Chapa Chapa: Katibu Mkuu Kiongozi yuko wapi?

Kuna post ambayo tulijadili sana jambo hili lakini hebu fikiria "Uchapwe viboko au ukafunguliwe kesi isiyokuwa na dhamana na hata kama ina dhamana bado ule danadana na kuozea jela?"
Hata mie ningekubali nichapwe tu kwa ajili ya familia yangu na wanaonitegemea.
Bob Bora kufa umesimama.. Nadhani Familia yako ingekuwa imara Zaid.. na ingekuheshimu
 
Nasikitika Mwanakijiji kuhamisha gori hata kwa jambo hili! mkuu wa mkoa aliwapiga wanafunzi tena kwa nguvu zote! tz ilisimama ikisubilia kauli ya mteule wake! unakumbuka kilichotokea!

JPM mwenyewe kwa mdomo wake akapongeza na kuongeza kauli waendelee kupigwa! baada ya hapo kila mmoja anainua mkono kupiga! et leo unamtupia lawama katibu kiongozi kweli?

Naibu waziri ni mteule wa Rais mamlaka ya kumwadhibu ni anayesifia viboko! usimpende mtu bila kuyachukia mabaya yake! huu mtindo mbovu ni wa JPM hebu mbebeshe yeye

Hakuna mtu mnafiki kama mkjj hapa JF , ni yeye aliepiga debe Sana kutetea watu ambao ndio Sasa wanaleta upumbafu huu
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Katibu Mkuu CCM zaidi ya Waziri Mkuu hivyo Katibu Mkuu Kiongozi ni kama PS wa Katibu Mkuu CCM
 
Tatizo kubwa wote wanaotakiwa kulikemea hilo hawajui msimamo wa MZEE BABA!!unaweza kulikemea kesho akaibuka na kuwapongeza hao wanaowachapa!!utajisikiaje?!!ila ngoja iabuke na kulikemea utawaona sasa viongozi wote ndio wanajifanya kulikemea!!!utumwa wa fikra ni mbaya sana!!
Hata huyo alieanzisha huu uzi ni kwa sababu Bashiru amekemea,ushamuona amekemea huu utawaka?
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Yule ni kamisaaa wa rais na ndio mpangaji wa uteuzi kazi yake sio kujionyesha
 
Narudia tena,kama huu uchaguzi ungekuwa na dosari na watanzania hawajaridhika kila mtu angeandamana.

Waganda hawakuridhika na Amin ndio maana walichukua siraha na kumg'oa. Usichanganye mada boss/ kamanda.

Watanzania hawana ujasiri wa kuandamana mahali ambapo polisi/ vyombo vya dola vimeagizwa viwaue. Ni watanzania wachache sana wenye uthubutu huo. Tuliona maandamano ya uchaguzi mdogo hapa Dar kwenye jimbo la Mtulia binti mdogo Aqwilina alipouawawa, viongozi wa cdm wote wakapewa kesi, na watu kibao kuachwa na vilema huku wakibambikiwa kesi. Usichanganye uoga na kutokuridhika. Kama ni kutokuridhika kuko wazi, ujasiri wa kuandamana kwa kutokuridhika ni suala jingine.

Iddi Amin alitolewa na jeshi la Tanzania, wananchi wa Uganda waliwaunga mkono jeshi la Tanzania kama sehemu ya kuchoka kunyanyaswa na kuuwawa. Hata hapa ikitokea nchi ikatuvamia, utakuja kuchukua mrejesho wa jinsi watu hawaridhiki na utawala wa shuruti wa ccm. Rejea kombe la Afrika timu yetu ilivyoenda Egypt, jinsi watu walikuwa wanashangilia tunavyofungwa.
 
Katibu Mkuu CCM zaidi ya Waziri Mkuu hivyo Katibu Mkuu Kiongozi ni kama PS wa Katibu Mkuu CCM

Hivi wewe unamjua katibu mkuu kiongozi ( Chief Secretary) ni nani?

