Chanzo cha kuchokana, kununiana katika mahusiano/ndoa na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili

Chanzo cha kuchokana, kununiana katika mahusiano/ndoa na jinsi ya kukabiliana na tatizo hili

Wandugu maisha ya mke na mume ni maelewano kati ya wawili, so inapaswa kuridhiana na kuheshimiana kuna wakati kuna kuwa na tofauti/ugomvi hilo haliepukiki maana mmetoka kwenye background tofauti la muhimu ni kuongea kwa busara (si kwa hasira) na kuombana msamaha ikibidi. Kisha mnamalizia na SEX kupunguza JOTO HASIRA
 
kama ni kupiga mwanamke utapiga mara ngapi? maana wao kila siku ni watu wa maneno, mi nafikiri dawa ni kunyamza kimya (usimjibu) uendelee na yako. akiwa sawa atajirudi tu
 
Nina rafiki yangu hawaongei na mumewe for 5 yrs. tatizo kubwa sijalijua maana nimesikia utetezi wa mke, mume hajanieleza ya kwake. Wanalala vyumba tofauti, kila mmoja anapika chakula chake, wana watoto wakubwa wanaofanya kazi. Tatizo watoto ni mabwetere fulani, waliolelewa maisha fake ya kusoma IST halafu pesa ya baba ikakata, hivyo nahisi wanaona maisha ya wazazi yako sawa.
Ni maisha ya ajabu ambayo mimi binafsi siyawezi, ningeshaondoka siku nyingi, lakini wao wapo tu wanapigana vikumbo humu ndani, hakuna anayemsemesha mwenzie.
Ni kama muvi, lakini ndio maisha.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Speechless aisee..! Mnaishije ndani ya nyumba huku mmenuniana miezi mitano? Mungu epushia mbali kabisa..!
 
Miezi mitano?Aiseee ni mingi sana jaribu kuongea hata na viongozi wenu wa dini au wazazi mtatue yanayowasibu ili muendeleze familia yenu maana mmeishakaa mda mrefu[/QUOTE]

Viongozi wa dini na wenyewe wana matatizo yao, ila yamefunikwa na kivuli cha dini, so sidhani kma ni dawa. Dawa mnayo ninyi wenyewe. Miaka 13 ni mingi sn. Jiulize vizur nini kimetokea. Wewe unaongea hivyo hapa kwa kuwa una access na JF, tukakuonea huruma sana. Lakini yawezekana na yeye angekuwa yupo JF, angeweza kusema MKE WANGU KANINUNIA MIEZI 5. Sisi wote hatujui the inner source ya magomvi yenu, ila ninyi wenyewe mnajua sana tu. Tumia mbinu zako za kike kumleta mshikaji kwenye reli mkayaongea. Yawezekana style yako ya kujishusha ni ile ya kusema "BASI TUFANYE MI NDO NIMEKOSA". Kma hivyo ndivyo, sio rahisi kukubali msamaha wko. Ni hayo tu.


Sent from my iPad using JamiiForums app
 
Ukimuona mtu anasherehekea miaka kadhaa ya ndoa msalimie shikamoo
 
daah leo nimepata mengi sana hapa, niwashukuruni sana wote mulochangia mada hii kwa busara za hali yajuu sana ukiachilia wachache mloleta maneno mbofumbofu! bado nipo naendelea fuatilia uzi huu elimishi kwangu kweli nimejifunza!!!
leo hii namimi ni mhanga kwa hili yaani tangu j2 ilopita had leo j2 hali ni tete mtu amenuna n'a chakula hakupikwi basi mm nimejitahid kua kimya coz kila nikibembeleza moto unazidi, nikitoka kazni hua nakula njian nikifika naoga nalala zangu, leo hapa nimelala nasoma jf lakin mwenzangu yupo sebulen analia sababu bado sijajua cjui ni ukimya wangu au laah!

tutaendelea kufahamishana wajamani ndoa. ndoano
 
Wajameni (hususani wanandoa) ni kitu cha kawaida wengi kukuta watu wamenuniana hatari yaani hawasemezan hata mwezi mzima, unakuta kuna ugomvi kati yao kwa ishu ndogo tu hasa wivu, kulea watoto, kazi,ndugu na kubamba sms/email za mchepuko.

