Hivi tumepata faida gani kuondokana na ukoloni wa mtu mweupe na kuingiza ukoloni wa mtu mweusi. Eti rasilmali zetu ambazo zingetusaidia kujiletea maendeleo ndizo tena tunapora wenyewe na zingine tunapeleka kuficha tena hukohuko kwa hao wakoloni weupe, rejea issue ya akina Chenge.
Kila mwaka ripoti ya CAG inaonyesha kwamba hatukustahili kabisa kudai huo mnaoita uhuru kwa sababu lengo la kudai uhuru ilikuwa ni sasa kupigania maslahi ya nchi ili wote wafurahie matunda ya uhuru lakini kilichopo ni kinyume chake kabisa halafu eti bado tu tunatafuta visingizio. Bure kabisa.