Katibu mkuu( General Secretary) wa chama cha mapinduzi CCM, yeye ndie msimamizi mkuu wa ilani ya CCM( Chama tawala), ilani inayotumika kutoa muongozo wa utekelezaji wa shughuli za serikali kwa miaka mitano ijayo( 2020-2025)
Watendaji wote wa serikali kwa sasa wanatekeleza majukumu yao kutokana na muongozo wa ilani ya CCM( 2020-2025)
Endapo ilani hiyo itafeli au kushindwa kutekelezwa ipasavyo, mtu wa kwanza kuulizwa na kuwajibika kwa kufeli huko, ni latibu mkuu wa CCM, kwa nafasi yake kama msimamizi mkuu wa ilani hiyo
Kwa hiyo katibu mkuu wa CCM anayo haki ya kutoa onyo kwa mtendaji yeyote wa serikali, ikiwa anaona mtendaji huyo ni kikwazo kwenye kutekeleza ilani ya chama chake( chama tawala kwa wakati huo)
Isipokuwa sasa, katibu mkuu wa CCM hana mamlaka ya kisheria ya kumuadhibu mtendaji yeyote wa serikali, Watendaji wa serikali wanaadhibiwa na mamlaka yao ya nidhamu