Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kwa sisi tuliuita mkate wa Mecca. Miaka ya nyuma wengi waliotoka Hijja walirudi nao, na ukizaa/ totoa unampatia na mwenzio, ukweli ni kwamba mmea ule ulikuwa ni Tiba. Sasa hivi mahujaji wengi waakiridi waanarudi na vitu vya kippuuzi zikiwemo simu na dildo.
Karibu mkuu.Asante mkuu
Alishapima rabinsia hanaohh pole sana mkuu, hana shida ya figo!?.
Asante mkuu,bila kuchemsha si ndio??Chukua pilipilimanga na binzali..changanya ..anywe asubuhi na jion kwa wiki mbili..utanishukuru badae..
Asante mkuu,nyanya chungu za asili au za kisasa??Achemshe majani ya nyanya chungu anywe asubuhi na jioni siku 21
Hata kama ana shida ya figo anapona
Anywe ikiwa imepoa tho
Za Asili mkuu.Asante mkuu,nyanya chungu za asili au za kisasa??
Daah...umenikumbusha mbali sana kipindi hiko Bi Mkubwa anafanya kazi Bank NBC alikuja nayo hiyo chapati ya ajabu,na tulikuwa tunaihifadhi kwnye chungu halafu juu tunaifunika kwa kitambaa,jioni mama akitoka job wote tunakunywa yale maji yake kuna kipindi tunavizia wakiacha ufunguo wa ndani kwao tunaingia na kuiimimina ile juice na kuinywa ilikuwa na ladha nzuri na tamu sana,mama alisema walipeana huko ofisini kwao na wafanya kazi wenzao wa Banki halafu sikumbuki ilipoteaje maana ilikuwa ni miaka ya 90 kipindi hiko..
Umenikumbusha mbali sana na hiyo Chapati ya ajabu
Ulikuwa ukilishwa chai ya rangi. Juice yake ilikuwa tamu sana. Nami niliupoteza kwa kutoongeza hiyo chai, kwenye hiyo miaka ya 90s.Ulitamba sana kwenye miaka ya mwishoni ya 90'.
Kila mtu akikatia kipande cha ' Fungus' mwenzani ili akaoteshe kwenye maji? Sijui ulipotelea wapi...
Sadakta. Uliwekwa chai ya rangi. Unauweka na baada ya siku kadhaa unamimina kwenye chombo na kunywa. Ikilala asubuhi una kuta utando juu, ndio inaanza hivyo, si lazima ukate kipande.Nakumbuka tulikuwa kunaweza chai ya rangu sio maji
Mkuu; Jaribu University of Dar es salaamHabari wakuu,
Mwishoni mwa mwaka 1998 na mwanzoni mwa miaka 2000 kuna wanajeshi walienda nchini China kuchukua mafunzo ya ngazi Fulani. Baada ya muda Fulani walirejea nchini, walirudi na vitu mbalimbali ikiwemo zawadi, mmoja kati ya wanajeshi hao ambaye tulikuwa na undugu nae, alirudi na mmea fulani mfano wa chapati kubwa sana yenye rangi nyeupe kijivu, ambayo ilikuwa inawekwa kwenye maji, ndani ya sufuria au bakuli kubwa na kujazwa maji, kisha baada ya kama week tatu au mwezi mmoja unamimina Yale maji yake ambayo huwa yamebadirika rangi na kuwa na rangi kama ya chai ya rangi.
Maji hayo huwa na ladha tamu sana kama uchachu fulani au kama ile ladha ya rosela! Wengine uweka sukari au asali kwa kuongeza ladha zaidi. Chapati hiyo ya Kichina ambayo hukuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele, na pia hukuwa na kutoa machapati mengine mengi, kwa mwezi unaweza kuvuna mimea chapati hiyo kama miwili au mitatu. Yaani kimsingi hayo machapati mimea huzaliana kila mwezi au baada ya miezi miwili.
Pia hufa, kwasababu chochote kile kilicho na uhai hufa basi pia mmea huo aina ya chapati hufa, kwasababu huishi ndani ya maji, basi kila baada ya mwezi lazima ubadilishe maji yake na kuongeza mengine! Ukiusahahu na kutokuongeza maji basi mmea huo utaukuta umekauka kabisa na kufa, maji yote yameisha. Mmea huo hula maji tu!
Sasa basi baada ya kupewa mmea chapati huo tulijitahidi kuutunza sana na kufaidi juice yake tamu ambayo pia nasikia ni dawa ya magonjwa kadhaa ya mwili wa mwanadamu, ambayo hutumiwa sana kule China kwa matibabu kadhaa. Kwa bahati mbaya kipindi fulani nnilisafiri kwenda mkoani nikiamini kwamba nitawahi kurudi Dar na kuuhudumia mmea wangu, lakini mambo hayakuwa kama nilivyopanga kwani nilipata dharura na kuchelewa kurudi Dar. Nilipowasili nilikuta ule mmea chapati wangu umeshakauka kabisa kwa kukosa maji na kunyauka kabisa na hatimaye kufa!
Kiukweli nilisikitika sana sana, nimejaribu kuutafuta ule mmea bila mafanikio. Hivyo naomba kama kuna mtu yuko humu Jamiiforums anaufahamu ule mmea, au anao, please naomba sana kwa unyenyekevu anisaidie mbegu yake wanandugu! Naomba sana!
Zile ni fungus. Hivyo ukimega kakipande kadogo ukaweka ktk chombo kingine ina- multiply.Huu mmea sidhani kama una mbegu, kinachofanyika ni kuwa kila unapotanuka ukikata kipande na kutia kwenye maji na chenyewe kinakua, kwahiyo cha muhimu ni kufanya timing kila unapokaribia kucover eneo lote la chombo chako unakata kidogo unatumbukiza kwenye chombo kingine chenye maji. Kifupi sijui kama kuna mbegu na sijui unapatikana wapi,ila hata mimi niliwahi kupewa na rafiki,nikakaa nao karibu miezi 2, nikajisahau ukawa ndio mwisho wake.
Ukiupata rudi hapa utugawie. Mimi niliutumia miaka ya 80Duh!
Kweli ni mmea mzuri sana, kuupata ni adimu sana, nimejitahidi sana kuutafuta humu mtaani bila mafanikio! Nikaona bora nije humu kwa waungwana najua sitakosa hata mawazo ya wapi pa kuupata!
Maana penye wengi hapaharibiki neno!