Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi nilitafutaga sana kipindi fulani ila nikakosa. Watoto wa elifu mbili hawajui hii kituHabari wakuu,
Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.
Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.
Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!
Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa!
Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana
Hapana sina, labda nikuulizie.Yes, exactly!
Nakumbuka hilo jina "KOMBUCHA"
Nilishasahau kitambo!
Kama bado unalo naliomba mkuu!
Hii kitu alikuja nayo shangazi kama sio dingi kutoka mkoani mbeya.
Huu mmea hata Tanzania tunao sababu tuna utajiri wa species nyingi sana za mimea.
Ngoja nikutafutie jina na ukipatikana nitashare na ninyi hapa jina na ikibidi tugawane mbegu ni mzuri sana ile kitu tulikuwa tunaigida sana juice yake.
Tuliweka kwenye zaidi ya vyomba sita tukilina maji yake. Alikuja kuharibu bi mkubwa alipookoka akaambiwa na pastor wake kuwa kile kitu ni mapepo na ni maagano ya mizimu. Yule pastor choko sana hadi leo namind kichizi nikimuona natamani nimlabue makofi na mitama maaana ndie alimchanganya bi mkubwa akaona ule m'mea una uhausiano na maswala ya giza na kumbe ni ukosefu tu wa elimu ya mimea na tiba asili.
Bi mkubwa aliyamwaga yale masufuria yote kimya kimya ndo hadi leo sijuagi pa kuupata.
Ungekuwa unashare na wengine now usingepata shida ya kupata mbegu.
Yaan huo mmea nautafuta kwa gharama yoyote, nakumbuka miaka ya 90 mzee alikuwa anatuletea, unatoa juice juice moja nzuri sana ambayo ni dawa na kinga ya maradhi mbali mbali, ni vizuri ukiwa nao ndani na kuizoesha familia kutumia juice yake badala ya kutumia juice za viwandani.
Exactly ndio hii hii.....
Sifa ya kukaa na ule m'mea ni kushare na wengine usiposhare unakuwa unaukosea.Dah, aha aha haaa!
Pole sana mkuu, inachekesha lakini pia inafurahisha!
Ni kweli hata Mimi kuna wakati lile lichapati lililopokuwa linazaa nilikuwa natenga masufuria mengine na mabakuli makubwa kama yakunawia mikono nayaweka hayo machapati mimea humo! Basi bi.makubwa akawa ana mind sana! Analalamika,"sasa wewe unataka kugeuza vyombo vyote kuwa vya kuwekea hilo lidude lako?!" Alafu sisi tutapikia wapi?!" aha ha haaa! ilikuwa zahama!
Ule mmea ulikuwa mzuri sana aisee,,, mpaka leo nautafuta lakini bado sijaupata!
Mwenye nao tunaomba wandugu!
Unaitwa KOMBUCHA nakumbuka enzi hizo tumeinywa sana juice yake kwa Bibi hukoooo Marangu. Aisee umenikumbusha mbali sana
Kombucha (also tea mushroom, tea fungus, or Manchurian mushroom when referring to the culture; Latin name Medusomyces gisevii[1]) is a fermented, lightly effervescent, sweetened black or green tea drink commonly consumed for its purported health benefits. Sometimes the beverage is called kombucha tea to distinguish it from the culture of bacteria and yeast.[2] Juice, spices, fruit or other flavorings are often added.
Kombucha
Uyoga wa MedusomitsetteYes, exactly!
Nakumbuka hilo jina "KOMBUCHA"
Nilishasahau kitambo!
Kama bado unalo naliomba mkuu!
Sifa ya kukaa na ule m'mea ni kushare na wengine usiposhare unakuwa unaukosea.
Unatakiwa uwe unawakatia watu na kuwagawia usambae. Ni m'mea ambao hautakiwi kumchaji mtu kuupata.