Nenda kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 60 , utajua katibu mkuu kiongozi ni nani
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Kama hata mwanasheria mkuu wa serikali ana shindwa kutolea ufafanuzi wa kisheria kuhusu huu ujinga una tegemea Katibu Mkuu kiongozi atapata wapi la kuongea wakati mshauri wao kisheria yuko kimya?
 
Mkuu wa wilaya na Naibu waziri waliohusika kutandika bakora watu hadharani ni viongozi walioteuliwa na rais Magufuli mwenyewe tena kwa mbwembwe.

Kama aliyewateua (Rais Magufuli) angekuwa hajafurahishwa na hilo jambo, nina uhakika kwa 100% hao wateuliwa wasingedumu kwenye hizo nyanzifa hata kwa siku moja, wangekuwa wameshatumbuliwa within few hours.

Katika hali hii, Katibu mkuu afanye nini?
Sycophant embraces sycophant and genius appreciates genius. Hawa viongozi wenye vurugu kama RC Albert Chalamila au Bashite, Byakwana wa Mtwara, Ole Lengai wa Hai wana akisi hulka na tabia za aliowateua.

Siyo lazima awatume kuleta vurugu mahali lakini wakifanya purukushani kama vile Byakwana alipokuwa Hai ya kuvuruga shamba la Freeman Mbowe, basi Magu anafurahi na anampandisha cheo kuwa RC Mtwara. Sycophant recognize each other by conduct.
 
Hivi wewe unamjua katibu mkuu kiongozi ( Chief Secretary) ni nani?

Nenda kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 60 , utajua katibu mkuu kiongozi ni nani
Usifokee watu JF! Uwe na adabu.
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Sio uongo, we have the most inactive Chief Secretary.
Impact yke kwenye Govt ni wakati wa kuapisha tu!
 
MzeeMwanakijiji itachukua miaka mingi Sana kurejesha heshima yako hapa Jf !😆😆🙄😆
Mkuu huwa tunatazama mada iliyo mbele yetu na si nani kaitoa.
Kama mada ina mantiki, ruksa kutoa maoni yako, kama ni u.pupu wewe saga uwezavyo.
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Mimi huwa nadhani kuwa Katibu Mkuu Kiongozi anahusika zaidi na viongozi wa ngazi za juu zaidi kuanzia Makatibu wakuu kwenda juu, ukiondoa Waziri Mkuu na walio juu yake
 
Ndio Mkuu wa watumishi wote wa umma...walioajiriwa
 
Kwanini Katibu Mkuu wa CCM azungumzie na kuonya watendaji wa serikali? Katibu Mkuu Kiongozi kazi yake ni kutangaza watenguliwa na wateuliwa tu? Yeye siyo sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa umma?

Wakoloni (Wajerumani hasa) walitumia Sana huu utaratibu wa kuchapa watu wazima pale Bomani (kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya). Na watu wazima wanakubali vipi kuchapa na mtu mzima mwingine? Kwa sababu hawataki au wanaogopa kupoteza kazi?
Katika mambo ambayo nilikuwa nachukizwa rohoni nilipokuwa mwanafunzi ilikuwa ni hili la kuchapana badala ya kuelekezana na kupeana elimu. Nashangazwa na mtu mzima kukubali kitendo hiki.

Niwapeni ushauri wengine wataudharau, lakini wananchi haswa wale wenye uwezo waelekee mahakamani kudai fidia za kifedha pale wanapofanyiwa sivyo. Kwa mfano mtu akiekwa rumande bila ya sababu ya msingi, akiachiwa asikubali yaishe arudi tena mahakamani na mahesabu ya kifedha alizopoteza wakati akilala rumande.

Nasema haya ni kwasababu nafahamu fedha za serekali zilivyokuwa ngumu kutoka. Wananchi wanapoanza na mtindo wa aina hii, ni wazi tutafika mahali serekali kuanza kubadili au kuondoa sheria zinazotoa mianya ya kipuuzi ya namna hii. Kwanza naona ni ushamba kweli kila siku ni ziara zisokuwa na kichwa wala miguu! Yaani kufanya ziara ndio kuonyesha utendaji ?
 
Back
Top Bottom