Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Huu mmea uliwahi kuniponya Athma nikiwa binti mdogo...Nilikuwa nikibanwa Mara kwa Mara na kutumia vidonge vya hospital na zile dawa za ku inhale lakini Mambo yalikuwa mperampera, Kama kawaida ya Tanzania Mambo ya milipuko Ni mengi,Mara Ngetwa3,Mara Ngoka11,Mara mayai ya kwale,Mara Kikombe Cha Mwaisapile...Basi ikatokea hili lichapati ,hii kitu nilikunywa Kama miezi miwili Nakumbuka mama yangu aliyapanda kwenye madishi,Basi nakunywa Kama juisi daily....ninachokumbuka baada ya hapo sijabanwa Tena kifua mpaka Sasa nimezeeka....Ila linachefua ukiliona Kama miutelezi gani sijui🥴

Aiseee,,, hongera sana!

Ule mmea kipindi tunautumia magonjwa yalikuwa hayakatizi kabisa!

Hapo kwenye ngetwa eleven na ngokwa umenikumbusha mbali sana! Enzi hizooo!
 
Aiseee,,, hongera sana!

Ule mmea kipindi tunautumia magonjwa yalikuwa hayakatizi kabisa!

Hapo kwenye ngetwa eleven na ngokwa umenikumbusha mbali sana! Enzi hizooo!
😂😂😂Hawa wahuni wa Ngetwa3 walipiga hela za Wananchi....Ule mmea bwana ulikuwa kinywaji poa Sana.
 
vipi unaongeza nguvu? maana sie wabongo hapo tu

utasambaa nchi nzima mpaka ndani ndani huko

Aha ha haaa!

Kwenye hili sifahamu mkuu, lakini unatibu na kuimarisha kinga mwili na utendaji wa mfumo wote wa mwili, huenda (may be) kwa njia Fulani unaweza kuwa unasaidia functional ya eneo hilo!
 
Tumekunywa sana juice ya hii kitu tulipokuwa wadogo. Mama alikuwa akitupa kila siku. Umenikumbusha mbali sana mkuu. Sijui iliishia wapi hii kitu jamani
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Mkuu tangu 1998 una uraibu mpaka leo 22?UMENIMIX BRAIN

Aha ha haaa! Acha tu mkuu,

I'm addicted, hata hapa tunaposimuliana nahisi ule uchachu wake kwenye ulimi!

Natamani kulipata hata leo hii!
 
Daa zamani sana huo mmea niliuona. Kuna jamaa alikuwa nao kama sikosei alikuwa anauita "mybao/mibao/maibao". Si na hakika na matamshi ya hilo jina ila mnaweza kuanzia hapo. Enzi hizo kila tukimuona jamaa ametoka kazini akiingia tu kwake kabla hajakaa tumeshafika na vikombe vyetu vya plastiki kujimiminia ilikuwa kama chai ya rangi hivi.
Maibao tea tressures.....black tea fungus....
 
Back
Top Bottom