Binafsi nimesha experiece minuno kadhaa unakuta wife amefanya kosa Fulani unaamuliza kistaarabu lakini atakavyo-react balaa hakubali kama alikosea bali hutafuta KUJITETEA kwa kumbushia makosa yangu ya zamani tukiwa wachumba.

Hapo mimi huwa kimyaaa ili niepushe hasira za kumshushia MAKONDE.

Basi unafuata MNUNO hata wiki 3. Hebu tujuzane ikitokea umekutana na mnuno kwa mwenzi wako dawa ni nini?


acha utani wewe,kubamba sms au email ni kitu kidogo? maadili yako yanatia wasi
 
Wajameni (hususani wanandoa) ni kitu cha kawaida wengi kukuta watu wamenuniana hatari yaani hawasemezan hata mwezi mzima, unakuta kuna ugomvi kati yao kwa ishu ndogo tu hasa wivu, kulea watoto, kazi,ndugu na kubamba sms/email za mchepuko.

Binafsi nimesha experiece minuno kadhaa unakuta wife amefanya kosa Fulani unaamuliza kistaarabu lakini atakavyo-react balaa hakubali kama alikosea bali hutafuta KUJITETEA kwa kumbushia makosa yangu ya zamani tukiwa wachumba.

Hapo mimi huwa kimyaaa ili niepushe hasira za kumshushia MAKONDE.

Basi unafuata MNUNO hata wiki 3. Hebu tujuzane ikitokea umekutana na mnuno kwa mwenzi wako dawa ni nini?


Hivi kubamba sms/e-mail ya mchepuko ni jambo dogo kwako.
Siku ukibamba sms ya mchepuko kwenye simu ya mkeo utachukulia poa tu na utakenua meno yako tu.
Tatizo mnataka ndoa wakati uaminifu hamna,ndoa zina maadili na miiko yake usipoifuata lazima ikushinde.
Usichukulie ndoa kama hatua/utaratibu katika maisha tu bali lazima ufahamu kuna majukumu,wajibu na mipaka ya kuifuata unapoingia kwenye ndoa.Sasa unaingia kwenye ndoa wakati kuchepuka kwako unaona jambo la kawaida aisee hii ni hasara kabisa.
Mnataka ndoa wakati hata maana,wajibu na mipaka ya ndoa hauijui ndo maana wengi zinawashinda mnabaki kuja kutusumbua tu huku Jf.
 
Na ww nuna harafu panua mapaja yake taratibu bila kumsemesha then zama kati.......................,,,,
 
Mimi sitakupiga kwa mikono na miguu ntakupiga kwa vitendo tuu mpaka utaomba upewe kipigo mwenyeweee,ukipika chakula sili,kugegedana sahau,nyumbani sirudi hata siku mbili mfululizo,simu yako sipokei msg sizijibu,story ndo staki kabisaaaa,chumba tutalala tofauti,kama mwanamke ana akili timamu atachunguzaa yooote yanayonikera na hatayafanya coz anajua akifanya reaction itakuwaje,kama mcharuko basi ataendelea kuzingua na kwa sababu hatujazaliwa tukiwa wawili kila mtu itabidi ashike lake!

makubwa!
 
Kwa staili hii ya wanandoa michepuko haitaisha. TACAIDS na MSD waongeze tu ARV maana zitahitajika sana 2015
 
Kila binadamu ana mapungufu yake, basi inapotokea kwa wanandoa kutozungumza kukaa kimya kwa jambo lolote hamna story, hamna salamu na mnalala kitanda kimoja. Je, kwa kawaida hali hii inabidi kwenda kwa muda gani? Wiki moja, mbili au mwezi au miezi?

 
Duuh hebu yazungumze yaishe....hii kitu kama bahati mbaya ikitokea ni muda wa siku zisizidi 3. Zaidi ya hapo mnapalilia mambo mengi, ambayo yataenda kuvunja ndoa yenu.
 
Back
Top Bottom