Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Katibu Mkuu kiongozi ameteuliwa na Rais ambaye ndio anayechochea siasa za kishamba za kutandika fimbo raia kinyume cha sheria .Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?
Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Kwa mfano , Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa hadharani alimpongeza na kumsifia RC wa Mbeya ndugu Chalamila kwa kuwatwanga fimbo wanafunzi waliotuhumiwa kuchoma mabweni , adhabu hii ilikuwa ni kinyume cha sheria za nchi , sasa haya yote Katibu Mkuu kiongozi anayajua , anafahamu kuwa mkuu wake anaunga mkono mambo haya , anawezaje kutoa kauli tofauti ?
Halafu ukiangalia kwa makini body language ya Bashiru kwenye jambo hili utajua tu kwamba anazuga ili kuwapumbaza wajinga , wala hamaanishi anachokisema .