Chanzo cha kushuka thamani kwa pesa ya South Africa, Rand kwa cent zaidi ya 30 dhidi ya USD$

Zulu Man Tz

Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
73
Reaction score
99
Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Reuben Brigety alisema siku ya Alhamisi Tarehe 11 May 2023 kuwa ana uhakika kwamba meli ya Urusi chini ya vikwazo vya Marekani ilichukua silaha kutoka kambi ya Simon's Town mwezi Disemba, akipendekeza uhamisho huo hauendani na msimamo wa Pretoria wa kutoegemea upande wowote katika vita vya Russia dhidi ya Ukraine.

Kauli ya balozi ikaathiri masoko ya kifedha
Dola ilipanda sana hadi randi 19.5150 Ijumaa asubuhi-kiwango chake cha juu zaidi dhidi ya sarafu ya Afrika Kusini kwenye rekodi-lakini baadaye iliteleza na kushuka hadi kwa randi 19.33.

2018-07-26T181424Z_125667727_UP1EE7Q1EO0O2_RTRMADP_3_SAFRICA-BRICS-1682428062.jpg

Maafisa wa Afrika Kusini wamejibu shutuma za Marekani kwamba meli ya Urusi ilikusanya silaha kutoka kambi ya wanamaji karibu na Cape Town mwishoni mwa mwaka jana.

Balozi wa Marekani mjini Pretoria aliitwa baada ya kusema ana uhakika kwamba meli ya Urusi ilikuwa imekusanya silaha kutoka Afrika Kusini.

Licha ya USA-Washington imeonya kwamba nchi zinazotoa msaada wa nyenzo kwa Urusi zinaweza kunyimwa ufikiaji wa masoko ya Amerika. Balozi huyo hakuwa na uhakika na ikamladhimu aombe radhi kwa Serikali ya Afrika ya Kusini siku ya ijumaa asbuhi.

Mawazo Binafsi
Bado dollar ya Marekani iko na nguvu kwny Uchumi wa Dunia na inaweza kusababisha economic sanctions kwa Nchi nyingine ila bado tuko na mbadala wa Nchi za BRICS kuanzisha Sarafu ya pamoja ambayo mpaka sasa Nchi zaidi ya 30 imekubaliana na mpango huo.

Ambazo ni Afghanistan, Algeria, Argentina, Bahrain, Bangladesh, Belarus, Egypt, Indonesia, Iran, Kazakhstan, Mexico, Nicaragua, Nigeria, Pakistan, Saudi Arabia, Senegal, Sudan, Syria, the United Arab Emirates, Thailand, Tunisia, Turkey, Uruguay, Venezuela, and Zimbabwe.

Je, utulivu utapatikana kwa Nchi wanachama wa BRICS maana wao kati ya wao wako na migogoro ili wafikie malengo yao ya pamoja kiuchumi dhidi ya Marekani?
 
South Africa wanapelekeshwa na huyo dikteta, sasa kama anawapenda basi awape huo umeme wa uhakika ulaya na Marekani ndio kwenye hela dunia hii na ndiko kwenye uchumi na bidhaa kujipeleka Brics ni kujitafutia majanga China na Russia hawana uhakika wa hata uchumi wao baada ya Vikwazo vya US, Yuan haiwezi kuwa ndio hela inayotaradad masokoni ukiacha dola na Euro
 
Hayo mambo ya De-dollarization ni kujidanganya tu hamna lolote.

Wakopeshaji wakubwa bado ni Marekani na washirika wake pamoja na mashirika ya kifedha walizounda wenyewe na sarafu wanazotumia ni hizo hizo ambazo hao Brics wanajaribu kukwepa na ukishakopeshwa utalipa tena kwa sarafu hizo hizo na wala hamna cha Brics wala cha nini.
 
Let us see mambo yatakavyoenda
 
Ndio maana the late Mwlm Nyerere aliyakata haya ya structure adjustment program (SAP) mikopo ya IMF na WB bado changamoto maana waendeshaji na wenye control ni USA
 
Tukusema Marekani ndiyo chanzo Cha machafuko karibu Kila kona ya Dunia muwe mnalelewa. Yani anakuchagulia marafiki, maadui, mfumo wa maisha, na anaamua uishi kwa muda gani hapa Duniani. Hovyo kabisa, poleni familia ya Sadam Husein, Gadafi, na hongera familia ya Osama bin Laden maana baba yenu aliukataa utumwa wa Marekani, bila kusahau familia ya Mugabe aliekataa kuwa kibaraka wa Marekani
 
