New Rider
Senior Member
- Jun 29, 2021
- 122
- 258
Habari wakuu,
Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.
Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.
Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!
Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa.
Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana.