachodai kipo.
 
“Chanzo cha dunia, uhai na ulimwengu ni nini?"

Chanzo huwa na ukomo (mwisho)
Uhai mwisho wake ni kifo. Vipi kuhusu dunia na ulimwengu mwisho wake ni nini?

Je ni lazima kila kitu kiwe na chanzo na mwisho? Kama ndivyo hata hicho chanzo unachokitafuta utahitaji kutafuta tena chanzo chake, tena na tena. Yani utatafuta sana chanzo cha chanzo cha chanzo .....
 
Chanzo kipo ndio maana wewe upo hapo , tatizo husemi unataka kubishana ukiambiwa ...Ishu iko wazi chanzo cha mwanadamu kipo mpaka wakaendeleza vizazi wakawa wengi .

kila siku idadi ya watu inaongezeka .
 
Mbona hujiulizi, Huyo aliye yapangilia maisha ya binadamu na viumbe wengine, Yeye pia alipangiliwa na nani?

Mbona una Exclude hicho kilicho pangilia maisha ya binadamu na viumbe wengine, kwenye kupangiliwa?

Kama hicho kilicho pangilia maisha ya binadamu na viumbe wengine hakihitaji mpangiliaji, Hata Maisha ya binadamu na viumbe wengine wote, Hayahitaji mpangiliaji.
 
wewe unakijua? Na je kama unajua basi mtu huyo mwenye akili ni wewe na kama haujui je utathibitishaje kama jibu lililotolewa ni sahihi?
Jibu swali, nenda kwenye mada, toa majibu bila Imani au sayansi. Acha blah blah.
 
Chanzo kipo ndio maana wewe upo hapo , tatizo husemi unataka kubishana ukiambiwa ...Ishu iko wazi chanzo cha mwanadamu kipo mpaka wakaendeleza vizazi wakawa wengi .

kila siku idadi ya watu inaongezeka .
Hicho chanzo, chanzo chake ni nini?

Hicho chanzo, kabla hakijawa chanzo, kilikuwa wapi?

Huko kilipokuwa, kulitoka wapi?

Na chanzo chake ni nini?
 
Literally kasema usitumie reference ya kidini au ya kisayansi we una ctrl P + V
 
Mbona hujiulizi, Huyo aliye yapangilia maisha ya binadamu na viumbe wengine, Yeye pia alipangiliwa na nani?
mpamgiliajiii yupo na sijui Kama na yeye kapangiliwa pia au la, kwa maana hata Nikijua Hilo halibadirishi huuu mpangilio uliopo…..

Uliukataaa mfano wAngu wa mikate,,, ukasema si kiumbe hai,,, ni kweli. Ila ndio mfano rahisi zaidiiii maana nikiweka kiumbe hai katika maelezo yangu ntakuwa najichanganya maana Hapa tunajadiri Mwanzo wa viumbe wote hai,,,,

So ntarejerea kwenye huo mfano,,,,, mikate hata ikijuaaa kwamba muoka mikate aliokwa ( alitokana) pia na nguvu Fulani,,, bado haibadirishi ukweliiii kwamba mikate yote inetengenezwa na yeye.
 
Jibu swali, nenda kwenye mada, toa majibu bila Imani au sayansi. Acha blah blah.
Mkuu, kwa kusema rejea yoyote isitumike swali lako umelifanya kuwa ni la kujibiwa kwa kufikirika, na kufikirika mara nyingi lazima blah blah zitokee, majibu lazima utayapokea ya blah blah. Vumilia majibu yote utakayopewa.
 
Hicho chanzo, chanzo chake ni nini?

Hicho chanzo, kabla hakijawa chanzo, kilikuwa wapi?

Huko kilipokuwa, kulitoka wapi?

Na chanzo chake ni nini?
Tulia usome acha ubishi 😀 😀 😀 mpaka watu kufika bilion 8 basi kulikuwana chanzo mpaka idadi ikafika hapa.
 
Mkuu, kwa kusema rejea yoyote isitumike swali lako umelifanya kuwa ni la kujibiwa kwa kufikirika, na kufikirika mara nyingi lazima blah blah zitokee, majibu lazima utayapokea ya blah blah. Vumilia majibu yote utakayopewa.
Kama nitakosea naomba kusahihishwa. Bwana Newton kwenye ile third law of motion alisema "In every action there is equal and opposite reaction" Je alifanya rejea wapi ?

Swali la msingi ? Tumia akili yako kujibu na kuja na jibu ambalo sio la kumezeshwa kwenye Dini au sayansi. Ndio maana nimesema Acha blablah jibu swali kwa kutumia akili yako, Njoo na principle yako iishi miaka Mia mbele.
 
Hapo inatakiwa kujibiwa na wasio na dini
 
mpamgiliajiii yupo na sijui Kama na yeye kapangiliwa pia au la,
Kama hujui mpangiliaji na yeye kapangiliwa au la, Sasa ulijuaje yupo?

Au unafosi tu kwamba kuna mpangiliaji, ilhali hata hujui huyo mpangiliaji mwenyewe katoka wapi?🤷
kwa maana hata Nikijua Hilo halibadirishi huuu mpangilio uliopo…..
Kwani lazima mpangilio uliopo uwe umepangiliwa?

Kwa nini unadhani mpangilio uliopo, lazima uwe umepangiliwa?

Kwa nini hudhani kwamba, mpangilio uliopo umejipangilia wenyewe tu?

Kama mpangilio huu uliopo lazima uwe umepangiliwa, Hata huyo mpangiliaji mwenyewe lazima awe amepangiliwa.

Mpangiliaji huyo hawezi kuwepo tu from no where.

Na kama si lazima kwamba mpangilio uliopo umepangiliwa, Basi pia hakuna haja ya kuwepo mpangiliaji wa mpangilio huu uliopo.
Uliukataaa mfano wAngu wa mikate,,, ukasema si kiumbe hai,,, ni kweli. Ila ndio mfano rahisi zaidiiii maana nikiweka kiumbe hai katika maelezo yangu ntakuwa najichanganya maana Hapa tunajadiri Mwanzo wa viumbe wote hai,,,,
Kwani lazima viumbe hai wote viwe na mwanzo?

Kama ulazima huo upo, Hata huo mwanzo wa viumbe hai wote, Lazima uwe na mwanzo wake mwingine. Hivyo hivyo to infinity

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo mwanzo maana kitazua maswali ya kiliwezaje kuwepo tu chenyewe, pasipo mwanzo.

Na kama si lazima kwamba kila kitu kilichopo kina mwanzo, Hata viumbe hai wote hatuna na hatuhitaji tuwe na mwanzo.
So ntarejerea kwenye huo mfano,,,,, mikate hata ikijuaaa kwamba muoka mikate aliokwa ( alitokana) pia na nguvu Fulani,,, bado haibadirishi ukweliiii kwamba mikate yote inetengenezwa na yeye.
Je huyo mtengenezaji wa mikate, yeye alitengenezwa na nani?

Na huyo aliye mtengeza, alitengenezwa na nani?

Unapoweka ulazima wa kwamba lazima awepo mtengenezaji, Je huoni kwamba kutakuwa na watengenezaji endless, wasio na mwisho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…