URUSI kupitia USSR wamelisaidia Sana bara la Afrika kujikomboa kutoka katika ukoloni wa western countries. Ila sisi waafrika mhhhhhh
Na viongozi nguli wa Afrika walikuwa wamelalia kwny sera za Urusi waliuwawa Haile Selassie, Muamar Ghadaffi, Patrick Lumumba, Kwame Nkrumah Marekani wanawachagulia waafrika watu wakushirikiana nao daaah 💔
 
Tukusema Marekani ndiyo chanzo Cha machafuko karibu Kila kona ya Dunia muwe mnalelewa. Yani anakuchagulia marafiki, maadui, mfumo wa maisha, na anaamua uishi kwa muda gani hapa Duniani. Hovyo kabisa, poleni familia ya Sadam Husein, Gadafi, na hongera familia ya Osama bin Laden maana baba yenu aliukataa utumwa wa Marekani, bila kusahau familia ya Mugabe aliekataa kuwa kibaraka wa Marekani
Tukupe maua yako mkuu🙏
 
Urusi au USSR hawajalisaidia bara la Africa, walisaidia nchi chache za Africa kwa maslahi yao ya vita baridi. Mfano hakuna msaada nchi za Africa Mashariki au Magharibi ziliupata kutoka USSR katika kutafuta uhuru wao kwa sababu kwanza nyingi ya hizi nchi baada ya WWII zilikuwa protectorates tu zilizokuwa zinaandaliwa kupata uhuru.
URUSI kupitia USSR wamelisaidia Sana bara la Afrika kujikomboa kutoka katika ukoloni wa western countries. Ila sisi waafrika mhhhhhh
 
Urusi au USSR hawajalisaidia bara la Africa, walisaidia nchi chache za Africa kwa maslahi yao ya vita baridi. Mfano hakuna msaada nchi za Africa Mashariki au Magharibi ziliupata kutoka USSR katika kutafuta uhuru wao kwa sababu kwanza nyingi ya hizi nchi baada ya WWII zilikuwa protectorates tu zilizokuwa zinaandaliwa kupata uhuru.
Ebu tufafanulie apo Mkuu kwa manufaa yao ya cold War kivipi maana Urusi kama Urusi haijwahi kumkoloni Mwafrika katika kuongeza thamani ya Nchi yake kama ilivyo Uingereza
 
South Africa wanapelekeshwa na huyo dikteta, sasa kama anawapenda basi awape huo umeme wa uhakika ulaya na Marekani ndio kwenye hela dunia hii na ndiko kwenye uchumi na bidhaa kujipeleka Brics ni kujitafutia majanga China na Russia hawana uhakika wa hata uchumi wao baada ya Vikwazo vya US, Yuan haiwezi kuwa ndio hela inayotaradad masokoni ukiacha dola na Euro
Kama Marekani anavyowapelekesha nyie NATO na EU kwa ujumla....
 
Ndio maana the late Mwlm Nyerere aliyakata haya ya structure adjustment program (SAP) mikopo ya IMF na WB bado changamoto maana waendeshaji na wenye control ni USA
Kwa hiyo utafanyaje sasa kama Nyerere mwenyewe ndio huyo alishindwa hadi akaamua kuachia ngazi ili mwingine ndio aje ayakubali hayo masharti na ndicho kinachofanyika na leo ndio tuko hoi zaidi na hatuna ujanja.
 
URUSI kupitia USSR wamelisaidia Sana bara la Afrika kujikomboa kutoka katika ukoloni wa western countries. Ila sisi waafrika mhhhhhh
Hivi tumepata faida gani kuondokana na ukoloni wa mtu mweupe na kuingiza ukoloni wa mtu mweusi. Eti rasilmali zetu ambazo zingetusaidia kujiletea maendeleo ndizo tena tunapora wenyewe na zingine tunapeleka kuficha tena hukohuko kwa hao wakoloni weupe, rejea issue ya akina Chenge.

Kila mwaka ripoti ya CAG inaonyesha kwamba hatukustahili kabisa kudai huo mnaoita uhuru kwa sababu lengo la kudai uhuru ilikuwa ni sasa kupigania maslahi ya nchi ili wote wafurahie matunda ya uhuru lakini kilichopo ni kinyume chake kabisa halafu eti bado tu tunatafuta visingizio. Bure kabisa.
 
Kwa hiyo utafanyaje sasa kama Nyerere mwenyewe ndio huyo alishindwa hadi akaamua kuachia ngazi ili mwingine ndio aje ayakubali hayo masharti na ndicho kinachofanyika na leo ndio tuko hoi zaidi na hatuna ujanja.
Umenikumbusha mzee wa ruksa haha
 
Back
Top Bottom